Sunday, 12 February 2017

KAMPUNI YA URANEX WAKABIDHI BATI 266 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE MPYA WILANI RUANGWA

Na: Mwanakheri Ally

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Ndugu Andrea Chezue ametoa shukurani kwa Kampuni ya Uranex inayojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya bunyu katika Wilaya ya Ruangwa kwa msaada wa bati waliotoa.

Mkurugenzi amepokea bati 266 kutoka kwa Uranex ambazo zitatumika katika kuwekeza madarasa matano na vyoo ambavyo vinajengwa katika shule ya sekondari mpya inayojengwa kwa nguvu za Wananchi, Halmshauri na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.

Aliyasema hayo wakati akipokea bati hizo kutoka kwa Meneja wa Uranes Mamboleo walipokuwa wanamkabidhi siku ya tarehe 11-02-2017 katika eneo la kiwanda cha kukamulia mafuta ya ufuta mjini Ruangwa.

Pia alisema Mkurugenzi "ujenzi wa vyumba vya madarasa umefikia katika hatua nzuri na unaenda kama ambavyo ilikuwa inategemewa na kesho wanaanza kupaua na kupiga mbao" aidha, aliwaomba Uranex waendelee na moyo huo huo wa kuweza kusaidia katika maeneo mengine wanatakapoombwa msaada.

''Tangu tumeanza ujenzi wa shule hii mpya Uranex tumekuwa nao bega kwa bega kwani walikuwa wanakwenda mara kwa mara kupitia katika eneo la ujenzi kuona hali ya kiujenzi inavyoendelea'' alisema.

Kampuni ya Uranex ilitoa msaada wa bati 266 kama ahadi waliyoitoa katika Ziara ya kikazi ya  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivyokuja mwezi wa Disemba mwaka 2016 ilyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa

Naye Mkuu wa Wilaya Joseph Mkrikiti aliwaomba wadau wengine ambao hawajatoa ahadi walizoahidi basi waweze kutoa ili kuweza kufanikisha ujenzi huo kuisha mapema na Watoto waliokosa nafasi katika shule ya Ruanngwa Sekondari waanze masomo katika shule hiyo mpya.

Aidha, aliuomba Uongozi wa Halmshauri kutunza rasilimali wanazopewa kwa ajili ya ujenzi ili isiwavunje moyo wanaotoa misaada hiyo na kumuomba Mkurugenzi kuwa makini na matumizi ya vifaa hivyo vinavyotolewa na Watu.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya aliuomba Uongozi wa kampuni ya Uranex kutokuwachoka pale wanapokuiwa wanaitaji msaada kwani wao ni Watu wanaowategemea kufanya Ruangwa kuwa Ruangwa ya maendeleo.

Baada ya kupokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na timu ya Wataalamu walioongozana nao waliweza kutembelea shule hiyo inayojengwa na uwanja wa mpira wa Nyasi bandia unaotegemea kujengwa Ruangwa mjini.


Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri na Wataalamu kutoka ofisa ya Mkuu wa Wilaya na wengine kutoka kampuni ya Uranex wakiwa wamesimama wanamsubiri Mkuu wa Wilaya afike katika eneo la tukio

Meneja wa Uranex Aizaki Mamboleo akiwa anaonesha mzigo wa bati walizozileta kama msaada kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa  katika shule mpya

(katikati )Meneji wa Uranex  akiwa na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji) Andrea Chezue (kushoto)Mkuu wa Wilaya wakiwa katika eneo la tukio la kupokea bati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akiwa anatoa shukurani kwa kampuni ya uranex kwa moyo waliouonesha wa kutoa msaada wa bati hizo

Meneja Uranex akiwa anamkabidhi Mkuu wa Wilaya bati walizoleta kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa na choo katika shule mpya.
Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anamkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue bati aliyozabidhiwa na Meneja wa Uranex

Mkuu wa Wilaya akiwa anaongea na watu waliohuidhuria katika tukio hilo baada ya kupokea bati 266 kutoka katika kampuni ya uranex(kushoto kwake) Katibu Tawala Haji na( kulia) Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue

Wataalamu kutoka Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa wakiwa wanamsikiliza Mkurugenzi Mtendaji akitoa shukurani zake kwa kampuni ya uranex
Vyumba vya madarasa ambavyo vinategemewa kuanza kupauliwa na ndiyo vyumba vitakavyowekwa bati zilizotolewa na uranex



Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na Mkurugenzi Andrea chaezue na wataalamu wengine katika eneo la shule mpya



Mafundi katika eneo la shule wakiwa wanatengeneza mbao kwa ajili ya kupandisha kenchi

Mafundi wakiwa wanaendelea na shughuli za kiujenzi ili kuweza kumaliza shughuli hiyo mapema

Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wakiwa wanakagua matundu ya vyoo katika shule hiyo mpya

Mkurugenzi akiwa anamuuliza fundi Juma kwanini ujenzi wa vyoo umesimama kwa maana hauendani na kasi ya madarasa


Mhandisi wa Ujenzi Nalupi akiwa anatoa maelezo katika uwanja unaotegemewa kujengwa wa nyasi bandia katika Wilaya ya Ruangwa kwa Mkuu wa Wilaya

Mkurugenzi Andrea Chezue akiwa anamapa maelezo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti(Kushoto) na (kulia ) Afisa Mipango Thomas Luambano

Mkurugenzi akiwa anaongea na Meneja wa Uranex Mamboleo (kulia)akimpa maelezo ya uwanja na mambo mengine yanatotegemewa kufanywa na Halmashauri kama kuwa na gadeni

Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa eneo la dodoma mahali ambapo uwanja unategemea kutengenezwa