Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku
kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi
wa huu wa Disemba mpaka Mei 2017.
Shughuli hizo ni pamoja na Unyago, Ndoa na Ngoma
za Majini. Alisema shughuli hizo
zinazofanywa na Wananchi zimekuwa
zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga la njaa mkoani
hapo.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi aliwataka Wananchi kuwa wavumilivu na waelewa
kwani janga la njaa halichagui Mkoa
bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilo kwa Wananchi wote.
“Sitaki kuwa Mkuu
wa Mkoa ambaye Mkoa wangu umekutwa na janga la njaa kwani hii ni aibu
kubwa hivyo Watu wawe makini
katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe".
Wakati huo huo Mhe. Zambi aliwataka Wananchi wa Ruangwa wajenge vyoo imara na
vya matumizi ya muda mrefu, ili kuweza kujiepusha na maradhi ya Kipindupindu
kama ambavyo yanaikabili Wilaya ya Kilwa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa aliwataka Watendaji wa vijiji kusimamia
zoezi la kila Mwananchi wa eneo lake anakuwa na choo imara na Mtu atakaekaidi kufanya ujenzi wa choo
cha nyumbani kwake basi achukuliwe hatua za kisheria.
Vilevile aliwasa
Wananchi kuwa na matumizi mazuri ya pesa wanazoipata za kuuza korosho au fidia
wanazolipwa na kuacha matumizi mabovu ya pesa hizo kama ambaVyo inafanywa na
baadhi ya Watu.
Mhe. Zambi
aliwakata Wananchi kutumia pesa wanazozipata katika kutengeneza maisha yao kama
katika kusomesha Vijana wao na
kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia zao.
Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anaongea na wanakijiji wa Kijiji cha Makanjiro |
Mkuu Wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wananchi wa kijiji cha Mandawa |