Thursday 20 April 2017

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Ya Wilaya Kukagua Maendeleo ya Miradi ya Kijamii

NA Mwanakheri Ally

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Mbekenyera Rashid Nakumbiya amewataka watendaji wa serikali za vijiji kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha tofauti za vyama.

Alisema jukumu la kiongozi kuitumikia jamii iliyompigia kura ni wajibu wa kila mmoja wao, aliwakata kujenga umoja kwa kuangalia masilahi ya wananchi waliowapiga kura kwa ajili yao.

Aliyasema hayo wakati akiongea na watendaji wa serikali za vijijini wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya kamati ya fedha Uongozi na Mipango,Iliyofanyika katika maeneo ya Chikundi, Namichiga, Namilema na Ruangwa mjini.

Mwenyekiti alisema ushirikiano ni muhimu kwa pande vyama vyote vya kisiasa katika kuleta maendelea na wasifanye vyama vikawaga wao wote ni watanzania na sifa ya mwafrika ni umoja na ushikamano

Aidha aliuomba uongozi wa Halmashauri kuwafanyia utaratibu wa kupata tenki za maji katika shule ambazo zinauhaba wa maji ili waweze kuvuna maji ya kutumia wanafunzi kipindi cha ukame.

Hata hivyo Mh.Nakumbiya alitoa pongezi  kwa uongozi wa halmashauri kwa kuweza kuwasaidia wanakijiji walioonesha nguvu zao na kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata zao.

Pia alitoa pongezi za kipekee kwa viongozi wa serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha zoezi la kuanzisha miradi kama zahanati na shule zao na kuwaomba wawe na moyo huo huo kwani maendeleo katika kijiji yanaanzwa kuletwa na wahusika wa eneo

 Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango walitembelea mradi wa zahanati ya kijiji cha chikundi, ujenzi wa vyumba vya madarasa Namichiga sekondari, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namileya na barabara za lami za mjini Ruangwa.



(Kushoto)Mwenyekiti wa kamati ya fedha, uongozi na mipango Rashidi Nakumbya akiwa anaangalia mafundi wanaendelea na kazi

Mwandishi wa mkutano Bashiru Kauchumbe akitambulisha msafara aliongozana nao

Afisa Mtendaji wa kata ya Mandawa Masunga Salida akiwa anatambulisha uongozi wa kijiji waliokuja kukutana na wanakamati


Mjumbe wa serikali ya kijiji akitoa shukurani kwa mwenyekiti wa kamati kwa ujio wao katika kjijiji cha Chikundi


(kushoto)mwenyekiti wa kamati akiwa anasikiliza risala kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji(kulia)diwani wa kata ya Nandanga Shabani Kambona



Mwenyekiti wa kamati akiwa anapokea risala iliyoandaliwa na serikali ya kijiji baada ya kusomwa mbele yake na mwenyekiti wa kijiji Muhidini Tumaini

(kushoto)Afisa Mipango Thomas Luambano akiwa anamsikiliza mh. Mwenyekiti (pili) Rashidi Nakumbya akitoa maneno yake baada ya kusomewa risala

Mh. mwenyekiti akiwa anakagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Namichiga(kushoto) mwenyekiti wa bodi ya shule

Moja ya mradi uliotembelewa na wanakamati wa vyumba vya madarasa namichaga sekondari

(kulia) Mkuu wa shule Ya Namichiga akiwa ameongozana na Afisa Mipango wa Wilaya

Mwenyekiti wa Kamati akiwa anaangali ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Namichiga

Wanakamati wa fedha, uongozi na mipango wakiwa wanakagua karo la choo katika shule ya Namichiga



Mtendaji wa Kijiji cha Namichiga Vicent Mapunda akikabidhi Risala yake kwa Mwenyekiti wa Halmashauri

Mh. Diwani wa kata ya Nanganga Shabani Kambona akiwa anatoa ushauri wake kwa serikali ya kijiji

Mh. Diwani ya kata ya Chienjere Rashidi Mnunduma akiwa anaongea na serikali ya kijiji na wanakamati


Diwani wa kata ya Namichiga Mikidadi Mbute akiwa anatoa kero zake mbele ya mwenyekiti wa kamati Rashidi Nakumbya




Mhandisi wa Ujenzi ndg. Saidi Munguja akiwa anasoma risala mbele ya wanakamati

Mwenyekiti akiwa anatoa maoni yake baada ya kuona mradi wa barabara za lami za mjini ruangwa

Wanakamati wakiwa wanamsikiliza mwenyekiti na wajumbe wengine maoni yao baada ya kumaliza ziara