Sunday, 1 January 2017

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMALIZA ZIARA YA SIKU TATU WILAYANI RUANGWA KWA KUFANYA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI NA KUFUNGUA OFISI YA CCM WILAYA YA RUANGWA

Na: Mwanakheri Ahmed

Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa ampongea mzee Juma Libende kwa kutoa eneo lake bure kwa Halmashauri  kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari iliyoanza ujenzi wake Desemba 2016.

Waziri Mkuu amempongeza Mzee huyo na kuwaambia wananchi wengine waigie mfano wa Juma kwani ameonesha uzalendo mkubwa kwa kitendo cha kutoa eneo lake bila kuhitaji malipo ya aina yoyote, alisema hiyo inonesha kuwa Watu wanataka Ruangwa yenye maendeleo.

Aliyasema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ruangwa na kufungua ofisi ya Chama Cha Mapindizu(CCM) Wilaya, Desemba 30, 2016 ikiwa ni mwisho wa Ziara ya Kikazi aliyoifanya Wilayani humo kuanzia Desemba 28 mpaka 30.

Vile vile alifanya harambee ya kuchangisha ili kuweza kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambapo Watu walijitokeza na kutoa ahadi zao na jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa, harambee hiyo ilifanyika sambamba na mkutano wa hadhara aliohutubia Waziri Mkuu mjini Ruangwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM Wilaya.
Waziri Mkuu akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM yaa Wilaya ya Ruangwa

Baadhi ya Wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mjini Ruangwa.




Baadhi ya Wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mjini Ruangwa.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi Wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,Ali Mtopa katika mkutano wa hadhara aliohutubia mjini Ruangwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi Wialyani  Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30 kushoto ni katibu wa CCM wa Wilaya ya  Ruangwa Issa Njijo.




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni  ya Pacco Gems Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Wilayani Ruangwa.



Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nandagala Wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha ya katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaaliwa kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Ruangwa.