Wednesday, 5 April 2017

MKUU WA WILAYA RUANGWA AMEWATAKA WANANCHI WA RUANGWA KUCHUKUA TAHADHARI KWA KUJENGA NYUMBA IMARA NA BORA



(kushoto)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaangalia mkorosho ulioanguka na anasikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo
Moja ya shamba la nyumbani lililoharibika na mvua kali iliyoambatana na upepo mkali
Mkuu wa Wilaya akiwa anatoa maelekezo baada ya kuona nyumba iliyoezuliwa na bati




Moja ya nyumba iliharibiwa na mvua kali iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Chinongwe


 Mkorosho ulioangushwa na upepo mkali baada ya kunyesha mvua kubwa kijijini hapo
Mkuu wa Wilaya na timu yake wakiwa wanaangalia nyumba iliyoharibu na kumpa pole mhanga wa maafa hayo
(Katikati)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na viongozi wa kijiji na wahanga wa mafuriko(Kushoto)Mwenyekiti wa Kijiji
Mtendaji wa Kijiji Jafari Namtima(aliyesimama) akiwa anasikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
Wanakijiji wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya akiwafariji na kuwapa mbinu za kuweza kujenga nyumba imara na bora
Na: Mwanakheri Ally

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kujenga nyumba zenye ubora na uimara kwa kufuata taratibu za ujenzi.

Aidha, Mkuu wa Wilaya amewataka mafundi wanaojishughulisha na shughuli za ujenzi wa nyumba kutumia fani zao za kiufundi kuwashauri wateja wao viwango vya nyumba imara vinavyoitajika kabla ya kuanza ujenzi. 

Mhe. mkirikiti ameyasema hayo wakati anaongea wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Chinongwe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa, mafuriko hayo yametokea usiku wa kuamkia jana baada ya kunyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Mhe. Mkirikiti aliwapa pole waathirika wote waliokubwa na hali ya kuezuliwa nyumba zao na kuharibikiwa na mashamba ya majumbani na kuwataka kutokutaka tama na hali hiyo.

Halikadhalika, Mkuu wa Wilaya aliwataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kuchukua tahadhari mapema kwani hali ya mvua iko maeneo yote hivyo ni wajibu wa kila Mwananchi kudhibiti eneo lake.

“Nimetembea katika nyumba zote zilizokubwa na upepo huo wa jana na nikagundua tatizo hatujengi nyumba zenye ubora na uimara kuanzia sasa viongozi wa kijiji waanze kusimamia masuala ya ujenzi wa nyumba zenye kiwango kunachotakiwa”alisema

Naye Afisa Kilimo Wilaya ya Ruangwa, aliwataka Wananchi kukata mikorosho iliyokaribu na nyumba zao kwani inaweza kuleta madhara makubwa ikiendelea kuachwa, kwasababu mikorosho hiyo haijapandwa kufuata vipimo vinayoitajika.

“Shimo la mkorosho linatakiwa kuwa na futi mbili ila hiyo mikorosho iliyopandwa majumbani mingi imepandwa kiholela basi naomba ambaye mkorosho wake upo karibu na nyumba na umepandwa bila kipimo husika aukate mara moja kuepusha madhara mengine makubwa”alisema

Mafuriko hayo yameharibu nyumba za watu 55, mashamba ya majumbani  na majeruhi 1 ambaye kwasasa amelazwa Hospitali ya Ndanda na hali yake anaendelea vizuri kwasasa.