NA MWANDISHI WETU
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Hamisi Kigwangala ameuangiza uongozi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kumalizia chumba cha upasuaji cha Kituo cha
Afya Mandawa kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia 06/10/2017.
Pia aliagiza kumaliziwa kwa
chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Mbekenyera kwa muda wa miezi 3 kwa
kubadilisha vyumba vilivyokusudiwaa kwa wodi za wazazi kuwa jengo la upasuaji.
Mhe, Naibu Waziri aliyasema
haya wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Ruangwa tarehe
06/10/2017 alipotembelea vituoa vya Afya vilivyopo katika Wilaya hiyo ambavyo
ni Kituo cha Afya cha Luchelegwa, Nkowe, Mbekenyera, na Mandawa pia alipata
nafasi ya kutembelea zahanati ya Nandagala.
Naibu Waziri alisema katika
utawala huu wa awamu ya tano ni lazima kila kituo cha Afya kiwe na chumba cha
upasuaji, hivyo ni bora kuwa na chumba kidogo kuliko kukosekana kabisa chumba cha upasuaji.
“Mhe Mkuu wa Wilaya wewe
hapa hauna vituo vya Afya una zahanati zenye majengo mengi vituo hivi
vinamapungufu mengi ila ni lazima kuwepo na vyumba vya upasuaji ili kusaidia na
kukidhi mahitaji ya wananchi” alisema Kigwangala.
Pia Naibu Waziri Kigwangala
alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuwezesha kupatikana kwa maji katika vituo
vyote vya afya vilivyopo katika wilaya hiyo alisisitiza kupatikana kwa maji
katika hospitali kubwa na kubadilisha mabomba yaliyopo sasa katika vituo na
hospitali ya wilaya.
Vile vile Naibu Waziri
Kigagwala aliutaka uongozi wa hospital kufanya mchakato wa kufunga mfumo wa
kielektroniki(GoT HOMIS) kwenye maeneo mengine na si kuishia mapokezi tu kama
ilivyo sasa ili kudhibiti vyema mapato yanayoingia katika vituo hivyo na
Hospitali ya Wilaya.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya
Dr, Japhet Simeo alimuomba Mhe, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii na
Jinsia Dr, Kigagwala awasaidie upatikanaji wa ramani rahisi zenye gharama
nafuu kwa wananchi.
Dr, Simeo alisema ramani zilizoletwa
Halmashauri zina na makadirio makubwa ya fedha ambayo kwa uhalisia utekelezaji
wake unakuwa ni mgumu kwa wananchi.
“Sera ya sasa inawataka
wananchi waanze kufanya shughuli za kimaendeleo kama ujenzi wa Zahanati mpaka
kwenye boma alafu Halmashauri zimalizie ila kwa makisio ya fedha zinazokuwa
zinaletwa inakuwa ngumu kwa wananchi kutekeleza Mhe, Kigagwala naomba suala
hili ukatusaidie lipatiwe ufumbuzi kutokana na hali za wananchi wetu”alisema
Dr, Simeo
|
kushoto) Mhe, Naibu Waziri Kigwagala akiwasili katika kituo cha Afya cha
Luchelegwa baada ya kutoka Lindi Mjini.(kulia) Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti |
|
Afisa Tabibu Msaidizi wa Kituo cha Afya Luchelegwa Godfrey Kalembo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr, Kigwagala alipotembelea kituo cha Afya Luchelegwa |
|
Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo akiwa anatoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dr, Kigwagala katika kituo cha Afya Luchelegwa |
|
(kushoto)Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Nandagala Chikongwe akiwa anateta jambo na Mhe, Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti |
|
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto akisaini kitabu cha wageni katika zahanati ya Nandagala alipofanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya hiyo |
|
Wambele) Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo akimuongoza Mhe Naibu Waziri alipokuwa anatoka kukagua jengo la wodi ya kina mama |
|
Mhe, Kigwagala akikagua ujenzi wa chumba cha kujifungulia kina mama na chumba cha upasuaji katika zahanati ya nandagala unaoendelea kujengwa |
|
(wakatika) Mhe Diwani wa kata ya Nandagala akimsindikiza Mhe Naibu waziri alipomaliza kukagua majengo katika zahanati ya nandagala |
|
moja ya Jengo la wodi ya kina baba na kina mama katika zahanati ya Nandagala |
|
(kushoto)Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti na kulia ni Naibu waziri wa Afya akisaini kitabu cha wageni katika kituo cha afya Nkowe |
|
Mhe, Kingwagala akikagua chuma cha kujifungulia kina mama katika kituo cha Afya Nkowe |
|
Naibu Waziri akielekea kukagua majengo yaliyopo katika Kituo cha Afya Nkowe alipofanya Ziara yake katika Wilaya ya Ruangwa |
|
Naibu Waziri wa Afya Dr, Kigwagala akiwaaga wauguzi wa kituo cha Afya Nkowe baada ya kumaliza kukagaua miundombinu katika kituo hiko |
|
Naibu Waziri Kigwagala akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ruangwa Dr, Regan alipotembelea hospital hiyo |
|
Naibu Waziri akiongea na Fundi sanifu Maabara alipotembelea maabara ya Hospitali ya Wilaya |
|
Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Simeo akimuonesha Naibu Waziri wa Afya Kigwagala taa ya chumba cha upasuaji kuthibitisha kama inafanya kazi |
|
Dr, Simeo akimuona Naibu Wzairi jengo lilalotegemewa kuwa chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Mbekenyera |
|
Mhe, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto chumba kitakachofanywa kuwa chumba cha upasuaji |