Friday, 3 February 2017

BARAZA LA WAFANYAKAZI WILAYA YA RUANGWA WAAFIKI BAJETI YA SHILINGI BILIONI 33.4 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

Na Mwanakheri Ally

Baraza la Wafanyakazi Wilaya ya Ruangwa limeafiki  bajeti iliyopangwa na Halmashauri ya Wilaya  ya mwaka 2017-2018 ambayo ni kiasi  cha Shilingi Bilioni 33.4 baada ya kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Wakuu wa Idara na Vitengo kufuatia kuwasilishwa kwa bajeti hiyo.

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya muwasilisha mada Afisa Mipango Joram Mbiha kuwasilisha bajeti hiyo kama ilivyopangwa na Halmashauri kwa Wajumbe wa Baraza hilo la Wafanyakazi, na Wajumbe hao kupata nafasi ya kutoa hoja zao na kupatiwa majibu na Wakuu wa Idara na Vitengo waliohudhuria kikao hicho.

Hayo yalifikiwa muafaka wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililoshirikisha Wajumbe mbalimbali kisheria, kikao hiko kilifanyika katika ukumbi wa soko la Kilimahewa mjini Ruangwa

Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ali Bakari akiwa anafanya ufunguzi wa Baraza hilo tarehe 30/1/2017 kulia Mwenyekiti wa Baraza........

Afisa Mipango Joram MBiha akiwasilisha mada mbele wa wajumbe wa Baraza

Wajumbe wa Baraza wakiwa wanasikiliza kwa umakini mada inavyowasilishwa na Afisa Mipango


Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akijibu hoja iliyoulizwa na mjumbe.(kushoto) Mwenyekiti wa Baraza Jafarani Mkangumbe (kulia Afisa Mipango Joram Mbiha

Wajumbe wa Baraza wakiwa wanasikiliza kwa umakini mada inavyowasilishwa na Afisa Mipango
Afisa Elimu Msingi Selemani Mrope akitoa ufafanuzi wa hoja iliyoibuka kutoka kwa katibu wa Baraza ndugu Ali Seleman

Mjumbe Amanzi Ndeo ambaye ni Afisa Kilimo Kata ya Nandagala akiuliza swali

Mkuu wa Idara ya Maeandeleo ya Jamii Grace Mwambe akijibu hoja ya Afisa Kilimo wa Nandagala

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Jafarani  Mkangumbe akiwa anateta jambo na Katibu wake bwana Ali Bakari Katoto

Sekretarieti ikiwa inasikiliza hoja wakati baraza likiendelea( kulia) Tunu Naftari na
(kushoto) Avodi Daniel

Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Ruangwa Baltazar Lukanga akiwasilisha hoja yake wakati wa Baraza hiloMganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akijibu hoja ya Katibu wa CWT wakati wa Baraza la Wafanyakazi.