Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
Rashidi Mnunduma, amewataka wananchi wanaopokea pesa za kaya masikini wazitumie
vizuri pesa hizo kwa kufanya shughuli za kiuchumi.
Alisema Mwenyekiti badala ya mtu kupokea hizo pesa
na kuanza kufanya matumizi yasiyoyalazima ni vizuri mtu akawekeza katika
kilimo, ufugaji wa kuku na biashara ndogondogo na hata kujenga nyumba nzuri ya kuishi.
Aliyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Uchumi,
Ujenzi na Mazingira baada ya kutembelea na Kukagua Miradi ya
Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ikiwa ni utekelezaji wake kila robo ya
mwaka.
Kamati
hiii iligawanyika katika makundi mawili kundi A na B makundi hayo yalifanya
ziara hiyo siku ya tarehe 20/7/2017 kundi A liliongozwa na Mwenyekiti wa
Kamati Mhe , Rashidi Mnunduma na Kundi B
na wajumbe.
Kamati
ilitembelea Miradi ambayo ni Mradi wa kuona ujenzi wa barabara ,
kata ya Namichiga, Ujenzi wa Zahanati, Muhuru ,Kuona mradi wa Tasaf, kijiji cha Nahanga kata
ya Mandawa, na kuona mradi wa msitu
Mchichila.
|
(katikati)Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Mhe, Rashindi Nnunduma akitoa maoni yake baada ya kuona mradi wa ujenzi wa barabara namichiga |
|
Mwenyekiti wa Kamati akiwa anaongea na wananchi wa Namichiga |
|
Mkazi wa Kijiji cha Namichiga bwana Malengo akiwa anatoa maoni kwa wanakamati |
|
Jengo la Zahanati kijiji cha Muhuru likiwa katika hatua za awali |
|
(katikati) Mhe, Diwani ya Kata ya Chunyu Kambona na (kushoto) Mwenyekiti wa Kamati |
|
Mtendaji wa kijiji cha Muhuru Awesa Juma akiwa anatoa maelezo ya Mradi kwa wanakamati(kulia)Mhe, Songea |
|
Wataalamu kutoka Halmashauri walioambatana Waheshimiwa Madiwani |
|
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nahanga akisoma taarifa mbele ya wanakamati |
|
(Katikati) Mnufaika wa mradi wa Tasaff III aliyejenga kwa fedha hizo |
|
Mwenyekiti wa Kamati Mhe, Mnunduma akisikiliza maelezo kutoka kwa mnufaika wa mradi huo |
|
Nyumba iliyojengwa na Hadija Lichenjera kwa fedha za Tasaf III |
|
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mchichili akiwa anatoa maelezo ya mradi wa Msitu uliopo katika kijiji chao |
|
Wajumbe wa Serikali ya Kijiji wakiwa katika ofisi ya kijiji |
|
Katibu wa Kamati Zuhura Makota akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati |
|
Afisa Misitu Masagya akiwa anatoa maelezo ya mradi huo mbele ya wanakamati |
|
Msitu uliopo katika kijiji cha Mchichila |
|
Msitu wa Mchichila wenye hekta 450 |
|
Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira wakiwa wanaangalia chanzo cha maji Mandawa |
|
Jengo la jipya la Radio Ruangwa likiwa katika hatua za ukamilishaji |