Sunday, 31 December 2017

Tafuteni Takwimu Mpya, Waziri Mkuu AagizaNA MWANDISHI WETU

Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Kilimo kutoka mikoa inayolima korosho, washirikiane kupata takwimu mpya za wakulima wa zao hilo.

Ametoa agizo hilo leo mchana jumapili, Desemba 31,2017) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya milioni 10 msimu wa 2017/ 2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

“Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa twakimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu” alisema Waziri Mkuu

“Afisa kilimo wa Wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo ana miche mingapi, na ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani “alisema.

Pia nilikwisha waagiza maafisa ushirika na viongoi wa vyama vya msingi(AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa kijiji, kwasababu wao wanaidadi kamili za watu    wanaowaongoza”alisema.

“Ninaimani tukifanya hili tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa nauwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao”alisisitiza

Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha kugawa miche kwa wakulima 10 kutoka Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwakilisha wenzao

 Mapema kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu za pili iliyotokana na vikonyo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mche mpya wa mkorosho Bi. Mwanahamisi Saidi, mkazi wa Kilimahewa, baada ya kuzinduzi kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 Mjini Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho  ,mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Hassani Jarufu wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa Miche Mipya ya Korosho kutoka kwa Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Domina Mkaranga, Wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018 mjini Ruangwa

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiangalia Mche Mpya wa Korosho, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya mikorosho alipotembelea vitalu vya miche hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue


Miche ya Mikorosho Mipya na bora iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa