Monday, 31 July 2017

Mhe, Nakumbiya Amewata Viongozi Wa Amcos Kuwa Wa Adilifu Katika Kutekeleza Majukumu YaoNA MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe,Rashidi Nakumbya amewataka viongozi wapya wa vyama vya ushirika (Amcos) kufanya kazi kwa uadilifu katika kutekeleza majukumu yao.

Mwenyekiti alisema viongozi waliobahatikia kupata nafasi katika vyama vya Amcosi waitumie nafasi hiyo kwa kufanya mambo yenye manufaa kwa wanaushirika na wanakulima wao.

Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Julai 28 mpaka 29 2017, katika ukumbi wa Rutesco Mjini Ruangwa.

Nakumbya alisema kipindi kilichopita baadhi ya viongozi wa Amcos walitumia madaraka yao vibaya kwa kuhujumu mali za wanachama hali iliyopelekea wanachama kukosa imani na viongozi wao.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti aliwataka waendesha bodaboda kufuata sheria za barabarani kama zinavyoelekezwa na vyombo vya usalama.

“Vijana wetu wanajisahau sana huko barabarani na hasa vijijini ambako wanaona hakuna  maaskari, wanabebana watu wanne pikipiki moja hili jambo ni hatari kwa usalama na maisha yao”alisema Mhe, Mkirikiti.

Pamoja na hayo mkuu wa wilaya alizungumzia rasilimali ya madini ambayo ina wawekezaji wengi na inakua kwa kasi sana wilayani Ruangwa akiitaka iangaliwe kwa undani ili kuepusha migogoro na upotezaji wa mapato ya serikali

” Watu wa madini tunatakiwa tuwaangalie kwa jicho la ndani zaidi” alisema Mh.Mkirikiti.

Aidha Mhe Diwani wa Kata ya Nandagala Mh. Chikongwe alitoa pongezi kwa Menejimenti ya wilaya ya Ruangwa na hasa Mkurungenzi Mtendaji  kwa juhudi alizozifanya za kuiendesha Halmashauri.

“Wakati Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue anafikia katika Halmashuari hii aliikuta madeni mengi sana ila kwa uchapakazi wake aliweza kupunguza madeni hayo kwa kiasi kikubwa na kuifanya Halmashauri kuwa katika hali nzuri mpaka sasa”alisema Chikongwe.Add caption

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ili afungue Mkutano wa Baraza


Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbiya akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani
Wataalamu wa Halmashauri wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Afisa Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akiwa anatoa nasaha zake kwa Wazazi na Mwanafunzi wa Kidato cha tano

Afisa Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akimkabidhi Zainabu Fedha alizochangiwa na Watumishi wa Halmashauri kwa Lengo la kwenda Kidato cha Tano


Waheshimiwa Madiwani wakiwa wanafuatilia Taarifa ya Mkurugenzi kwa umakini zaidi

Mwakilishi Kutoka Taasisi ya Namaigo Abdallah Said akiwa anatoa maelezo ya huduma wanazozitoa

Diwani wa Kata ya Nadagala Mhe, Chikongwe akiwa anatoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Menejimenti

Mhe, Diwani akiwa anauliza swali kwa Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri

(kulia) Diwani wa Viti Maalumu Paulina Muya na (kushoto) Diwani wa Kata ya Mandawa wakiwa kwenye kikao cha Baraza

Mhe, Diwani wa Viti Maalumu akiulizwa swali kipindi cha maswali na majibu

Mhe, Diwani wa Kata ya Nandagala akiwa anaomba kura kwa Madiwani wengine baada ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti


Mhe, Diwani wa Viti Maalumu akiwa anaomba kura kwa Madiwani wengine baada ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti


Mkuu wa Wilaya akiwa anazungumza na Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri katika Mkutano wa Baraza


Katibu Tawala wa Halmashauri Twaha Mpembenwe akiwa anafuatilia Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji

Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Mkutano wa Baraza julai 29/ 2017

waandishi wa mkutano wakifatilia kwa makiniTuesday, 25 July 2017

DC Mkirikiti: Wazazi Waliowapeleka Watoto Unyago Kipindi Hiki Cha Masomo Wachukuliwe Hatua za kali za Kisheria.

 Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mh. Joseph  Mkirikiti amewataka wenyeviti wa Vijiji vilivyopo wilayani Ruangwa kuwachukulia hatua za kisheria watu walio wapeleka watoto wao katika sherehe za unyago wakati shule zimefungiliwa.

Alitoa msisitizo huo baada ya kutembelea shule ya Msingi Makanjiro na kugundua upungufu wa wanafunzi nane wa darasa la 3 ambao wamepelekwa jando  huku masomo yanaendelea mashuleni.

Wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika kata ya Makanjiro yenye vijiji vitano (5), ambavyo ni Chinokole, Chikoko, Mbagara, Makanjiro na Chilangalile.
Mkuu wa Wilaya alisema hapingi suala la wakazi wa Ruangwa kufanya masuala ya unyango, anaruhusu ila yafanyike wakati wa likizo kama anavyowaeleza katika mikutano yake.

“Kila sehemu inamila yake na watu wanatakiwa kuheshimu mila hizo naheshimu mila za wakazi wangu wa Ruangwa ila suala la elimu ni muhimu na nitajitahidi kulifuatilia kwa ukaribu zaid hivyo fanyeni shughuli za unyango wakati wa likizo”alisema, Mhe,Mkirikiti

Aidha wakati wa ziara hiyo Mh.Mkirikiti alisema msimu huu wa korosho atakua makini zaidi na watu ambao wamekuwa na tabia ya kuwaibia wakulima korosho kwani  huwarudisha nyuma wakulima na kuwakatisha tamaa.

“Mwaka jana wizi ulikuwa mkubwa ila tulikuja kungundua hilo mwishoni mwa msimu mwaka huu mwanzo tu wa msimu nitafuatilia kila mahala, mkulima wa korosho hakikisha umeshasajiliwa kwenye daftari la wakulima”alisema Mhe, Mkirikiti.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya Twaha Mpembwene aliwataka wananchi wa kata ya Makanjiro kuishi kwa upendo na watumishi  walio katika kata hiyo kwani wao ndiyo kama wazazi kwao.

Pia aliwataka walimu wa shule ya Sekondari Makanjiro kuwa wavumilivu kwani wao ni watu muhimu katika jamii hiyo na pia Serikali inawategemea katika kuzalisha matokeo mazuri kwa wanafunzi wa shuleni hapo.


MKuu wa wilaya ya Ruangwa akizungumza na wajumbe wa serikali ya Kijiji cha Chinokole kata ya Makanjiro

Moja ya Bustani inayohudumiwa na mradi wa umwagiliaji wa Chinokole


Mkuu wa wilaya akitoa maelekezo ya utunzaji wa Scheme ya umwagiliaji iliyopo katika kijiji cha Chinokole

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mh, Joseph Mkirikiti na Afisa Utumishi wa Wilaya ya Ruangwa Festo Mwangalika wakikagua mradi wa bwawa la umwagiliaji Chinokole


Mkuu wa wilaya ya Ruangwa na Afisa Tawala (aliyevaa miwani) wakizungumza na wavamizi wa eneo la umwagiliaji ambalo wanalitumia kama sehemu ya kufyatulia matofali

Wavamizi wa eneo la mradi wa umwagiliaji kama walivyokutwa wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya Ruangwa wakiendelea na shughuli zao za ufyatuaji wa matofali.

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chinokole na wataalam waliongozana na Mkuu wa wilaya wakisikiliza maagizo kutoka kwa mkuu wa wilaya kuwa eneo la umwagilijaji ni mali ya jamii.


Mtendaji wa kata ya Makanjiro Mohamed Mamba akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Chinokole kwa Mkuu wa wilaya ya Ruangwa.

wananchi wa kata ya makanjiro wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya RuangwaAfisa Tawala wa Wialaya ya Ruangwa Mh. Twaha Mpembenwe akizungumza na wananchi wa wa kata ya Makanjiro wakati wa ziara yakikazi ya mkuu wa wilaya Ya Ruangwa

Add caption

Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Makanjiro Glory Kiria akimsomea MhMkuu wa wilaya taarifa ya Bima ya Afya ya jamii (CHF)(kulia) Mh. Diwani wa kaa ya maknjiro na walimu wa shule ya sekondary makanjiro wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya ya Ruangwa

walimu wa shule ya sekondari Makanjiro wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake katika shule hiyo.

Wataalam wa Kata ya Makanjiro wakisikiliza maelekezo ya mkuu wa wilaya Mh. Joseph Mkirikiti

wananchi wa kijiji cha chikoko kata ya Makanjiro wakisikiliza hotuba ya mh. mkuu wa wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake

Mh, Joseph MKirikiti akihutubia wananchi wa kijiji cha Chikoko  Kata ya makanjiro wakati wa ziara yake ya kazi (kulia) Afisa Tawala wilaya ya Ruangwa Mh. Twaha Mpembenwe


Thursday, 20 July 2017

Mhe,Mnunduma: Amewataka wanufaika wa Mpango wa Tasaf III Kuzitumia Fedha Hizo Kwa Shughuli Za Kiuchumi

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Rashidi Mnunduma, amewataka wananchi wanaopokea pesa za kaya masikini wazitumie vizuri pesa hizo kwa kufanya shughuli za kiuchumi.

Alisema Mwenyekiti badala ya mtu kupokea hizo pesa na kuanza kufanya matumizi yasiyoyalazima ni vizuri mtu akawekeza katika kilimo, ufugaji wa kuku na biashara ndogondogo na hata kujenga nyumba nzuri ya kuishi.

Aliyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira baada ya kutembelea   na Kukagua  Miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ikiwa ni utekelezaji wake kila robo ya mwaka.

 
Kamati hiii iligawanyika katika makundi mawili kundi A na B makundi hayo yalifanya ziara hiyo siku ya tarehe 20/7/2017 kundi A liliongozwa na  Mwenyekiti wa Kamati Mhe , Rashidi Mnunduma na Kundi B  na wajumbe.

Kamati ilitembelea Miradi  ambayo ni Mradi wa kuona ujenzi wa barabara , kata ya  Namichiga, Ujenzi wa Zahanati, Muhuru  ,Kuona mradi wa Tasaf, kijiji cha Nahanga kata ya  Mandawa, na kuona mradi wa msitu Mchichila.

(katikati)Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mhe, Rashindi Nnunduma akitoa maoni yake baada ya kuona mradi wa ujenzi wa barabara namichiga


Mwenyekiti wa Kamati akiwa anaongea na wananchi wa Namichiga

Mkazi wa Kijiji cha Namichiga bwana Malengo akiwa anatoa maoni kwa wanakamati

Jengo la Zahanati kijiji cha Muhuru likiwa katika hatua za awali

(katikati) Mhe, Diwani ya Kata ya Chunyu Kambona na (kushoto) Mwenyekiti wa Kamati


Mtendaji wa kijiji cha Muhuru Awesa Juma akiwa anatoa maelezo ya Mradi kwa wanakamati(kulia)Mhe, Songea

Wataalamu kutoka Halmashauri walioambatana Waheshimiwa MadiwaniMwenyekiti wa Kijiji cha Nahanga akisoma taarifa mbele ya wanakamati

(Katikati) Mnufaika wa mradi wa Tasaff III aliyejenga kwa fedha hizo

Mwenyekiti wa Kamati Mhe, Mnunduma akisikiliza maelezo kutoka kwa mnufaika wa mradi huo

Nyumba iliyojengwa na Hadija Lichenjera kwa fedha za Tasaf III

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mchichili akiwa anatoa maelezo ya mradi wa Msitu uliopo katika kijiji chao

Wajumbe wa Serikali ya Kijiji wakiwa katika ofisi ya kijiji

Katibu wa Kamati Zuhura Makota akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati

Afisa Misitu Masagya akiwa anatoa maelezo ya mradi huo  mbele ya wanakamati


Msitu uliopo katika kijiji cha Mchichila

Msitu wa Mchichila wenye hekta 450


Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira wakiwa wanaangalia chanzo cha maji Mandawa


Jengo la jipya la Radio Ruangwa likiwa katika hatua za ukamilishaji