Na Mwanakheri Ally
Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa Mheshimiwa Joseph Mkirikiti ametoa shukurani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa msaada
wa vifaa vya ujenzi lililoutoa katika shule mpya ya Sekondari ya Kassim
Majaliwa iliyopo Ruangwa Mjini.
Shirika la Nyumba la
Taifa limetoa msaada wa bati 300 na mifuko ya saruji 300 katika shule mpya ya
Kassim Majaliwa ikiwa ni kwa lengo la kuanza ujenzi wa Maabara shuleni hapo.
Mheshimiwa Mkirikiti
aliliomba shirika hilo lisichoke kutoa msaada kwani shule hiyo bado ni changa na
ina mahitaji mengi ya miundo mbinu ambayo hayajakamilika kujengwa pia alilitoa
hofu kwa kusema kuwa vifaa vilivyotolewa vitatumika kama inavyotakiwa.
“Tunataka shule hii iwe
ni shule ya mfano katika Mkoa wa Lindi hivyo vifaa vilivyotolewa tutavitumia
vizuri katika kujenga miundombinu yenye hadhi inayohitajika ili kuifanya shule
hii kuwa imara na ya kudumu”, alisema Mh,Mkirikiti.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Thomas Luambano akiongea na Meneja wa (NHC) Gibson Mwaigomole katika Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa |
kushoto) Meneja wa (NHC) Mkoa Gibson Mwaigomole(kulia)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti wakiwa katika chumba cha makabidhiano ya msaada uliotolewa na (NHC) |
Meneja NHC akikabidhi bati kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa walipoenda kutoa msaada |
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akipokea mifuko ya saruji 300 kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa |
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msaada kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) |