Sunday, 31 December 2017

Tafuteni Takwimu Mpya, Waziri Mkuu Aagiza



NA MWANDISHI WETU

Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Kilimo kutoka mikoa inayolima korosho, washirikiane kupata takwimu mpya za wakulima wa zao hilo.

Ametoa agizo hilo leo mchana jumapili, Desemba 31,2017) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya milioni 10 msimu wa 2017/ 2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi.

“Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na kusimamia kwa umakini upatikanaji wa twakimu za wakulima na maeneo yanayolimwa, haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu” alisema Waziri Mkuu

“Afisa kilimo wa Wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo ana miche mingapi, na ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani “alisema.

Pia nilikwisha waagiza maafisa ushirika na viongoi wa vyama vya msingi(AMCOS) mpaka chama kikuu cha ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Mwenyekiti wa kijiji, kwasababu wao wanaidadi kamili za watu    wanaowaongoza”alisema.

“Ninaimani tukifanya hili tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa nauwezo mkubwa wa kuwahudumia wakulima wake, tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji yao”alisisitiza

Waziri Mkuu alipanda mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha kugawa miche kwa wakulima 10 kutoka Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao waliwakilisha wenzao

 Mapema kabla ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu za pili iliyotokana na vikonyo





Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi mche mpya wa mkorosho Bi. Mwanahamisi Saidi, mkazi wa Kilimahewa, baada ya kuzinduzi kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 Mjini Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho  ,mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Hassani Jarufu wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa Miche Mipya ya Korosho kutoka kwa Afisa Ubanguaji Bodi ya Korosho Domina Mkaranga, Wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018 mjini Ruangwa

Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa akiangalia Mche Mpya wa Korosho, wakati akikagua kitalu cha miche hiyo, katika kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya mikorosho alipotembelea vitalu vya miche hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue


Miche ya Mikorosho Mipya na bora iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

Friday, 24 November 2017

Mhe, Ndemanga Awataka Waendesha Pikipiki Kujifunza Alama za Barabarani Ili Kupunguza Ajali Za Barabarani



NA MWANAKHERI ALLY

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe, Shaibu Ndemanga aliyekuwa anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani, amewataka waendesha Pikipiki kujifunza alama za barabarani kwa umakini na kuzitumia kama ambavyo zinaelekezwa.

Mhe, Ndemanga aliwataka waendesha pikipiki wanavyoenda kujifunza kuandesha chombo hiko cha moto wanapaswa kuzingatia  somo la alama barabarani kwani hii itasaidia sana kupunguza ajali 

Mgeni Rasmi Mhe, Ndemaga aliyasema hayo katika siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani Kimkoa katika Wilaya ya Ruangwa iliyofanyika kuanzia 20/11/2017 hadi 24/11/2017.

Pia Mhe, Ndemaga alisisitizi suala la kujifunza alama za barabarani lisiwe ni la madereva tu wanaoendesha chombo hiko hata wananchi wanapaswa kujifunza na kuzielewa alama hizo ili kufanikiwa kupunguza ajali za barabarani.

“Lindi isiyo na jali za barabarani inawezekana na katika kufanikisha hili ni wajibu wa kila mwananchi wa Mkoa wa Lindi kujifunza umuhimu wa alama hizo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kwa ajali zinazotokea”alisema Ndemanga.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Lindi aliwataka waendesha pikipiki kwa ajili ya kujipatia riziki kuheshimu kazi hiyo na kuiona kama ni kazi nyingine kwani ndiyo sehemu inayowaingizia kipato na kufanya kuendesha maisha yao ya kila siku.

“Kazi mnayoifanya mnapaswa kuiheshimu kwa kiasi kikubwa kwani haina tofauti na kazi ya mtu anaenda ofisini kila siku asubuhi, nidhamu katika kazi yako ni chachu ya maendeleo” alisema Mhe, Ndemanga.


Vilevile Mgeni Rasmi aliwataka maafisa wa zimamoto kupita katika kila ofisi ya serikali kuangalia kama wanamifumo na vifaa vya kuzimia moto na ofisi itakayokosa vifaa hivyo basi mara moja iweke vifaa hivyo.

“Siyo tu maofisini hata katika taasisi zote za serikali kama shule na zahanati inapaswa ziwe na vifaa hivyo kwani hizi ni sehemu za mfano hata kwa jamii, wekeni vifaa vya zima moto katika maeneo hayo muhimu”alisema Ndemanga.

Pia Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kupunguza Umasikini na Kutunza Mazingira(APEC) Masalu Regu Rwandiko alitoa shukurani na kuiomba serikali kuendelea kuipatia ushirikiano taasisi hiyo inapofika katika Wilaya au Mmkoa kwa ajili ya kutoa huduma za elimu ya Usalama barabarani, elimu ya ujasiliamali na ulinzi shirikishi kwa waendesha pikipiki.

Masalu alisema kwa elimu wanayoitoa katika maeneo mbalimbali inasaidia  kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali barabarani na kwa Wilaya ya Ruangwa ajali zimepungua kwa asilimia 76 .

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti aliwataka wakazi wa Ruangwa kutumia fursa zinazojitokeza kama ya kukopeswa pikipiki ambapo mkopeshwaji atapaswa kulipia kiasi cha fedha laki 4 za kitanzania kwa kuanzia alafu atapewa pikipiki hiyo na ataendelea kulipia kidogokidogo huku akiwa amekabidhiwa pikipiki yake

Aidha Mhe, Mkirikiti aliwataka vijana kuacha kukaa katika vijiwe muda wa kazi, fursa hizo zinajitokeza wanapaswa kuzipokea kwa mikono miwili na kuanza kufanya utekelezaji wake.

“Ikifika 2018 sitaki kuona vijiwe na nitavivunja mchana kweupe ndani ya Wilaya yangu sitaki watu wazembe na ndiyo maana nilipambana katika kuvunja vijiwe vyote vya (pull table) sasa ikifika huo mwaka nitamaliza vijiwe vyote vilivyobaki”alisema Mhe, Mkirikiti.

Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha wananchi wa Mkoa Lindi na walio nje ya Lindi kuhudhuria katika sikukuu ya Maulidi ambayo kitaifa itafanyika katika Wilaya ya Ruangwa mkesha tarehe 30/11/2017 na sikukuu yenyewe itakuwa 1/12/2017.


“Karibuni tushereke siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W) tumejiandaa kupokea wageni kila mwenye nafasi anakaribishwa kujumuika na wanarungwa katika siku muhimu kama hiyo”alisema Mhe, Mkirikiti.




Ndugu Selemani Issa akiwa anakimbia na gunia kabla ya kilele cha maadhimishi kulianza michezo mbalimbali

Selemani issa akiwa anapokea mkono wa hongera kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi baada ya kushinda kukimbia kwa gunia

Washiriki wa kuvuta kamba wakishindana kuvuta kamba katika uwanja wa shule ya msingi Likangala

Mshirikia wa mchezo wa kukimbiza kuku maarufu kama Yondo sista akiwa ameshika kuku aliyemkimbiza wakati wa shindano hilo



Maandamano ya washiriki walifunzu mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani, elimu ya Ujasilimia Mali na Ulinzi na shirikishi kwa Waendesha pikipiki

Wanafunzi wa shule ya Msingi Likangara na Ruangwa wakiwa kwenye maandamano siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki Nenda Kwa Usalama Barabarani

Katikati)Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Shaibu Ndemanga (kulia kwake) Kamanda wa Polisi Mkoa Renata Mzinga (RPC) na (kushoto) Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakipokea maandamano ya washiriki waliopata elimu kutoka kwa( APEC)

(kushoto)Mkuu wa Polisi Wilaya (katikati)Mkuu wa TAKUKURU Edings Mwakamboja wakipokea msafara wa maandamano

Mgeni Rasmi Shaibu Ndemanga akisaini kitabu cha wageni katika banda la TAKUKURU alipokuwa anatembelea mabanda

Afisa TAKUKURU Angela Mwakalambo akitoa maelezo kwa wageni baada ya banda lao kutembelewa


Mtekenelojia wa Maabara Godfrey Eriyo akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi baada ya kutembelea baada la Afya


Mgeni Rasmi akioneshwa vifaa vinavyotumika barabarani na maaskari kwa ajili ya kudhibiti mwendo kasi

Mgeni Rasmi akitokea kukagua mabanda yaliyopo katika viwanja vya likangala

Wacheza ngoma wa Ndege la Jeshi wakitumbuiza katika kilele cha Maadhimisho ya Kilele cha Wiki Nenda Kwa Usalama

Mhe, Ndemanga akipokea zawadi ya kitamba cha suti kutoka kwa washiriki waliofunzu mafunzo yaliyotolewa na (APEC)

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO) Joseph Shilinde akizungumza na wananchi katika siku ya kilele cha Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani


Mgeni Rasmi akihutubia siku ya Kilele cha Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Kimkoa Katika Wilaya ya Ruangwa


Mshiriki wa mafunzo yaliyotolewa na (APEC) akipokea cheti na mwanamke pekee aloiyeshirikia katika mafunzo hayo ya elimu ya usalama barabarani, elimu ya ujasilimia mali na ulinzi shirikishi kwa waendesha pikipiki.

Kipa wa timu ya Bodaboda akienda kupokea zawadi ya timu yao baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mpira wa miguu

Mwanafunzi wa shule ya msingi Ruangwa akienda kupokea zawadi kwa niaba ya wanakwaya wenzie baada ya kushinda nafasi ya tatu

Mwananfunzi wa Shule ya Msingi ya Likangala akipokea zawadi kwa niaba ya wanakwaya wenzie baada ya kuibuka wa shindi wa kwanza


Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akifunga Kilele cha Maadhimishio Ya Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani





Sunday, 8 October 2017

Mhe, Kigwangala Ameagiza Kukarabatiwa Kwa Vyumba Vya Upasuaji Katika Vituo Vya Afya Ruangwa

NA MWANDISHI WETU

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Hamisi Kigwangala ameuangiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kumalizia chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Mandawa kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia 06/10/2017.

Pia aliagiza kumaliziwa kwa chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Mbekenyera kwa muda wa miezi 3 kwa kubadilisha vyumba vilivyokusudiwaa kwa wodi za wazazi kuwa jengo la upasuaji.

Mhe, Naibu Waziri aliyasema haya wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Ruangwa tarehe 06/10/2017 alipotembelea vituoa vya Afya vilivyopo katika Wilaya hiyo ambavyo ni Kituo cha Afya cha Luchelegwa, Nkowe, Mbekenyera, na Mandawa pia alipata nafasi ya kutembelea zahanati ya Nandagala.

Naibu Waziri alisema katika utawala huu wa awamu ya tano ni lazima kila kituo cha Afya kiwe na chumba cha upasuaji, hivyo ni bora kuwa na chumba kidogo kuliko kukosekana kabisa  chumba cha upasuaji.

“Mhe Mkuu wa Wilaya wewe hapa hauna vituo vya Afya una zahanati zenye majengo mengi vituo hivi vinamapungufu mengi ila ni lazima kuwepo na vyumba vya upasuaji ili kusaidia na kukidhi mahitaji ya wananchi” alisema Kigwangala.

Pia Naibu Waziri Kigwangala alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuwezesha kupatikana kwa maji katika vituo vyote vya afya vilivyopo katika wilaya hiyo alisisitiza kupatikana kwa maji katika hospitali kubwa na kubadilisha mabomba yaliyopo sasa katika vituo na hospitali ya wilaya.

Vile vile Naibu Waziri Kigagwala aliutaka uongozi wa hospital kufanya mchakato wa kufunga mfumo wa kielektroniki(GoT HOMIS) kwenye maeneo mengine na si kuishia mapokezi tu kama ilivyo sasa ili kudhibiti vyema mapato yanayoingia katika vituo hivyo na Hospitali ya Wilaya.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo alimuomba Mhe, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii na Jinsia Dr, Kigagwala awasaidie  upatikanaji wa ramani rahisi zenye gharama nafuu kwa wananchi.
Dr, Simeo alisema ramani zilizoletwa Halmashauri zina na makadirio makubwa ya fedha ambayo kwa uhalisia utekelezaji wake unakuwa ni mgumu kwa wananchi.

“Sera ya sasa inawataka wananchi waanze kufanya shughuli za kimaendeleo kama ujenzi wa Zahanati mpaka kwenye boma alafu Halmashauri zimalizie ila kwa makisio ya fedha zinazokuwa zinaletwa inakuwa ngumu kwa wananchi kutekeleza Mhe, Kigagwala naomba suala hili ukatusaidie lipatiwe ufumbuzi kutokana na hali za wananchi wetu”alisema Dr, Simeo
kushoto) Mhe, Naibu Waziri Kigwagala akiwasili katika kituo cha Afya cha Luchelegwa baada ya kutoka Lindi Mjini.(kulia) Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti

Afisa Tabibu Msaidizi wa Kituo cha Afya Luchelegwa Godfrey Kalembo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr, Kigwagala alipotembelea kituo cha Afya Luchelegwa

Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo akiwa anatoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dr, Kigwagala katika kituo cha Afya Luchelegwa

(kushoto)Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Nandagala Chikongwe akiwa anateta jambo na Mhe, Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akisaini kitabu cha wageni katika zahanati ya Nandagala alipofanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya hiyo

Wambele) Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo akimuongoza Mhe Naibu Waziri alipokuwa anatoka kukagua jengo la wodi ya kina mama


Mhe, Kigwagala akikagua ujenzi wa chumba cha kujifungulia kina mama na chumba cha upasuaji katika zahanati ya nandagala unaoendelea kujengwa

(wakatika) Mhe Diwani wa kata ya Nandagala akimsindikiza Mhe Naibu waziri alipomaliza kukagua majengo katika zahanati ya nandagala

moja ya Jengo la wodi ya kina baba na kina mama katika zahanati ya Nandagala

(kushoto)Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti na kulia ni Naibu waziri wa Afya akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha afya Nkowe

Mhe, Kingwagala akikagua chuma cha kujifungulia kina mama katika kituo cha Afya Nkowe

Naibu Waziri akielekea kukagua majengo yaliyopo katika Kituo cha Afya Nkowe alipofanya Ziara yake katika Wilaya ya Ruangwa

Naibu Waziri wa Afya Dr, Kigwagala akiwaaga wauguzi wa kituo cha Afya Nkowe baada ya kumaliza kukagaua miundombinu katika kituo hiko

Naibu Waziri Kigwagala akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ruangwa Dr, Regan alipotembelea hospital hiyo

Naibu Waziri akiongea na  Fundi sanifu Maabara alipotembelea maabara ya Hospitali ya Wilaya

Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Simeo akimuonesha Naibu Waziri wa Afya Kigwagala taa ya chumba cha upasuaji kuthibitisha kama inafanya kazi


Dr, Simeo akimuona Naibu Wzairi jengo lilalotegemewa kuwa chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Mbekenyera

Mhe, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto chumba kitakachofanywa kuwa chumba cha upasuaji