Na Mwanakheri Ally
Naibu Waziri wa Nishati
na Madini Dr. Medadi Kalemani amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa
Lindi kutenga fedha zitakazofanya shughuli ya ‘wiring’ katika taasisi za umma katika msimu wa REA III.
Aliyasema hayo katika
kijiji cha Chinongwe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi alipokuwa
anazindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).
Dr Kalemani aliwataka
wakazi wa Kijiji cha Chinongwe waitumie fursa hiyo vizuri kwa kuweka umeme
majumbani mwao, kwani wamepata bahati katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa
wa Lindi wao wamepata nafasi ya kwanza ya kupata huduma hiyo.
“Umeme ni uchumi, umeme
ni kila jambo tunakila sababu ya kuipongeza Serikali kwa kuhakikisha kuwa kila
mwananchi anapata huduma nzuri za jamiii, hivyo msiishie kuweka umeme majumbani
tu utumieni kufanya shughuli za kiuchumi”alisema Dr Kalemani.
Vilevile alimtaka
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Mkoa wa Lindi kufanya utaratibu wa kuanzisha madawati
ya kuhudumia wateja wenye shida ya kuunganishiwa umeme katika vijiji ambavyo
mradi unapita.
“Sitaki kusikia
mwananchi anatembea kilometa 30 kwenda mjini kufuatilia suala la kuunganishiwa
umeme nataka TANESCO ndiyo muwafuate wateja kwani mteja ni mfalme narudia tena ni mwiko mteja
kumfuata TANESCO” alisema Dr Kalemani.
Pia alimtaka mkandarasi
atakayekuwa anafanya ‘wiring’ katika
makazi ya watu aidhinishwe na TANESCO wenyewe ili kuepuka vishoka na kuepuka
suala la bei kutofautiana wakati zoezi hilo likiendelea.
“TANESCO chondechonde
msiwawekee wananchi wetu bei kubwa ya kufanya ‘wiring’, bei iwe nafuu ili kila mwananchi aweze kupata huduma hiyo,
tunataka kila mwananchi autumie umeme kuanzisha viwanda vidogovidogo”alisema Mh,
Kalemani.
Naye Mkurugenzi wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamohanga alitoa pongezi kwa serikali kwa kuweza
kusimamia na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma nzuri za kijamii.
“Serikali ya awamu ya
tano inataka kila kijiji na vitongoji vyake umeme uweze kuwafikia wakazi wake
na ndiyo maana umeme ni uchumi na umeme ni kila kitu wananchi watumie fursa hii
vizuri”, alisema Namhanga.
Nyamohanga alisema vijiji
348 vilivyopo katika Mkoa wa Lindi vinatakiwa vipatiwe umeme, ila Wakandarasi
wataanza na vijiji 175 ambavyo kazi yake itafanyika kwa wiki 24, wakimaliza
hiyo wataendelea na vijiji 173 vitakavyobaki.
|
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalemani baada ya kuwasili sehemu ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa baada ya kuwasili uwanjani Chinongwe |
|
Dr Kalemani akiwasili katika kijiji cha Chinongwe alipoenda kuzindua mpango wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Dr Kalemani akisalimia wanakikundi cha ngoma wa kijiji cha chinongwe alipowasili |
|
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akinong'ona na Dr kalemani kabla ya tukio la
uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Chinongwe |
|
(kushoto) Dr Kalemani, (katikati) Katibu Tawala wa Mkoa Ramadhani Kaswa
na (kulia) Mhandisi Gissima Nyamohanga wakiwa katika uwanja wa uzinduzi
wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme mkoa wa Lindi wakiwa katika uwanja wa uzinduzi wakisubiri mgeni rasmi awasili |
|
(aliyevaa koti la rangi ya maziwa)Mganga Mkuu wa Wilaya Dr Japhet Simeo
wapili yake Mkuu wa Kitengo cha Ugavi Oscar Magoge wakiwa katika
uzinduzi wa REA III |
|
Wananchi wa Kijiji cha chonongwe wakiwa katika uwanja wa Uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akiwa anasikiliza hotuba ya Mhe Naibu Waziri |
|
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akienda kutunza
wacheza ngoma wa jeshi la dege wa Wilayani Ruangwa na nyuma yake ni Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti |
|
Wanakikundi cha dege la jeshi wakiwa wanatumbuiza katika uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha chinongwe |
|
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ruangwa Twaha Mpembenwe akitoa utambulisho wa watu alioambatana nao kutoka wilaya ya Ruangwa |
|
Diwani ya kata ya Luchelegwa Jaffari Chande akisalimia wakazi wa Chinongwe na wageni kwa niaba ya Diwani wa kata hiyo |
|
Mkuu wa Wilaya Mhe, Joseph Mkirikiti akisalimia wakazi wa Chinongwe na akitumia bafasi hiyo kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa aweze kumkaribisha Mgeni rasmi |
|
Katibu Tawala Mkoa Ramadhani Kaswa akimkaribisha Mgeni Rasmi ili azindue Mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Wakazi wa chinongwe wakiwa na furaha ya kupelekewa umeme katika kata hiyo wakiwa katika uwanja wa uzinduzi |
|
Dr Kalemani akiongea na wakazi wa chinongwe alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
Wafanyakazi wa TANESCO wakiwa wamebeba vifaa vya UMETA wakisubiri Dr Kalemani aweze kuvigawa kwa wazee |
|
Dr Kalemani akigawa vifaa vya umeta kwa wazee wasiojiweza wa kijiji cha
Chinongwe alipoenda kuzindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu
katika mkoa wa Lindi |
|
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akikata utepe kwenda katika jiwe la uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika Mkoa wa Lindi |
|
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kalemani akizindua mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu katika Mkoa wa Lindi |
|
Diwani ya kata ya Luchelegwa Jaffari Chande akiangalia jiwe la uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu |
|
jiwe la uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu lililoweka na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalemani
|