Saturday, 4 February 2017

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 33.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018


Na: Mwanakheri Ally

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, limepitisha mapendekezo  ya mpango wa bajeti kiasi cha Tsh. 33,499,533,375 kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kati ya fedha hizo ni Tsh.8, 854,027,476 kwa ajili ya ruzuku ya miradi ya maendeleo, Tsh.835,764,000 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida, Tsh 20,828,509,629 mishahara na  Tsh. 2,931,240,000 ni mapato ya ndani.

Vipaumbele vya mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/2018 vimegawanyika katika sekta mbalimbali ambazo ni kuboresha huduma za jamii kwenye sekta ya maji, kukarabati barabara, ujenzi wa miundombinu kwa shule za msingi na sekondari na uboreshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji.

Sambamba na mapendekezo  hayo ya bajeti Halmashauri imewasilisha ombi maalumu lenye jumla ya Tsh 3,400,000,000.00 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya kisasa na tayari eneo wa ajili ya ujenzi wa mradi huo limeishatengwa lenye ukubwa wa ekari 60.

Baraza limetilia mkazo suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuhakikisha mianya ya ukwepaji kodi inadhibitiwa ili miradi iliyopangwa kutekelezwa kupitia vyanzo vya ndani iweze kukamilika, Aidha Baraza la Madiwani limeiomba serikali kuleta fedha za ruzuku kama ilivyopangwa ili kufanikisha malengo ya Halmashauri.

Mkurungenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Andrea Chezue akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmshauri Rashidi Nakumbia aweze kufungua kikao maalumu cha Baraza la Halmashauri cha kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Joseph Mkrikiti na wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Rashidi Nakumbia akiwa anafungua kikao maalumu cha Baraza la Halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka 2017/2018(kulia) wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe.Joseph Mkirikiti

Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika utulivu wakisikiliza Mkurugenzi Mtendaji akiwasilisha Bajeti mbele ya Madiwani na wataalamu kutoka Halmashauri ya Ruangwa

Diwani wa kata ya Makanjiro Saidi kawale akiwa na diwani wa viti maalumu Zuwena Kitatichingi wakiwa wanasikiliza mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/2018

Mwandishi wa mkutano Bahati Kasambano akiwa anasikiliza na kuandika yanayozungumzwa na Mkurugenzi

Afisa Mipango Thomas Luambano akiwa na Afisa Elimu Msingi Selemani Mrope wakifuatilia uwasilishwaji wa bajeti

Diwani wa kata ya chienjele Rashidi Nnuduma akiwa na Diwani wa kata ya luchelegwa Omari Chande wakiwa wanafuatilia kwa umakini mchakato wa uwasilishwaji wa mapendekezo ya bajeti ya  mwaka 2017/2018

Afisa Utumishi wa Halmshauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo ya bajeti 2017/2018
Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri Andrea Chezue pembeni yake Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbia(kulia) Mkuu wa Willaya Joseph Mkirikiti (mwisho) Kaimu Mwenyekiti Shabani Kambona wakiwa wanasikiliza hoja za madiwani

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri katika kikao Maalumu cha Baraza la Halmshauri cha Kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018
Wajumbe waliohudhuria kikao maalumu cha baraza la Halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Dr Japhet Simeo akiwa anawasilisha majibu ya wajumbe waliopima Afya jana kabla ya kuanza kikao maalumu cha baraza la halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018

Waheshimiwa Madiwani wakiwa wapo nje ya ukumbi wa Rutesco kilipofanyika kikoa baada ya kuupitisha mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/2018


Friday, 3 February 2017

MKURUGENZI WILAYA YA RUANGWA AWAHIMIZA MADIWANI NA WADAU WENGINE WA ELIMU KUKEMEA UTORO MASHULENI

Na: Mwanakheri Ally

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa Ndg. Andrea Chezue amewaomba Waheshimiwa Madiwani wamsaidie katika maeneo yao kutokomeza utoro mashuleni na kusaidia kurudisha Watoto walioacha shule kurudi shuleni kama mwanzo.

Alisema ni wajibu wa Halmshauri na Madiwani kuwaunga mkono Idara ya Elimu ili wafanikiwe  kumaliza tatizo la utoro sugu na utoro wa reja reja kwani hilo si jukumu la Watu wa Elimu tu ni jukumu la kila Mwananchi wa Wilaya ya Ruangwa.

Ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichoanza tarehe 1 mpaka tarehe 2 Februari 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa

Aidha, Mkurungezi Mtendaji alisema sambamba na kutokomeza utoro  Halmshauri imejipanga kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa ndani ya Wilaya mpaka kufikia Juni 2017 atakuwa amemaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyoitajika

Vilevile aliwataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi ili kuweza kufanikiwa katika malengo yaliyowekwa ya kuwa na Ruangwa yenye maendeleo, kwani inawezekana kama kutakuwa na ushirikiano.

Mkurugenzi aliwaomba  Madiwani ambao katika kata zao kuna miradi iliyoanzishwa na Wananchi basi waweze kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi ili, Halmashauri iweze kutia nguvu zake katika kumalizia miradi hiyo kama ilivyoada.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Rashid Nakumbi aliwaambia wajumbe wa Baraza la Madiwani bila ushirikiano hakuwezi kuwa na maendeleo hivyo inapaswa wataalamu wa Halmshauri na Madiwani washirikiane hii itasaidia kuwa na kasi na kuleta maendeleo katika Wilaya ya Ruangwa

Pia aliwataka Madiwani na Wataalamu wa Halmshauri kujitoa kwenye masuala ya kupima Afya  kwani hii itasaidia kuwashawishi Wananchi kujitoa kwa hiari kwenda kupima Afya, kabla ya kikao kuanza cha Baraza la Madiwani, Wajumbe walipata nafasi ya kuanza kupima Afya zao kwa hiari.

Naye, Diwani wa Chibula Mhe.Omari Songea kwa niaba ya wa Madiwani wengini alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa jitihada anazozionesha za kuifanya Mji wa Ruangwa kuwa na maendelea na kumuahidi kutoa ushirikiano kama inavyotakiwa ili kuweza kufikia malengo.

Mkurugenzi mtendaji Adrea Chezue akiwa anamkaribisha mwenyekiti katika Rashidi Nakumbia( mwisho) Makamu Mwenyekiti Shabani Kambona
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye Baraza la Halmshauri

Diwani wa kata ya Matambarare Omari Li akiwa anasoma kwa umakini taarifa

Mwandishi wa Mkutano Bashiru Kauchumbe akiwa anamsikiliza muwasilisha mada

Afisa utumishi wa Halmashauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akiwa anasoma kablasha alilokabidhiwa(kushoto) Mhandisi Fransis Kakama

Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika hali ya utulivu wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmshauri akiongea

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Maji na Afya mh  EliasNkane




Afisa Elimu Msingi akiwa anajibu Hoja za Madiwan(kushoto) kaimu muweka Hazina gervas Bidogo

Waandishi wa Mkutano(kushoto)Bahati Kasambano(kulia) Bashiru Kauchumbe

Afisa Utumishi  Festo j Mwanagalika akiwa anajibu hoj zaa kutoka kwa Diwani

Kaimu Afisa Elimu Anna Nasu akiwa anajibu hoja zinazohusiana na masuala ya Elimu iliyoulizwa na Madiwani

Wataalamu kutoka Halmashauri wakiwa wanasikiliza mada zinazowasilishwa

Waheshimiwa Madiwani wakliwa wananyoosha mikono ili wapate nafasi ya kuuliza maswali yao.

Waheshimwa Madiwani wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wakisikiliza hoja zinazowasilishwa

Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa kwenye Baraza wakisikiliza hoja zinazowasilioshwa






BARAZA LA WAFANYAKAZI WILAYA YA RUANGWA WAAFIKI BAJETI YA SHILINGI BILIONI 33.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Na Mwanakheri Ally

Baraza la Wafanyakazi Wilaya ya Ruangwa limeafiki  bajeti iliyopangwa na Halmashauri ya Wilaya  ya mwaka 2017-2018 ambayo ni kiasi  cha Shilingi Bilioni 33.4 baada ya kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatia kuwasilishwa kwa bajeti hiyo.

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya muwasilisha mada Afisa Mipango Joram Mbiha kuwasilisha bajeti hiyo kama ilivyopangwa na Halmashauri kwa Wajumbe wa Baraza hilo la Wafanyakazi, na Wajumbe hao kupata nafasi ya kutoa hoja zao na kupatiwa majibu na Wakuu wa Idara na Vitengo waliohudhuria kikao hicho.

Hayo yalifikiwa muafaka wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililoshirikisha Wajumbe mbalimbali kisheria, kikao hiko kilifanyika katika ukumbi wa soko la Kilimahewa mjini Ruangwa

Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ali Bakari akiwa anafanya ufunguzi wa Baraza hilo tarehe 30/1/2017 kulia Mwenyekiti wa Baraza........

Afisa Mipango Joram MBiha akiwasilisha mada mbele wa wajumbe wa Baraza

Wajumbe wa Baraza wakiwa wanasikiliza kwa umakini mada inavyowasilishwa na Afisa Mipango


Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akijibu hoja iliyoulizwa na mjumbe.(kushoto) Mwenyekiti wa Baraza Jafarani Mkangumbe (kulia Afisa Mipango Joram Mbiha

Wajumbe wa Baraza wakiwa wanasikiliza kwa umakini mada inavyowasilishwa na Afisa Mipango
Afisa Elimu Msingi Selemani Mrope akitoa ufafanuzi wa hoja iliyoibuka kutoka kwa katibu wa Baraza ndugu Ali Seleman

Mjumbe Amanzi Ndeo ambaye ni Afisa Kilimo Kata ya Nandagala akiuliza swali

Mkuu wa Idara ya Maeandeleo ya Jamii Grace Mwambe akijibu hoja ya Afisa Kilimo wa Nandagala

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Jafarani  Mkangumbe akiwa anateta jambo na Katibu wake bwana Ali Bakari Katoto

Sekretarieti ikiwa inasikiliza hoja wakati baraza likiendelea( kulia) Tunu Naftari na
(kushoto) Avodi Daniel

Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Ruangwa Baltazar Lukanga akiwasilisha hoja yake wakati wa Baraza hilo



Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akijibu hoja ya Katibu wa CWT wakati wa Baraza la Wafanyakazi.

Wednesday, 1 February 2017

MGANGA MKUU WILAYA YA RUANGWA AWAHAMASISHA WANANCHI KIJIJI CHA CHIMBILA 'A' KUJITOKEZA NA KUENDELEZA UJENZI WA ZAHANATI


Na: Mwanakheri Ally

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Dr. Japhet Simeo  amewahamasisha Wananchi wa Kijiji cha Chimbila 'A' na Manokwe kuanza taratibu za ujenzi wa boma za Zahanati kama walivyoagizwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake Wilayani hapo iliyofanyika mwezi mliopita.

Dr. Simeo aliwaambia Wanakijiji wa  Chimbila 'A' wajitahidi  waanze ujenzi wa Zahanati kwa nguvu zao kwani kuanza kwao kwa ujenzi itawasaidia kupata msaada kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na sikutegemea kusubiria Serikali ije iwaanzishie ujenzi.

Hayo aliyaeleza wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa ujenzi wa Zahanati uliofanyika katika ofisi ya Serikali ya kijiji cha Chimbila 'A'.

Mganga Mkuu aliwaambia kama watajitahidi kuwa na kasi katika suala la ujenzi wa Zahanati basi mwezi wa Nane mwaka 2017 Zahanati hiyo itaweza kufunguliwa kama watakuwa wamemaliza ujenzi.

Aidha, Dr. Simeo alitumia nafasi hiyo kuwapa pole Wanakijiji wa Chimbila 'A' kwa kuuguliwa na Diwani wao Daniel Mtawa  na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu kwao.

“kuweni na uvumilivu kwani hiki nikipindi kigumu kwenu ila zidisheni dua na maombi kwani Mh Diwani anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Muhimbili” alisema.

Mganga Mkuu Dokta Japhet Simeo akiwa katika kijiji cha Chimbila 'A' katika mkutano wa Kijiji wa kuhamashisha ujenzi wa Zahanati.


Mjumbe wa SerIkali ya Kijiji cha Chimbila 'A' akiwa anatoa mchango wake wa mawazo ni vipi wataweza kujenga Zahanati hiyo
Wanakijiji wa Chimbila 'A' wakiwa wanamsikiliza kwa umakini Mganga Mkuu
Wananchi wa Chimbiila A wakiwa katika mkutano wa kijiji wa uhamasishaji wa ujenzi wa Zahanati




Viongozi wa Kijiji cha Chimbila wakiwa wanaelekea kwenye eneo lililochaguliwa na wananchi kwa ujenzi wa zahanati
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akiwa anaongea na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Manokwe wakati wa kukagua eneo litakalojengwa zahanati katika kijiji hicho

Eneo la Kijiji cha Chimbila A linalotegemewa kujengwa Zahanati
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akiwa anaongea na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chimbila A wakati wa kukagua eneo litakalojengwa zahanati katika kijiji hiko
Viongozi wa Serikali ya kijiji Manokwe wakiwa wanaangalia eneo la kufanya ujenzi wa Zahanati kijijini hapo

Mtendaji wa Kijiji wa Chimbila A akiwa na Wajumbe wa kijiji hiko wakimuonesha Mganga Mkuu eneo wanalotaka kujenga zahanati 

Eneo la Kijiji cha Chimbila A linalotegemewa kujengwa Zahanati lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 4


Mganga Mkuu akiwa na viongozi wa kijiji cha Chimbila wakiwa wanaangalia eneo la ujenzi wa Zahanati huku mganga mkuu akiwa anawapa mbinum za kuanzisha ujenzi