Sunday, 12 February 2017

WANANCHI WILAYA YA RUANGWA WAHIMIZWA KUPANDA MICHE YA MIKOROSHO ILI KUKUZA UCHUMI NA KUHIFADHI MAZINGIRA

Na: Mwanakheri Ally

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Mama Anna Abdallah amewahamasisha Wananchi wa Mji wa Ruangwa kupanda miche ya korosho kwa wingi katika maeneo yao kama ilivyo kampeni ya upandaji miti inayoendelea.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo alisema "kwani lengo la kupanda miti  ni kuepukana na jangwa na Watu kuwa na sehemu za kupumzikia hivyo basi ni bora kupanda miti ya korosho kwasababu itamsaidia Mwananchi kupata kivuli na pia kuongeza kipato unapofika muda wa kuvuna korosho hizo".

Aliyasema hayo wakati wa kufanya uziduzi wa kampeni ya kupanda mikorosho mipya 5000 katika kila kijiji kwa msimu wa 2016/2017 katika kijiji cha Chimbila 'B' tarehe 10/02/2017 wakati akiongea na Wananchi wa Kijiji hicho.

Pia aliwataka Wananchi kutumia fursa hiyo ya kuwa na miche mipya na kuipanda katika mashamba yao kwani lengo la kuwa na miche hiyo mipya ni kuongeza uzalishaji wa zao la korosho katika Mkoa wa Lindi.

Naye mgeni Rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi aliwaambia Wakuu wa Wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Lindi washindane katika kupanda miche hiyo mipya kwani hii italeta manufaa makubwa katika Wilaya hizo kwa kukuwa kiuchumi.

Alisema Mkuu wa Mkoa "inawezekana kufikia malengo ambayo Halmshauri zimejiwekea kama wataweza kuwahamasisha Wananchi wao kupanda miche mipya na kuwasimamia hao wanaokabidhiwa hiyo miche katika kuipanda na kuihudumia mpaka kufikia kipindi cha uvunaji.

Aidha Mkuu wa Mkoa Zambi aliwaambia Wakulima  wanaokabidhiwa miche hiyo ya korosho waweze kuitunza na waisimamie vizuri bila kuangalia kama wamepewa bure au wamenunua kwani kufanya hivyo itasaidia kuongeza uzalishaji katika zao la korosho.

Bodi ya Korosho Tanzania imefanya uzinduzi wa kampeni ya kupanda mikorosho mipya 5000 kila Kijiji katika msimu wa 2016-2017 katika Kijiji  cha Chimbila 'B' ikiwa ni mwanzo wa uzinduzi ambao utafanyika katika Mikoa mingine tena.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.Godfrey Zambi wa pili kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mama Anna Abdallah wa kwanza kulia wakiwa wanasubiri shughuli ya uziduzi ianze
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania akiwa anaongea na Wananchi wa Kijiji cha Chimbila 'B' wakati wa uziduzi wa kampeni ya kupanda mikorosho mipya 5000, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya korosho Dastani Kaijage na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Twaha Mpembenwe akimkaribisha Mgeni Rasmi aweze kuongea na Wananchi wa Chimbila 'B'


Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akiwa anaongea na Wanakijiji cha Chimbila 'B' na Wataalamu waliohudhulia uzinduzi wa kampeni ya kupanda mikorosho mipya 5000 kila Kijiji


Wanakijiji na Wataalamu kutoka Wilaya za Mkoa wa Lindi wakiwa wanaangalia kikundi cha ngoma kikitumbuiza 

Kikundi cha Ngoma cha Nangumbu Lekatulinge kikiwa kinajiandaa kuingia uwanjani kutumbuiza 

Wapigaji Ngoma wa kikundi cha Lekatulinge wakiwa wanapiga ngoma zao kwa madoido ya kufikisha ujumbe kwa wananchi



Wanakikundi wa Likatulinge wakiwa wanaimba kwa kucheza kwa kufaraha m,bele ya mgeni Rasmi


Mjumbe wa Bodi ya Korosho Edga Maokolo akiwa anatumbuiza mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa baada ya kupewa nafasi ya kipekee 

Miche ya miti ya korosho 4300 ya kikundi cha jitegemee ikiwa imeoteshwa vizuri na ikiwa tayari kwenda kupandwa katika mashamba

Mohamed Chilambo akiwa anasoma risala mbele ya mgeni rasmi kabla ya kumumkabidhi miche ya korosho
Mama Anna akimkabidhi mche wa mkorosho mkulima Asha kwa ajili ya kwenda kupanda shmabani kwake

Mkuu wa Wilaya akiwa anapokea mche wa mkorosho kutoka kwa Afisa Kilimo Vailet Richard kwa ajili ya kwenda kupanda

Mratibu wa Korosho Richard Bendera akiwa anatoa maelezo kwa wakurugenzi watendaji wa halmashauri ya Ruangwa, Liwale na Kiliwa jinsi ya kupanda mche wa korosho

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa akiwa anapanda Mche wake wa Mkorosho katika shamba la mkulima lililochaguliwa

Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa akiwa amemaliza kupanda mche aliokabidhiwa


Mwenyekiti wa Manspaa ya Lindi Makwinya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Adrea Chezue wakiwa wamemaliza kupanda mkorosho
Mwenyekiti wa Manspaa ya Lindi  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa wakiwa wananawa mikono baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Liwale  Justine Monko akiwa anapanda mche aliokabidhiwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Liwale akiwa amemaliza kupanda mti wake na akisubiri kuumwagilia maji

Mjumbe wa Bodi ya Korosho Faith Mitambo akiwa anaandaa mche wake wa ajili ya kupanda

Mkurugenzi wa Manspaa ya Lindi akiwa anafanya maandalizi ya kupandikiza Mche aliokabidhiwa kupanda

Mkurugenzi wa Manspaa ya Lindi Jomaary Mrisho Satura akiwa anapanda mche aliokabidhiwa

Mkurugezi wa Manspaa ya Lindi akiwa amaemaliza kupanda miche wake

Afisa Kilimo wa Wilaya ya Ruangwa akiwa anapanda mche wa mkorosho

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania akiwa ananawa mikono baada ya kumaliza kubanda mti wake