Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kuwa wavumilivu na wenye subira katika suala la kupatikana kwa maji safi na salama katika kila Kijiji kilichokuwa ndani ya Wilaya hiyo, kwani anafanya jitihada za kila namna ili kuweza kumaliza changamoto hiyo.
Alisema ndani ya Uongozi wake wa miaka mitano hii ya mwanzoni anataka kuhakikisha anakabiliana na kumaliza changamoto ya Umeme na Maji katika Wilaya ya Ruangwa, kwani ameshaanza mikakati ya kutafuta Wafadhili watakaowasaidia kuchimba visima virefu na kupima maji kama ni salama kwa matumizi ya Binaadamu.
Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza wa Wananchi wa kijiji cha Chimbila A, Manokwe, Ng'au, na Nadagala wakati wa Ziara yake aliyoifanya ndani ya Wilaya ya Ruangwa siku ya Tarehe 27 mwezi Desemba 2016
Waziri Mkuu akisalimiana na Mkurugenzi wa Nachingwea{DED} Bakari Mohamedi Bakari |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT 843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu |