NA Mwanakheri Ally
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ,Mhe, Rashidi Nakumbya amewata wakazi wa Wilaya ya Ruangwa kumuunga mkono
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa.
Amewataka wananchi kufanya kazi bega kwa bega na Mhe,
Waziri katika kuleta maendeleo katika wilaya ya Ruangwa kwa Kushiriki shughuli za kimaendeleo alisema,maendeleo
katika wilaya hii ni jukumu la kila mkazi wa eneo hili.
Alisema haya wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani
lililofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Mei 17 mpaka 18 katika ukumbi wa
Rutesco mjini Ruangwa.
Mhe, Nakumbya aliwataka waheshimiwa Madiwani wa Wilaya
ya Ruangwa kuhakikisha wanatumia nafasi zao katika kuhamasisha wananchi wao
katika kuchangia kufanya shughuli za kimaendeleo katika kata zao.
“Nisiwe mchoyo wa kushukuru kama watu wamefanya vizuri
basi ni wajibu wangu kuwapa pongezi, nawapongeza wananchi wa kata ya Nachingwea
na Ruangwa kwa kazi nzuri ya waliyoifanya ya kujitolea katika ujenzi wa shule ya mpya ya
Sekondari Kassim Majaliwa” alisema Mhe, Nakumbya.
Aidha alimtaka Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue kuongea
vizuri na wachimbaji wa visima waliopo katika
wilaya kwa ajili ya kuchimba visima, waanze na shule ya sekondari mpya kwani
ikianza bila maji itakuwa shida kwa wanafunzi na walimu.
“Shule yetu ni nzuri sana ila itaendelea kuwa nzuri pale
maji yatakapopatikana, maji ni uhai hatuwezi kuanza kutumia shule hiyo bila
kuwa na maji kwani itakuwa mateso kwa
watoto wetu wakike pamoja na walimu ” alisema Mhe, Nakumbya.
Pia Mhe, Nakumbya aliwataka wananchi wa wilaya ya
Ruangwa kuhakikisha wanasafisha mashamba yao ya mikorosho ili mgao wa dawa ya
kupulizia utakapofika kila Mkulima aweze kupata dawa hiyo na pia alisisitiza
itazingatiwa zaidi kwa wale ambao wenye mashamba masafi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Mhe,
Eliasi Nkane aliwaomba wakuu wa shule na Afisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha
wanafuatilia sheria ya mtoto anayeaacha kwani watoto hawa wasipochukuliwa hatua
inasababisha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaoacha shule.
“Zama za sasa imepunguza sana idadi ya watoto wa mitaani
hivyo walimu na maafisa elimu ni wajibu wao kuwachukulia hatua watoto hawa
wanaocha masomo ili tuzidi kutokomeza suala la watoto wa mtaani” alisema mhe Nkane.
|
(kushoto)Diwani wa kata ya Namichiga Mikidadi Mbute akiwa anasikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri akizungumza na (kulia) Diwani wa viti maalumu |
|
Mhe, Diwani wa kata ya Mbwemkuru Selemani Likuche akiwa anawasilisha taarifa ya kata yake |
|
Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japheti Simeo akiwa anajibu hoja |
|
Wataalamu kutoka halmashauri wakiwa wanasikiliza uwasilishwaji wa taarifa za kata na Madiwani |
|
Wakuu wa idara na vitengo wakiwa wanasikiliza uwasilishwaji wa tarifa |
|
Waheshimiwa Madiwani wakiwa wanafuatilia kwa umakini mkutano wa Baraza |
|
Mhe, Diwani wa kata ya Luchelegewa Jaffari Chande akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mtendaji |
|
Waheshimiwa wakiwa wanasikiliza kwa umakini Mkutano ukinaendelea |
|
(katikati)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Rashidi Nakumbiya (kulia kwake) Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Shabani na kushoto kwake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri |
|
Mkuu wa Idara ya Fedha Frank Chonya akiwa anajibu hoja iliyoulizwa na Mhe, Diwani |
|
Diwani wa Viti Maalum Paulina Mmuya akiwasilisha Taarifa ya kata ya Nachingwea |
|
Diwani wa kata ya Ruangwa Mhe, Omari Pendeka akiwasilisha taarifa ya kata yake |
|
Afisa Elimu Sekondari Bihuria Shabani akijibu hoja iliyouliza |
|
Mhe, Diwani wa Viti Maalumu Amina Naenje akiwasilisha taarifa ya kata ya Mnacho |
|
kushoto) Mwandishi wa Mkutano Bashiri Kauchumbe akiwa anafuatilia mkutano unavyoendelea |
|
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lawrence Mapunda akijibu hoja iliyotoka kwa Mhe, Diwani |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri akitoa ufafanuzi kwa wajumbe na waheshimiwa Madiwani |
|
|
Wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Baraza la Madiwani wakifuatilia mjadala iliyokuwa inaendelea |
|
(kushoto) Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani na kulia kwake mkuu wa idara ya Mipango |
|
Kiamu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Moses Mkwesela akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sheria |
|
Diwani wa kata ya Nandagala Chikongwe akiuliza swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbya akifunga Mkutano wa Baraza |