Barabara ya Nachingwea ikiwa katika hatua za mwanzo za ujenzi wa lami
Na: Mwanakheri Ally
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Suleimani
Jafo amemtaka mkandarasi anaemiliki Kampuni ya Wanyumbani Construction anayejenga barabara za lami katika Wilaya ya Ruangwa
kujenga barabara hizo katika kiwango cha ubora unaotakiwa na kwa muda uliopangwa.
Pia amemtaka Mkadarasi huyo
kutumia malighafi za ujenzi zilizokusudiwa ili kuweza kufanikiwa kuwa na barabara zenye
ubora uliokusidiwa na zitakazodumu muda mrefu.
Mhe.
Jafo ameyasema hayo wakati akikagua
barabara za lami zinazojengwa na mkadarasi mwenye Kampuni ya Wanyumbani
Construction wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika katika Wilaya
ya
Ruangwa.
Aidha, Naibu Waziri huyo alimtaka
Mkurungezi wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Andrea Chezue kuendelea kufuatilia kwa
ukaribu ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule mpya inayojengwa Wilayani hapo
ili shule hiyo iweze kuwa na ubora.
“kwa kuangalia jinsi
majengo yalivyo, inaonesha kabisa majengo haya yana ubora unaotakiwa hivyo
hongereni sana na hongera zaidi kwa Mbunge wa Jimbo kwa msaada alioutoa na
anaoendelea kuutoa katika ujenzi wa shule hiyo” alisema
Wakati huo huo Naibu Waziri Jaffo amewataka Watumishi wa Wilaya ya Ruangwa kuacha kufanya kazi
kwa mazoea na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kufikia kasi inayotakiwa.
Alisema Naibu Waziri Watumishi wa Ruangwa wanapaswa kuwa mfano wa kuingwa katika Wilaya nyingine
kwani wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili wasimuangushe Waziri Mkuu.
“Msijibweteke na msifanye
kazi kwa mazoea huu ni wakati wa kubadilika na kuwa Watu wapya kama ujabadilika
basi fanya kubadilika mara moja ili uweze kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli” alisema.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe.Joseph Mkirikiti aliwataka Watumishi
kuzingatia maagizo ya Naibu Waziri na kuyafanyia kazi kwani ni wajibu wa
kila Mtumishi kufanya kazi kwa bidii na kufuata taratibu za
kiutumishi.
Aidha alimuahidi Naibu Waziri kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa na kuyatafutia ufumbuzi kama inavyotakiwa mara moja.
|