Thursday, 25 May 2017

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour Awaasa Wananchi wa Ruangwa Katika Kukuza Uchumi wa ViwandaWakulima Wilayani Ruangwa, wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira ya kufikia na kufanikiwa mpango wa serikali wa kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda.

Wito huu alitolewa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Amour Hamad Amour, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nandalaga alipotembelea shamba na kiwanda cha kukamua mafuta ya zao la Alizeti.

Aliwataka wananchi kuongeza bidii katika sekta ya kilimo ambayo itapelekea kuwa na viwanda kwa wingi kwasababu kilimo na viwanda ni vitu viwili vinavyotegemeana. Wakulima  wanao wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kuifanya nchi kufikia uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.

Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa ni wakulima, hivyo wanayo nafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanazofanya. Amour, alifananua kuwa ili wakulima waweze kufanikisha azima hiyo wanapaswa kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye kile cha viwanda.

"Badala ya kuuza mazao ghafi, wakulima wanapaswa kufikiria kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha na mtakuza uchumi wenu wenyewe" alisema Amour.

Aidha alisema kama Tanzania ikifanikiwa kuwa nchi ya viwanda, basi kutakuwa na faida nyingi kama kuongeza ajira ya mtu mmoja mmoja, kukuza uchumi wa taifa na kubadilisha mfumo wa maisha kutoka katika hali duni mpaka kuwa na hali nzuri.

"Lengo ni  kuona hadi kufika mwaka 2025, wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini na kufikia uchumi wa kati. Ila kufanikiwa katika suala la viwanda inabidi wananchi wakazane kufanya kilimo kwa wingi na wabadili mbinu za kilimo" alisema Amour.

Vile vile alimtaka Mkuu wa Wilaya kuweka mkakati wa kuzuia matumizi mabaya ya chandarua kwasababu wananachi wanabadili matumizi ya vyandarua. Badala ya kufunga kwenye vitanda vyao wanafunga kwenye bustani zao. Hivyo aliwataka wananchi kuwa na fikira za kubadilika na si kuishi kwa mazoea.

Wakati huo huo, Mkimbiza Mwenge , Fredirick Joseph Ndahani, alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa mapokezi mazuri waliyoyapata  na kusisitiza Halmashauri kuongoza jitihada za kusaidia vikundi vya wajasiriamali na hasa vijana.


Mkuu wa Wilaya Lindi  Shaibu Issa Ndemanga akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Rukia Muwango

Mkimbiza Mwenge Uhuru Bahati Mwaniguta Lugodisha akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru Kitaifa

Mkimbiza Mwenge  Bahati Lugodisha akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Talawa Twaha Mpembenwe

(katikati)Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour(kushoto kwake)Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue na (kulia kwake)Kaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango (kushoto kwake) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe

Wakuu wa Idara wakiwa wanausubiri Mwenge wa Uhuru  baada ya kuwasili katika uwanja wa shule ya msingi Nandagala

Katikati)Kaimu Mkuu wa Idara ya Tehama Jitetete Mbonde (kushoto kwake) Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bihuria Shabani na( kulia) Mkuu wa idara ya Utawala Festo j Mwangalika

Wananchi wakiwa wanasubiri Mwenge wa Uhuru ufike katika kijiji cha Ipingo

Mkimbiza Mwenge Fedrick Joseph Mdahani akiwa anatoa maelezo katika banda la kuku Ipingo


Mkimbiza Mwenge Ndahani akiwa anatoa maelekezo ya vifungashio vya sabuni kwa wakikundi ipigo

Katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue (kulia) Mkimbiza mwenge Bahati Lugodisha na (kushoto) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Hawa Mchopa wakiwa wanasikiliza burudani kutoka kwa mwanafuzni mwenzao

Wananchi wakiwa katika uwanja wakamsikiliza Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiongea


Mwenge wa uhuru Kitaifa ukiwa katika Shule ya Hawa Mchopa

Mkimbiza Mwenge Bahati Mwaniguta Lugodisha akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Nangumbu


Kikundi cha wanawake wakiwa na mafuta waliokamua ya alizeti


Bwana shamba wa Nandagala Amanzi Mbeo akiwa anatoa maelezo ya shamba la alizeti

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa anazungumza na wanakijiji cha Nandagala baada ya kutembelea shamba na kiwanda cha kukamua alizeti

Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiwa anaweka zege katika ndoo kwenye Zahanati ya Nandagala kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili

Wakimbiza Mwenge wakiwa wanaagalia jinsi ya kutega mbu

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anagawa chandarua kwa mwanakijiji wa Nandagala


Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anaangalia jinsi amplifaya inavyofanya kazi iliyotengenezwa na kikundi cha Mkuti


Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za lami mjini Ruangwa

Mhandisi wa Ujenzi Mashaka Nalupi akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara za lami mjini RuangwaKaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango akiwa anatoa maelekezo kabla ya kwenda Nachingwea kukabidhi

Mkimbiza Mwenge Fredirick Joseph Ndahani akitoa neno la shukurani baada ya kuwasili Ruangwa mjini

(katikati)Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa ameishakabidhiwa Wilaya ya Nachingwea(kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Bakari Mohamed Bakari

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akimkabidhi Mwenge wa Uhuru  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akiwa anatoka kukabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Nachingwea

Thursday, 18 May 2017

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Awataka Wananchi Kumuunga Mkono Waziri Mkuu Katika Kushiriki Shughuli za Maendeleo


NA Mwanakheri Ally

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ,Mhe, Rashidi Nakumbya amewata wakazi wa Wilaya ya Ruangwa kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa.

Amewataka wananchi kufanya kazi bega kwa bega na Mhe, Waziri katika kuleta maendeleo katika wilaya ya Ruangwa kwa Kushiriki shughuli za kimaendeleo alisema,maendeleo katika wilaya hii ni jukumu la kila mkazi wa eneo hili.

Alisema haya wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Mei 17 mpaka 18 katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa.

Mhe, Nakumbya aliwataka waheshimiwa Madiwani wa Wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kuhamasisha wananchi wao katika kuchangia kufanya shughuli za kimaendeleo katika kata zao.

“Nisiwe mchoyo wa kushukuru kama watu wamefanya vizuri basi ni wajibu wangu kuwapa pongezi, nawapongeza wananchi wa kata ya Nachingwea na Ruangwa kwa kazi nzuri ya waliyoifanya ya kujitolea katika ujenzi wa shule ya mpya ya Sekondari Kassim Majaliwa” alisema Mhe, Nakumbya.

Aidha alimtaka Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue kuongea vizuri na  wachimbaji wa visima waliopo katika wilaya kwa ajili ya kuchimba visima, waanze na shule ya sekondari mpya kwani ikianza bila maji itakuwa shida kwa wanafunzi na walimu.

“Shule yetu ni nzuri sana ila itaendelea kuwa nzuri pale maji yatakapopatikana, maji ni uhai hatuwezi kuanza kutumia shule hiyo bila kuwa na maji kwani  itakuwa mateso kwa watoto wetu wakike pamoja na walimu ” alisema Mhe, Nakumbya.

Pia Mhe, Nakumbya aliwataka wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanasafisha mashamba yao ya mikorosho ili mgao wa dawa ya kupulizia utakapofika  kila Mkulima aweze kupata dawa hiyo na pia alisisitiza itazingatiwa zaidi kwa wale ambao wenye mashamba masafi.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mhe, Eliasi Nkane aliwaomba wakuu wa shule na Afisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha wanafuatilia sheria ya mtoto anayeaacha kwani watoto hawa wasipochukuliwa hatua inasababisha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule.

“Zama za sasa imepunguza sana idadi ya watoto wa mitaani hivyo walimu na maafisa elimu ni wajibu wao kuwachukulia hatua watoto hawa wanaocha masomo ili tuzidi kutokomeza suala la watoto wa mtaani” alisema mhe Nkane.

                              


(kushoto)Diwani wa kata ya Namichiga Mikidadi Mbute akiwa anasikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri akizungumza na (kulia) Diwani wa viti maalumu


Mhe, Diwani wa kata ya Mbwemkuru Selemani Likuche akiwa anawasilisha taarifa ya kata yake

Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japheti Simeo akiwa anajibu hoja

Wataalamu kutoka halmashauri wakiwa wanasikiliza uwasilishwaji wa taarifa za kata na Madiwani

Wakuu wa idara na vitengo wakiwa wanasikiliza uwasilishwaji wa tarifa

Waheshimiwa Madiwani wakiwa wanafuatilia kwa umakini mkutano wa Baraza

Mhe, Diwani wa kata ya Luchelegewa Jaffari Chande akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji


Waheshimiwa wakiwa wanasikiliza kwa umakini Mkutano  ukinaendelea

(katikati)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Rashidi Nakumbiya (kulia kwake) Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Shabani na kushoto kwake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri

Mkuu wa Idara ya Fedha Frank Chonya akiwa anajibu hoja iliyoulizwa na Mhe, DiwaniDiwani wa Viti Maalum Paulina Mmuya akiwasilisha Taarifa ya kata ya Nachingwea

Diwani wa kata ya Ruangwa Mhe, Omari Pendeka akiwasilisha taarifa ya kata yake

Afisa Elimu Sekondari Bihuria Shabani akijibu hoja iliyouliza


Mhe, Diwani wa Viti Maalumu Amina Naenje akiwasilisha taarifa ya kata ya Mnacho

kushoto) Mwandishi wa Mkutano Bashiri Kauchumbe akiwa anafuatilia mkutano unavyoendelea

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lawrence Mapunda akijibu hoja iliyotoka kwa Mhe, Diwani


Mwenyekiti wa Halmashauri akitoa ufafanuzi kwa wajumbe na waheshimiwa Madiwani


Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Baraza la Madiwani wakifuatilia mjadala iliyokuwa inaendelea


(kushoto) Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani na kulia kwake mkuu wa idara ya Mipango


Kiamu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Moses Mkwesela akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sheria


Diwani wa kata ya Nandagala  Chikongwe akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu


Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbya akifunga Mkutano wa Baraza