Wednesday 1 February 2017

MGANGA MKUU WILAYA YA RUANGWA AWAHAMASISHA WANANCHI KIJIJI CHA CHIMBILA 'A' KUJITOKEZA NA KUENDELEZA UJENZI WA ZAHANATI


Na: Mwanakheri Ally

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Dr. Japhet Simeo  amewahamasisha Wananchi wa Kijiji cha Chimbila 'A' na Manokwe kuanza taratibu za ujenzi wa boma za Zahanati kama walivyoagizwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake Wilayani hapo iliyofanyika mwezi mliopita.

Dr. Simeo aliwaambia Wanakijiji wa  Chimbila 'A' wajitahidi  waanze ujenzi wa Zahanati kwa nguvu zao kwani kuanza kwao kwa ujenzi itawasaidia kupata msaada kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na sikutegemea kusubiria Serikali ije iwaanzishie ujenzi.

Hayo aliyaeleza wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa ujenzi wa Zahanati uliofanyika katika ofisi ya Serikali ya kijiji cha Chimbila 'A'.

Mganga Mkuu aliwaambia kama watajitahidi kuwa na kasi katika suala la ujenzi wa Zahanati basi mwezi wa Nane mwaka 2017 Zahanati hiyo itaweza kufunguliwa kama watakuwa wamemaliza ujenzi.

Aidha, Dr. Simeo alitumia nafasi hiyo kuwapa pole Wanakijiji wa Chimbila 'A' kwa kuuguliwa na Diwani wao Daniel Mtawa  na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kipindi hiki kigumu kwao.

“kuweni na uvumilivu kwani hiki nikipindi kigumu kwenu ila zidisheni dua na maombi kwani Mh Diwani anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Muhimbili” alisema.

Mganga Mkuu Dokta Japhet Simeo akiwa katika kijiji cha Chimbila 'A' katika mkutano wa Kijiji wa kuhamashisha ujenzi wa Zahanati.


Mjumbe wa SerIkali ya Kijiji cha Chimbila 'A' akiwa anatoa mchango wake wa mawazo ni vipi wataweza kujenga Zahanati hiyo
Wanakijiji wa Chimbila 'A' wakiwa wanamsikiliza kwa umakini Mganga Mkuu
Wananchi wa Chimbiila A wakiwa katika mkutano wa kijiji wa uhamasishaji wa ujenzi wa Zahanati




Viongozi wa Kijiji cha Chimbila wakiwa wanaelekea kwenye eneo lililochaguliwa na wananchi kwa ujenzi wa zahanati
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akiwa anaongea na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Manokwe wakati wa kukagua eneo litakalojengwa zahanati katika kijiji hicho

Eneo la Kijiji cha Chimbila A linalotegemewa kujengwa Zahanati
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akiwa anaongea na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Chimbila A wakati wa kukagua eneo litakalojengwa zahanati katika kijiji hiko
Viongozi wa Serikali ya kijiji Manokwe wakiwa wanaangalia eneo la kufanya ujenzi wa Zahanati kijijini hapo

Mtendaji wa Kijiji wa Chimbila A akiwa na Wajumbe wa kijiji hiko wakimuonesha Mganga Mkuu eneo wanalotaka kujenga zahanati 

Eneo la Kijiji cha Chimbila A linalotegemewa kujengwa Zahanati lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 4


Mganga Mkuu akiwa na viongozi wa kijiji cha Chimbila wakiwa wanaangalia eneo la ujenzi wa Zahanati huku mganga mkuu akiwa anawapa mbinum za kuanzisha ujenzi