Monday, 31 July 2017

Mhe, Nakumbiya Amewata Viongozi Wa Amcos Kuwa Wa Adilifu Katika Kutekeleza Majukumu YaoNA MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe,Rashidi Nakumbya amewataka viongozi wapya wa vyama vya ushirika (Amcos) kufanya kazi kwa uadilifu katika kutekeleza majukumu yao.

Mwenyekiti alisema viongozi waliobahatikia kupata nafasi katika vyama vya Amcosi waitumie nafasi hiyo kwa kufanya mambo yenye manufaa kwa wanaushirika na wanakulima wao.

Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika Julai 28 mpaka 29 2017, katika ukumbi wa Rutesco Mjini Ruangwa.

Nakumbya alisema kipindi kilichopita baadhi ya viongozi wa Amcos walitumia madaraka yao vibaya kwa kuhujumu mali za wanachama hali iliyopelekea wanachama kukosa imani na viongozi wao.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti aliwataka waendesha bodaboda kufuata sheria za barabarani kama zinavyoelekezwa na vyombo vya usalama.

“Vijana wetu wanajisahau sana huko barabarani na hasa vijijini ambako wanaona hakuna  maaskari, wanabebana watu wanne pikipiki moja hili jambo ni hatari kwa usalama na maisha yao”alisema Mhe, Mkirikiti.

Pamoja na hayo mkuu wa wilaya alizungumzia rasilimali ya madini ambayo ina wawekezaji wengi na inakua kwa kasi sana wilayani Ruangwa akiitaka iangaliwe kwa undani ili kuepusha migogoro na upotezaji wa mapato ya serikali

” Watu wa madini tunatakiwa tuwaangalie kwa jicho la ndani zaidi” alisema Mh.Mkirikiti.

Aidha Mhe Diwani wa Kata ya Nandagala Mh. Chikongwe alitoa pongezi kwa Menejimenti ya wilaya ya Ruangwa na hasa Mkurungenzi Mtendaji  kwa juhudi alizozifanya za kuiendesha Halmashauri.

“Wakati Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue anafikia katika Halmashuari hii aliikuta madeni mengi sana ila kwa uchapakazi wake aliweza kupunguza madeni hayo kwa kiasi kikubwa na kuifanya Halmashauri kuwa katika hali nzuri mpaka sasa”alisema Chikongwe.Add caption

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ili afungue Mkutano wa Baraza


Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbiya akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani
Wataalamu wa Halmashauri wakiwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani

Afisa Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akiwa anatoa nasaha zake kwa Wazazi na Mwanafunzi wa Kidato cha tano

Afisa Maendeleo ya Jamii Grace Mwambe akimkabidhi Zainabu Fedha alizochangiwa na Watumishi wa Halmashauri kwa Lengo la kwenda Kidato cha Tano


Waheshimiwa Madiwani wakiwa wanafuatilia Taarifa ya Mkurugenzi kwa umakini zaidi

Mwakilishi Kutoka Taasisi ya Namaigo Abdallah Said akiwa anatoa maelezo ya huduma wanazozitoa

Diwani wa Kata ya Nadagala Mhe, Chikongwe akiwa anatoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Menejimenti

Mhe, Diwani akiwa anauliza swali kwa Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri

(kulia) Diwani wa Viti Maalumu Paulina Muya na (kushoto) Diwani wa Kata ya Mandawa wakiwa kwenye kikao cha Baraza

Mhe, Diwani wa Viti Maalumu akiulizwa swali kipindi cha maswali na majibu

Mhe, Diwani wa Kata ya Nandagala akiwa anaomba kura kwa Madiwani wengine baada ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti


Mhe, Diwani wa Viti Maalumu akiwa anaomba kura kwa Madiwani wengine baada ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti


Mkuu wa Wilaya akiwa anazungumza na Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri katika Mkutano wa Baraza


Katibu Tawala wa Halmashauri Twaha Mpembenwe akiwa anafuatilia Taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji

Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika Mkutano wa Baraza julai 29/ 2017

waandishi wa mkutano wakifatilia kwa makini