Friday 14 July 2017

Waziri Mkuu Akabidhi Pikipiki 49 Kwa Vijana Wa Ruangwa



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.



Amekabidhi pikipiki hizo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Likangara.

Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.

Amesema vijana wanaoendesha pikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.

“Ukiendesha pikipiki lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Nandagala na kuridhishwa maendeleo yake.

Amesema kukamilika kwa majengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma za afya kwa mama na mtoto. Pia itawapunguzia kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati alipo tembelea na kukagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi seti ya tv na king’amuzi chake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP.  Rajab Nyange,  wakati akikagua ujenzi wa Gereza la Wilaya Ruangwa,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi


                             
PMO_1616 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Ruangwa Mjini katika mkutano wa hadhara aliyo uitisha,  akiwa kwenye ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Liwale Zuberi Kuchauka, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani

Add captio1692 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi Hamida Abdallah katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazin


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Lindi Manispaa,  Selemani Kaunje, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi
Add captionWaziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Nachingwea Elias Masala, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira na jezi Diwani wa Kata ya Luchelegwa, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017


Add captionWaziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi king’amuzi chake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue,wakati akikabidhi pikipiki kwa vijana, kiwa kwenye ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea pikipiki aina ya SANLG kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Alan Lin katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Wauza Pikipiki na spea Taifa Martin Mbwana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi

Add captionWaziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi pikipiki kwa niaba ya waendesha bodaboda 49 wa Wilaya ya Ruangwa waliokabidhiwa pikipiki Juma Selemani, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikaz

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waendesha bodaboda waliokabidhiwa pikipiki 49 kwa mkopo, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,  akiwa kwenye ziara ya kikazi