Monday 21 August 2017

Dr Kalemani Azindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mkoa wa Lindi

Na Mwanakheri Ally

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr. Medadi Kalemani amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Lindi kutenga fedha zitakazofanya shughuli ya ‘wiring’ katika taasisi za umma katika msimu wa REA III.

Aliyasema hayo katika kijiji cha Chinongwe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi alipokuwa anazindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

Dr Kalemani aliwataka wakazi wa Kijiji cha Chinongwe waitumie fursa hiyo vizuri kwa kuweka umeme majumbani mwao, kwani wamepata bahati katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Lindi wao wamepata nafasi ya kwanza ya kupata huduma hiyo.

“Umeme ni uchumi, umeme ni kila jambo tunakila sababu ya kuipongeza Serikali kwa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma nzuri za jamiii, hivyo msiishie kuweka umeme majumbani tu utumieni kufanya shughuli za kiuchumi”alisema Dr Kalemani.

Vilevile alimtaka Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Mkoa wa Lindi kufanya utaratibu wa kuanzisha madawati ya kuhudumia wateja wenye shida ya kuunganishiwa umeme katika vijiji ambavyo mradi unapita.

“Sitaki kusikia mwananchi anatembea kilometa 30 kwenda mjini kufuatilia suala la kuunganishiwa umeme nataka TANESCO ndiyo muwafuate wateja kwani mteja ni mfalme narudia tena ni mwiko mteja kumfuata TANESCO” alisema Dr Kalemani.

Pia alimtaka mkandarasi atakayekuwa anafanya ‘wiring’ katika makazi ya watu aidhinishwe na TANESCO wenyewe ili kuepuka vishoka na kuepuka suala la bei kutofautiana wakati zoezi hilo likiendelea.

“TANESCO chondechonde msiwawekee wananchi wetu bei kubwa ya kufanya ‘wiring’, bei iwe nafuu ili kila mwananchi aweze kupata huduma hiyo, tunataka kila mwananchi autumie umeme kuanzisha viwanda vidogovidogo”alisema Mh, Kalemani.

Naye Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamohanga  alitoa pongezi kwa serikali kwa kuweza kusimamia na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma nzuri za kijamii.

“Serikali ya awamu ya tano inataka kila kijiji na vitongoji vyake umeme uweze kuwafikia wakazi wake na ndiyo maana umeme ni uchumi na umeme ni kila kitu wananchi watumie fursa hii vizuri”, alisema Namhanga.

Nyamohanga alisema vijiji 348 vilivyopo katika Mkoa wa Lindi vinatakiwa vipatiwe umeme, ila Wakandarasi wataanza na vijiji 175 ambavyo kazi yake itafanyika kwa wiki 24, wakimaliza hiyo wataendelea na vijiji 173 vitakavyobaki.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalemani baada ya kuwasili sehemu ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa baada ya kuwasili uwanjani Chinongwe

Dr Kalemani akiwasili katika kijiji cha Chinongwe alipoenda kuzindua mpango wa kusambaza umeme vijijini  awamu ya tatu

Dr Kalemani akisalimia wanakikundi cha ngoma wa kijiji cha chinongwe alipowasili

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akinong'ona na Dr kalemani kabla ya tukio la uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Chinongwe

(kushoto) Dr Kalemani, (katikati) Katibu Tawala wa Mkoa Ramadhani Kaswa na (kulia) Mhandisi Gissima Nyamohanga wakiwa katika uwanja wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme mkoa wa Lindi wakiwa katika uwanja wa uzinduzi wakisubiri mgeni rasmi awasili
(aliyevaa koti la rangi ya maziwa)Mganga Mkuu wa Wilaya Dr Japhet Simeo wapili yake Mkuu wa Kitengo cha Ugavi Oscar Magoge wakiwa katika uzinduzi wa REA III





Wananchi wa Kijiji cha chonongwe wakiwa katika uwanja wa Uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akiwa anasikiliza hotuba ya Mhe Naibu Waziri

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akienda kutunza wacheza ngoma wa jeshi la dege wa Wilayani Ruangwa na nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti

Wanakikundi cha dege la jeshi wakiwa wanatumbuiza katika uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha chinongwe
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Twaha Mpembenwe akitoa utambulisho wa watu alioambatana nao kutoka wilaya ya Ruangwa




Diwani ya kata ya Luchelegwa Jaffari Chande akisalimia wakazi wa Chinongwe na wageni kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo

Mkuu wa Wilaya Mhe, Joseph Mkirikiti akisalimia wakazi wa Chinongwe na akitumia bafasi hiyo kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa aweze kumkaribisha Mgeni rasmi

Katibu Tawala Mkoa Ramadhani Kaswa akimkaribisha Mgeni Rasmi ili azindue Mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu

Wakazi wa chinongwe wakiwa na furaha ya kupelekewa umeme katika kata hiyo wakiwa katika uwanja wa uzinduzi

Dr Kalemani akiongea na wakazi wa chinongwe alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu

Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa wamebeba vifaa vya UMETA wakisubiri Dr Kalemani aweze kuvigawa kwa wazee

Dr Kalemani akigawa  vifaa vya umeta kwa wazee wasiojiweza wa kijiji cha Chinongwe alipoenda kuzindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika mkoa wa Lindi


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akikata utepe kwenda katika jiwe la uzinduzi wa  mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika Mkoa wa Lindi

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akizindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika Mkoa wa Lindi

Diwani ya kata ya Luchelegwa Jaffari Chande akiangalia jiwe la uzinduzi  wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu

jiwe la uzinduzi  wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu lililoweka na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalemani









NHC Imetoa Msaada Wa Mabati 300 na Saruji 300 Katika Shule Ya Sekondari Kassim Majaaliwa



Na Mwanakheri Ally

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Joseph Mkirikiti ametoa shukurani kwa Mkurugenzi  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa msaada wa vifaa vya ujenzi lililoutoa katika shule mpya ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Ruangwa Mjini.

Shirika la Nyumba la Taifa limetoa msaada wa bati 300 na mifuko ya saruji 300 katika shule mpya ya Kassim Majaliwa ikiwa ni kwa lengo la kuanza ujenzi wa Maabara shuleni hapo.

Mheshimiwa Mkirikiti aliliomba shirika hilo lisichoke kutoa msaada kwani shule hiyo bado ni changa na ina mahitaji mengi ya miundo mbinu ambayo hayajakamilika kujengwa pia alilitoa hofu kwa kusema kuwa vifaa vilivyotolewa vitatumika kama inavyotakiwa.

“Tunataka shule hii iwe ni shule ya mfano katika Mkoa wa Lindi hivyo vifaa vilivyotolewa tutavitumia vizuri katika kujenga miundombinu yenye hadhi inayohitajika ili kuifanya shule hii kuwa imara na ya kudumu”, alisema Mh,Mkirikiti.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Thomas Luambano akiongea na Meneja wa (NHC) Gibson Mwaigomole katika Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa
kushoto) Meneja wa (NHC) Mkoa Gibson Mwaigomole(kulia)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti  wakiwa katika chumba cha makabidhiano ya msaada uliotolewa na (NHC)


kushoto) Meneja wa (NHC) Mkoa Gibson Mwaigomole(katikati)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti na( kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Thomas Luambano wakiwa katika chumba cha makabidhiano ya msaada uliotolewa na (NHC) na (wamwisho) Katibu Tawala wa Wilaya Twaha Mpembenwe

Meneja NHC akikabidhi bati kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa walipoenda kutoa msaada

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akipokea mifuko ya saruji 300 kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa

kushoto) Meneja wa (NHC) Mkoa Gibson Mwaigomole(katikati)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti na( kulia) ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Thomas Luambano wakiwa katika chumba cha makabidhiano ya msaada uliotolewa na (NHC)

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti akitoa neno la shukurani baada ya kupokea msaada kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)