Na: Mwanakheri Ally
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa Ndg. Andrea Chezue amewaomba Waheshimiwa Madiwani wamsaidie katika maeneo yao kutokomeza utoro mashuleni na kusaidia kurudisha Watoto walioacha shule kurudi shuleni kama mwanzo.
Alisema ni wajibu wa Halmshauri na Madiwani kuwaunga mkono Idara ya Elimu ili wafanikiwe kumaliza tatizo la utoro sugu na utoro wa reja reja kwani hilo si jukumu la Watu wa Elimu tu ni jukumu la kila Mwananchi wa Wilaya ya Ruangwa.
Ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichoanza tarehe 1 mpaka tarehe 2 Februari 2017 kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa
Aidha, Mkurungezi Mtendaji alisema sambamba na kutokomeza utoro Halmshauri imejipanga kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa ndani ya Wilaya mpaka kufikia Juni 2017 atakuwa amemaliza ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyoitajika
Vilevile aliwataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi ili kuweza kufanikiwa katika malengo yaliyowekwa ya kuwa na Ruangwa yenye maendeleo, kwani inawezekana kama kutakuwa na ushirikiano.
Mkurugenzi aliwaomba Madiwani ambao katika kata zao kuna miradi iliyoanzishwa na Wananchi basi waweze kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi ili, Halmashauri iweze kutia nguvu zake katika kumalizia miradi hiyo kama ilivyoada.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Rashid Nakumbi aliwaambia wajumbe wa Baraza la Madiwani bila ushirikiano hakuwezi kuwa na maendeleo hivyo inapaswa wataalamu wa Halmshauri na Madiwani washirikiane hii itasaidia kuwa na kasi na kuleta maendeleo katika Wilaya ya Ruangwa
Pia aliwataka Madiwani na Wataalamu wa Halmshauri kujitoa kwenye masuala ya kupima Afya kwani hii itasaidia kuwashawishi Wananchi kujitoa kwa hiari kwenda kupima Afya, kabla ya kikao kuanza cha Baraza la Madiwani, Wajumbe walipata nafasi ya kuanza kupima Afya zao kwa hiari.
Naye, Diwani wa Chibula Mhe.Omari Songea kwa niaba ya wa Madiwani wengini alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa jitihada anazozionesha za kuifanya Mji wa Ruangwa kuwa na maendelea na kumuahidi kutoa ushirikiano kama inavyotakiwa ili kuweza kufikia malengo.
|
Mkurugenzi mtendaji Adrea Chezue akiwa anamkaribisha mwenyekiti katika Rashidi Nakumbia( mwisho) Makamu Mwenyekiti Shabani Kambona |
|
Waheshimiwa Madiwani wakiwa kwenye Baraza la Halmshauri |
|
Diwani wa kata ya Matambarare Omari Li akiwa anasoma kwa umakini taarifa |
|
Mwandishi wa Mkutano Bashiru Kauchumbe akiwa anamsikiliza muwasilisha mada |
|
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akiwa anasoma kablasha alilokabidhiwa(kushoto) Mhandisi Fransis Kakama |
|
Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika hali ya utulivu wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmshauri akiongea |
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Maji na Afya mh EliasNkane |
|
Afisa Elimu Msingi akiwa anajibu Hoja za Madiwan(kushoto) kaimu muweka Hazina gervas Bidogo |
|
Waandishi wa Mkutano(kushoto)Bahati Kasambano(kulia) Bashiru Kauchumbe |
|
Afisa Utumishi Festo j Mwanagalika akiwa anajibu hoj zaa kutoka kwa Diwani |
|
Kaimu Afisa Elimu Anna Nasu akiwa anajibu hoja zinazohusiana na masuala ya Elimu iliyoulizwa na Madiwani |
|
Wataalamu kutoka Halmashauri wakiwa wanasikiliza mada zinazowasilishwa |
|
Waheshimiwa Madiwani wakliwa wananyoosha mikono ili wapate nafasi ya kuuliza maswali yao. |
|
Waheshimwa Madiwani wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wakisikiliza hoja zinazowasilishwa |
|
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa kwenye Baraza wakisikiliza hoja zinazowasilioshwa |