Wakulima Wilayani Ruangwa, wameaswa kushiriki utekelezaji
wa dhamira ya kufikia na kufanikiwa mpango wa serikali wa kuwa na nchi yenye
uchumi wa viwanda.
Wito huu alitolewa na
Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Amour Hamad Amour, wakati akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Nandalaga alipotembelea shamba na kiwanda cha
kukamua mafuta ya zao la Alizeti.
Aliwataka wananchi kuongeza bidii katika sekta ya kilimo
ambayo itapelekea kuwa na viwanda kwa wingi kwasababu kilimo na viwanda ni vitu
viwili vinavyotegemeana. Wakulima wanao wajibu
wa kushiriki kikamilifu katika kuifanya nchi kufikia uchumi wa viwanda kupitia
sekta ya kilimo.
Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya
Ruangwa ni wakulima, hivyo wanayo nafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali
kupitia kazi wanazofanya. Amour, alifananua kuwa ili wakulima waweze kufanikisha
azima hiyo wanapaswa kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha
kawaida na kwenda kwenye kile cha viwanda.
"Badala ya kuuza mazao ghafi, wakulima wanapaswa
kufikiria kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeongeza
thamani mazao mnayozalisha na mtakuza uchumi wenu wenyewe" alisema Amour.
Aidha alisema kama Tanzania ikifanikiwa kuwa nchi ya
viwanda, basi kutakuwa na faida nyingi kama kuongeza ajira ya mtu mmoja mmoja,
kukuza uchumi wa taifa na kubadilisha mfumo wa maisha kutoka katika hali duni
mpaka kuwa na hali nzuri.
"Lengo ni kuona hadi kufika mwaka 2025, wananchi
wameondoka kwenye lindi la umasikini na kufikia uchumi wa kati. Ila kufanikiwa
katika suala la viwanda inabidi wananchi wakazane kufanya kilimo kwa wingi na wabadili mbinu za kilimo" alisema
Amour.
Vile vile alimtaka Mkuu wa Wilaya kuweka mkakati wa kuzuia
matumizi mabaya ya chandarua kwasababu wananachi wanabadili matumizi ya vyandarua. Badala ya kufunga kwenye vitanda vyao wanafunga kwenye bustani zao. Hivyo
aliwataka wananchi kuwa na fikira za kubadilika na si kuishi kwa mazoea.
Wakati huo huo, Mkimbiza Mwenge , Fredirick Joseph Ndahani, alitoa pongezi
kwa uongozi wa Wilaya kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kusisitiza Halmashauri kuongoza jitihada
za kusaidia vikundi vya wajasiriamali na hasa vijana.
|
Mkuu wa Wilaya Lindi Shaibu Issa Ndemanga akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Rukia Muwango |
|
Mkimbiza Mwenge Uhuru Bahati Mwaniguta Lugodisha akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru Kitaifa |
|
Mkimbiza Mwenge Bahati Lugodisha akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Talawa Twaha Mpembenwe |
|
(katikati)Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour(kushoto kwake)Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue na (kulia kwake)Kaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango (kushoto kwake) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe |
|
Wakuu wa Idara wakiwa wanausubiri Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili katika uwanja wa shule ya msingi Nandagala |
|
Katikati)Kaimu Mkuu wa Idara ya Tehama Jitetete Mbonde (kushoto kwake) Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bihuria Shabani na( kulia) Mkuu wa idara ya Utawala Festo j Mwangalika |
|
Wananchi wakiwa wanasubiri Mwenge wa Uhuru ufike katika kijiji cha Ipingo |
|
Mkimbiza Mwenge Fedrick Joseph Mdahani akiwa anatoa maelezo katika banda la kuku Ipingo |
|
Mkimbiza Mwenge Ndahani akiwa anatoa maelekezo ya vifungashio vya sabuni kwa wakikundi ipigo |
|
Katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue (kulia) Mkimbiza mwenge Bahati Lugodisha na (kushoto) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe |
|
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Hawa Mchopa wakiwa wanasikiliza burudani kutoka kwa mwanafuzni mwenzao |
|
Wananchi wakiwa katika uwanja wakamsikiliza Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiongea |
|
Mwenge wa uhuru Kitaifa ukiwa katika Shule ya Hawa Mchopa |
|
Mkimbiza Mwenge Bahati Mwaniguta Lugodisha akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Nangumbu |
|
Kikundi cha wanawake wakiwa na mafuta waliokamua ya alizeti |
|
Bwana shamba wa Nandagala Amanzi Mbeo akiwa anatoa maelezo ya shamba la alizeti |
|
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa anazungumza na wanakijiji cha Nandagala baada ya kutembelea shamba na kiwanda cha kukamua alizeti |
|
Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiwa anaweka zege katika ndoo kwenye Zahanati ya Nandagala kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili |
|
Wakimbiza Mwenge wakiwa wanaagalia jinsi ya kutega mbu |
|
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anagawa chandarua kwa mwanakijiji wa Nandagala |
|
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anaangalia jinsi amplifaya inavyofanya kazi iliyotengenezwa na kikundi cha Mkuti |
|
Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za lami mjini Ruangwa |
|
Mhandisi wa Ujenzi Mashaka Nalupi akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara za lami mjini Ruangwa |
|
Kaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango akiwa anatoa maelekezo kabla ya kwenda Nachingwea kukabidhi |
|
Mkimbiza Mwenge Fredirick Joseph Ndahani akitoa neno la shukurani baada ya kuwasili Ruangwa mjini |
|
(katikati)Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa ameishakabidhiwa Wilaya ya Nachingwea(kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Bakari Mohamed Bakari |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akiwa anatoka kukabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Nachingwea |