Na: Mwanakheri Ally
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji-Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Omari Pendeka, amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kushiriki katika shughuli za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata au Vijiji vyao na kujua kuwa miradi hiyo ya kimaendeleo kama vile Zahanati, Barabara na Shule zinazojengwa ni mali ya Wananchi wenyewe na si Serikali.
Mhe. Omari Pendeka ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wanakamati wa Huduma za Jamii wakati wa Ziara ya Kamati ya Elimu Afya na Maji walipokuwa wanatembelea na kuhamasisha shughuli za Maendeleo katika Kijiji cha Namilema na Mbekenyera.
Kaimu Mwenyekiti huyo aliwataka Wanakamati kuwasimamia Mafundi kwa ukaribu ili kufanikisha shughuli hizo kwa muda uliopangwa, pia aliwataka Wanakamati kuwahamasisha Wananchi ili waweze kujitolea pale ambapo watakuwa wanahitajika.
|
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji, Mhe. Omari Pendeka(katikati) akiwa anazungumza na Wanakamati wa Huduma za Jamii, Diwani wa Viti Maalum Nandagala Amina R Naenje(kushoto) kulia Diwani likuche wa Mbwemkuru |
|
Wajumbe ya kamati ya Maji, Afya na Elimu wakiwa wanapata utambulisho kutoka kwa wenye kamati ya ujenzi kijiji cha Namilema |
|
Mafundi wakiwa wanaendelea na ujenzi katika Shule ya Msingi Namilema |
|
Wajumbe wa kamati ya Elimu Afya na Maji wakiwa wamewasili katika eneo linalotarajiwa kujengwa Zahanati ya Namilema |
|
Wajumbe wa Kamati ya Elimu Afya na Maji wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa ni Madiwani na Wakuu wa Idara |
|
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na Maji akiwa anawasili shule ya Sekondari Mbekenyera kukagua miradi iliyopo shuleni hapo(kulia) Afisa Elimu Taaluma Robert Bujiku |
|
Mkuu wa Shule ya Mbekenyera Shanly Nchimbi akiwa anasoma taarifa fupi kwa wanakamati ya Elimu Afya na Maji waliofika shuleni hapo |
|
Moja ya madarasa yaliyokwisha kamilika shule ya sekondari Mbekenyera |
|
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbekenyera Mikidadi Mbule akiwa anatoa maelezo ya mradi wa ujenzi ya wodi ya akina Mama ulipofikia kwa wanakamati wa Elimu Afya na Maji. |
|
Kaimu Mwenyekiti akiwa anaongea na Wanakamati katika Kituo cha Afya Mbekenyera |
|
Wanakamati wakiwa wanakagua ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Mbekenyera |
|
Yusuf Chilumba Afisa Elimu Ufundi akiwa anaiongoza kamati ya Elimu Afya na Maji kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo unaofanyika shuleni hapo |