Na Mwanakheri Ally
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfery Zambi amewataka
wakurungenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Liwale, Kilwa na Nachingwea kuhakikisha
Zahanati zilizopo ndani ya Wilaya hizo hazifungwi kutokana na upungufu
utakaojitokeza wa watumishi waliokutwa na tatizo la vyeti feki.
Mh Mkuu wa Mkoa Zambi alisema wakurungenzi watendaji wa Halmashauri
hizo wajitahidi kuhamisha wauuguzi watakaokuwa wengi katika eneo moja wapelekwe
katika zile zahanati ambazo zinautaji zaidi ya watumishi.
Aliyasema hayo wakati akihutubia katika sherehe za siku
ya wafanyakazi dunia iliyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa kwenye uwanja wa
shule ya msingi likangara ambapo inafanyika kwa mwaka mara moja mwezi wa 5
tarehe 1.
Kauli hiyo imetokana na agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri
ya Muungano John Pombe Magufuli la watumishi waliokutwa na vyeti feki waache
kazi mara moja laasivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha alisema Serikali imejipanga kupambana na watumishi
wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea kwani uongozi wa awamu hii haupo katika
kulea watu wasiotaka kubadilika.
Pia aliwataka walimu wa shule za msingi na sekondari
waache kunung’unika kuhusu ya maslahi
yao kwani manunguniko yanaweza wasababisha washindwe kufanyakazi ipasavyo na
kusababisha matokea mabaya ya mitihani ya taifa.
“Serikali inajitahidi kutatua matatizo yanaowakabili
hivyo ni wakati wa walimu huko mashuleni kufanya kazi kwa bidii na kubadilisha
matokea ya darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka huu”alisema.
Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau
mbalimbali katika shughuli za mwenge ambazo katika mkoa wa Lindi mwenge utapokelewa tarehe
21 na wilaya ya Ruangwa tarehe 23 na 24 mwezi wa tano.
Wakati huo huo Mratibu wa Tucta mkoa wa Lindi Fatma .s.
Chaunga aliomba serikali kuweza kupunguza kiwango cha kodi kwa wafanyakazi ipungue
kutokana asilimia 9 mpaka 7 kwani bado hiyo asilimia 9 nikubwa kutokana na
mshahara wa watumishi wengi.
Pia aliomba serikali
kuangalia uchumi wa viwanda uweze kuzingatia ajira kwa wazawa kwanza
kwasababu kunawatu wengi wanaelimu ya kutosha kufanya kazi katika viwanda
hivyo.
Hata hivyo Bi Fatma aliipongeza serikali kwa juhudi zake za elimu bure,
hali hii imesababisha wazazi wengi kupata nafasi ya kupeleka watoto wao shule
kwasababu hamna gharama ya ada wanayokutanayo na imesaidia kupunguza watoto
wazururaji huko vijijini na mjini.
|
Watumishi wakiwa katika maandamano kabla ya kuanza kwa sherehe |
|
Wafanyakazi wa Nida wakiwa katika maandamano |
|
wafanyakazi wa Tanesco wakiwa katika maandamano wakiwa na bango linalisema Lipa deni lako ili kutimiza azma ya serikali ya uchumi wa viwanda |
|
Chama cha wafanyakazi Talgwu Halmashauri ya Lindi wakiwa na bango linalosema uchumi wa viwanda uzingatie haki na heshima ya wafanyakazi |
|
Watumishi wakiwa wanasubiri kuingia katika uwanja wa shule ya likangara ili mgeni rasmi apokee maandamano hayo |
|
(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akiwa anaangalia kikundi cha ngoma cha dege la jeshi wakitumbuiza |
|
Kikundi cha dege ya Jeshi cha Ruangwa kikiwa kinatumbuiza mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa |
|
(kushoto) Mratibu wa Tucta Mkoaakiwa anaangalia ka umakini ngoma inayotumbuizwa(kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea |
|
Wananchi wakiwa wamejitokeza katika uwanja wa Likangara kuangalia sherehe za Mei Mosi |
|
Watumishi waliohudhuria katika sherehe ya mei mosi wakiwa wanaangalia burudani mbalimbali |
|
Wananchi wakubwa kwa watoto wakiwa katika uwanja wa likangara wakiangalia sherehe zinavyoendelea |
|
Wafanyakazi waliojitokeza kucheza ngoma pamoja na dege la jeshi |
|
Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa katika banda la Nmb akipokea maelezo kutoka wafanyakazi wa bank hiyo |
|
(kushoto)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa Rashid Nakumbya akiwa na Msahiki Meya wa Lindi |
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Bakari M bakari |
|
Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa katika banda la Nida akisikiliza maelezo kwa Afisa Msajili wa Nida Khalaf Mwalim |
|
Katikati)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa akiwa na Mkurungenzi wa ya Liwale |
|
Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue akiwa anamkabidhi mteja kitambulisho chake baada ya kutembelea banda la nida |
|
Kikundi cha ngoma cha wanafunzi wakiwa wanatumbuiza |
|
Mratibu wa Tucta Mkoa wa Lindi Fatma S Chaunga akiwa anasoma risala mbele ya mgeni rasmi |
|
Mh, Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anahutubia wafanyakazi katika uwanja wa likangara |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa anatoa ahadi yake ya kuwasaidia kikundi cha dege ya jeshi nguo rasmi za kuvaa sehemu kama hizo |
|
Mfanyakazi hodari akiwa anapokea pesa na cheti kutoka kwa mkuu wa mkoa |
|
Bwanashamba wa rondo akienda kupokea zawadi yake kwa kuwa mtumishi hodari |
|
Mwalimu wa shule ya Sekondari Mnacho Benjamin akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi |
|
Afisa Uchaguzi wa Wilaya Yusuph Chilumba akipokea cheti chake na kiasi cha pesa laki 3 |
|
Mfanyakazi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Happiness Mpaza fundi akipokea zawadi kutoka kwa mkuu wa mkoa |
|
Mfanyakazi wa Shirika la umeme akipokea zawadi ya tv nch 32 kwa mkuu wa mkoa |