Wednesday, 7 December 2016

MKURUGENZI WILAYA YA RUANGWA AWAASA WANANCHI KUSHIRIKI KWENYE SHUGHULI ZA MAENDELEO

Na: Mwanakheri Ahmed
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Ruangwa, Ndugu  Andrea Chezue amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo zinazoendelea Wilayani hapo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa  madarasa.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo katika mkutano alioufanya na Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii (WDC), wakati wa kujadili  suala la kujenga vyumba vya madarasa vinne vinavyotakiwa kujengwa hivi karibuni.

Ujenzi huo wa vyumba vya madarasa manne umefuatia kuongezeka kwa idadi kubwa ya ufaulu wa Wanafunzi Wa darasa la saba kwa mwaka 2016, hivyo kupelekea Wanafunzi  179 kukosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza kwa mwaka 2017.