Na:
Mwanakheri Ally
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, limepitisha
mapendekezo ya mpango wa bajeti kiasi
cha Tsh. 33,499,533,375 kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kati ya fedha hizo ni Tsh.8, 854,027,476 kwa ajili ya ruzuku ya miradi ya maendeleo, Tsh.835,764,000 ni ruzuku ya matumizi ya kawaida,
Tsh 20,828,509,629 mishahara na Tsh.
2,931,240,000 ni mapato ya ndani.
Vipaumbele vya mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/2018
vimegawanyika katika sekta mbalimbali ambazo ni kuboresha huduma za jamii kwenye sekta ya maji, kukarabati barabara, ujenzi wa miundombinu kwa shule za msingi na sekondari na uboreshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji.
Sambamba na mapendekezo hayo ya bajeti Halmashauri imewasilisha ombi
maalumu lenye jumla ya Tsh 3,400,000,000.00 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
Hospitali ya Wilaya ya kisasa na tayari eneo wa ajili ya ujenzi wa mradi huo
limeishatengwa lenye ukubwa wa ekari 60.
Baraza limetilia mkazo suala la ukusanyaji wa mapato ya
ndani kwa kuhakikisha mianya ya ukwepaji kodi inadhibitiwa ili miradi
iliyopangwa kutekelezwa kupitia vyanzo vya ndani iweze kukamilika, Aidha Baraza la Madiwani limeiomba serikali kuleta fedha za ruzuku kama ilivyopangwa ili kufanikisha
malengo ya Halmashauri.
|
Mkurungenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Andrea Chezue akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmshauri Rashidi Nakumbia aweze kufungua kikao maalumu cha Baraza la Halmashauri cha kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Joseph Mkrikiti na wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Mhe.Rashidi Nakumbia akiwa anafungua kikao maalumu cha Baraza la Halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka 2017/2018(kulia) wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe.Joseph Mkirikiti |
|
Waheshimiwa Madiwani wakiwa katika utulivu wakisikiliza Mkurugenzi Mtendaji akiwasilisha Bajeti mbele ya Madiwani na wataalamu kutoka Halmashauri ya Ruangwa |
|
Diwani wa kata ya Makanjiro Saidi kawale akiwa na diwani wa viti maalumu Zuwena Kitatichingi wakiwa wanasikiliza mapendekezo ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/2018 |
|
Mwandishi wa mkutano Bahati Kasambano akiwa anasikiliza na kuandika yanayozungumzwa na Mkurugenzi |
|
Afisa Mipango Thomas Luambano akiwa na Afisa Elimu Msingi Selemani Mrope wakifuatilia uwasilishwaji wa bajeti |
|
Diwani wa kata ya chienjele Rashidi Nnuduma akiwa na Diwani wa kata ya luchelegwa Omari Chande wakiwa wanafuatilia kwa umakini mchakato wa uwasilishwaji wa mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2017/2018 |
|
Afisa Utumishi wa Halmshauri ya Ruangwa Festo j Mwangalika akifuatilia uwasilishwaji wa mapendekezo ya bajeti 2017/2018 |
|
Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri Andrea Chezue pembeni yake Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbia(kulia) Mkuu wa Willaya Joseph Mkirikiti (mwisho) Kaimu Mwenyekiti Shabani Kambona wakiwa wanasikiliza hoja za madiwani |
|
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na Madiwani na Wataalamu wa Halmashauri katika kikao Maalumu cha Baraza la Halmshauri cha Kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 |
|
Wajumbe waliohudhuria kikao maalumu cha baraza la Halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 |
|
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Dr Japhet Simeo akiwa anawasilisha majibu ya wajumbe waliopima Afya jana kabla ya kuanza kikao maalumu cha baraza la halmshauri cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 |
|
|
Waheshimiwa Madiwani wakiwa wapo nje ya ukumbi wa Rutesco kilipofanyika kikoa baada ya kuupitisha mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/2018 |