Sunday, 12 February 2017

MKURUGENZI WILAYA YA RUANGWA AWAHIMIZA WALIMU KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO

Na: Mwanakheri Ally

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Andrea Godfrey Chezue amewaaasa Walimu na kuwataka kuwa na nidhamu katika maeneo yao ya kazini na hata nje ya kazini kwani hii itasaidia kuweza kurekebisha nidhamu kwa Wanafunzi wanaowafundisha.

Alisema Mwalimu mwenye nidhamu ni rahisi kumfanya Mwanafunzi anaemfundisha kuwa na nidhamu ambayo itapelekea kuongeza kiwango cha ufaulu katika mitihani ya ndani na nje ya shule.

Hayo ameyaongea wakati wa kikao cha wadau wa elimu kilichohusisha Waratibu Elimu Kata, Wataaluma, Wakuu wa shule na Makamu kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco kikiwa na lengo la kuangalia njia za kuweza kutoka katika hali ya ufaulu wa sasa uliopo na kufikia nafasi nzuri zaidi.

Naye Afisa Utumishi wa Wilaya ya Ruangwa, Festo Mwangalika amewataka Walimu kutenga muda wa kuzungumza na Wanafunzi wanaowafundisha pale ambapo wanakuwa wamewakosea kwani hii inaaweza ikasaidia kubadili mienendo mimbovu ya Wanafunzi.

Pia aliwaambia  Walimu na Waratibu Elimu Kata kuweza kuwafuatilia Wanafunzi wanaowafundisha ili kuweza kubaini wenye tabia mbovu na kuwasaidia mapema kwani hii itasaidia hata kuongeza ufaulu wa Wanafunzi kwani Mwanafunzi mwenye adabu ni rahisi kuwa na maendeleo mazuri.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari, Bi. Hawa Mchopa Bi Zena alisema ilikuweza kuongeza kiwango cha ufaulu katika Wilaya ya Ruangwa inatakiwa Wazazi wawape Walimu ushirikiano katika malezi ya Wanafunzi hao ili kuweza kufikia lengo

Kwani  Watoto hawalelewi na Walimu na Wazazi tu , bali malezi ya Moto ni yajamii nzima, hivyo Jamii inatakiwa kutoa ushirikiano katika malezi hii itasaidia kutoka katika eneo moja kwenda eneo jingine katika hali ya ufaulu.

Afisa Taaluma Robert Bujiku wa Halmashauri ya Ruangwa akiwa anafanya utambulisho wa wadau wa elimu hao waliosimama ni waratibu elimu kata 
Afisa Taaluma akiendelea kufanya utambulisho na hao waliosimama ni wakuu wa shule zilizopo katika wilaya ya Ruangwa
Afisa Taaluma akiendelea kutambulisha na hao ni walimu wakuu wasaidizi wa shule za Wilaya ya Ruangwa
Waratibu wa Elimu kata, Wataaluma Wakuu wa Shule na wasakidizi wao wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti
Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wadau wa elimu (kushoto) Afisa Taalum Richard Bujiku (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Festo J mwangalika akiwa anaongea na wadau wa elimu katika kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuongeza ufaulu wa wanafunzi
Mkuu wa Shule ya Sekondari Likunja Mohammed Lukangaakiwa anatoa maoni yake ya jinsi ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika Wilaya ya Ruangwa
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbekenyera Shanly Nchimbi akiwa anawasilisha moani yake ya kwanini ufaulu kwa mwaka huu wilaya ya Ruangwa kwa kidato cha nne umeshuka na nijinsi gani mwakani utaweza kuiongezeka
Wadau wa Elimu na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Ruangwa wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa shule ya Mbekenyera
Mkuu wa Shule ya Nambilanje Mwl. Kilindo akitoa maoni yake katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukimbi wa Rutesco
Mwalimu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari Nambilanje Tibazarwa akitoa maoni yake ya kuongeza ufaulu na akizungumza vitu vinavyosababisha kushuka kwa ufaulu.
Naye Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Ruangwa akitoa changamoto zilizosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika shule hiyo