Monday, 16 January 2017

KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII WILAYA YA RUANGWA YAFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI YA KIJAMII

Na: Mwanakheri Ally

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji-Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Omari Pendeka, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kushiriki katika shughuli za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata au Vijiji vyao na kujua kuwa miradi hiyo ya kimaendeleo kama vile Zahanati, Barabara na Shule zinazojengwa ni mali ya Wananchi wenyewe na si Serikali.

Mhe. Omari Pendeka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wanakamati wa Huduma za Jamii wakati wa Ziara ya Kamati ya Elimu Afya na Maji walipokuwa wanatembelea na kuhamasisha shughuli za Maendeleo katika Kijiji cha Namilema na Mbekenyera.

Kaimu Mwenyekiti huyo aliwataka Wanakamati kuwasimamia Mafundi kwa ukaribu ili kufanikisha shughuli hizo kwa muda uliopangwa, pia aliwataka Wanakamati kuwahamasisha Wananchi ili waweze kujitolea pale ambapo watakuwa wanahitajika.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji, Mhe. Omari Pendeka(katikati) akiwa anazungumza na Wanakamati wa Huduma za Jamii, Diwani wa Viti Maalum Nandagala Amina R Naenje(kushoto) kulia  Diwani  likuche wa Mbwemkuru
Wajumbe ya kamati ya Maji, Afya na Elimu wakiwa wanapata utambulisho kutoka kwa wenye kamati ya ujenzi kijiji cha Namilema
Mafundi wakiwa wanaendelea na ujenzi katika Shule ya Msingi Namilema

Wajumbe wa kamati ya Elimu Afya na Maji wakiwa wamewasili katika eneo linalotarajiwa kujengwa Zahanati ya Namilema

Wajumbe wa Kamati ya Elimu  Afya na Maji wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa ni Madiwani na Wakuu wa Idara 

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji akiwa anawasili shule ya Sekondari Mbekenyera kukagua miradi iliyopo shuleni hapo(kulia) Afisa Elimu Taaluma Robert Bujiku
Mkuu wa Shule ya Mbekenyera  Shanly Nchimbi akiwa anasoma taarifa fupi kwa wanakamati ya Elimu Afya na Maji waliofika shuleni hapo
Moja ya madarasa yaliyokwisha kamilika shule ya sekondari MbekenyeraMganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbekenyera Mikidadi Mbule akiwa anatoa maelezo ya mradi wa ujenzi ya wodi ya akina Mama ulipofikia kwa wanakamati wa Elimu Afya na Maji.
Kaimu Mwenyekiti akiwa anaongea na Wanakamati katika Kituo cha Afya Mbekenyera
Wanakamati wakiwa wanakagua ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Mbekenyera
Yusuf Chilumba Afisa Elimu Ufundi akiwa anaiongoza kamati ya Elimu Afya na Maji  kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo unaofanyika shuleni hapo

Thursday, 12 January 2017

MKUU WA MKOA WA LINDI AWAASA WATUMISHI KUZINGATIA KANUNI NA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

Na: Mwanakheri Ally
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amewataka Watumishi wa Wilaya ya Ruangwa kuzingatia maadili na miiko ya Utumishi wa Umma

Mkuu wa Mkoa aliwausia Watumishi kwa kuwakumbusha wajibu wao na kuwaonya matumizi mabaya ya simu za mkononi wakati wa muda wa kazi, pia aliwaasa kuacha mazoea ya karibu na Wanafunzi ambayo yatapelekea mahusiano yasiyokuwa rasmi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Walimu wa Shule ya Sekondari Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya hiyo tarehe 11/01/ 2017.

Pia aliwaambia Watumishi hasa wa kada ya Elimu kuwa wao ni Wazazi na Viongozi wa Jamii  inayowazunguka hivyo wanapaswa kuwa mfano mzuri wa kuingwa katika Jamii, na wanapaswa kuzingatia mavazi yenye maadili wanapokuwa maeneo ya kazi.

 Aidha, Mkuuhuyo wa Mkoa alimtaka Mkuu wa Wilaya  ya Ruangwa, Mhe. Joseph Mkirikiti kufuatilia Watoto wenye utoro sugu mashuleni kwa kuanza kuwakamata Wazazi wao na pia Watoto hao kuchukuliwa hatua kwa pamoja ili kuweza kufanikisha kutokomeza utoro mashuleni.

Vilevile aliutaka uongozi wa Halmshauri kuzingatia kujenga vyoo ambavyo havitumi maji mengi katika ujenzi wa shule mpya inayojengwa Wilayani hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, alisema ameanzisha mkakati wa kukabiliana na Watoto wenye utoro sugu kwa kuweka utaratibu wa kupelekewa idadi ya Wanafunzi watoro kila siku ya Jumatatu na utaratibu huuuinaanza mara moja.