NA MWANAKHERI ALLY
Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ramadhani Kaswa amewataka
wanavikundi wa saccos wanaokopa kutoka katika mfuko wa halmashauri kuweza
kurejesha mkopo wao kwa wakati.
Alisema kuweza kufanya hivyo kwa wakati itasaidia kuwapa
nafasi vikundi vingine kuweza kukopa na kubadili kiwango cha maisha kutokana na
biashara watakazokuwa wanafanya.
Ameyasema hayo wakati akiongea na kikundi cha vijana
saccos mjini Ruangwa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maendeleo miradi
ya Halmashauri.
Aidha alisema ni vyema wahasibu wa kwenye saccos wapewe
mafunzo ya kuweza kuendesha mifumo ya utunzaji fedhana vitabu vya kifedha ili
waweze kuandesha saccos zao kitaalamu zaidi na itasaidia kuwa na umakini katika
suala za kifedha.
Wakati huo huo Katibu Tawala alitoa pongezi kwa uongozi
wa Wilaya kwa ujumla kwa kufanikiwa kujenga shule mpya kwa wakati mfupi na kwa
kuzingatia viwango na ubora vya kiufundi
‘’Mazingira ya shule ni mazuri kwa mwanafunzi kupatia
elimu ila mafundi zidisheni kasi ili shule iweze kumalizika mapema na wanafunzi
waanze kutumia majengo yao”alisema
Pia alimtaka Mhandisi wa Maji kufikiria mbinu za kuweza
kuwasaidia Shule ya Sekondari Mbekenyera ili waweze kupata jenereta lao la
kutumia kupampu maji katika kisima.
|
jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya lililopo katika hatua za ukamilishaji |
|
Katibu Tawala Ramadhani Kaswa akiwa anakagua jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ruangwa |
|
Katibu Tawala akiangalia ujenzi ulipofikia wa jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya Joseph Mkirikiti |
|
Katibu Tawala(katikati) na msafara wake wakiwa katika shule mpya iliyopo kata ya Nachingwea |
|
Wanafunzi wakiwa wanafanya usafi katika maeneo ya shule mpya |
|
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotegemewa kuhamia katika shule hiyo mpya wakiwa wanasafisha mazingira |
|
Wanafunzi wakiwa wanapanda maua mbele ya vyumba vya madarasa |
|
Muonekano wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule mpya inayoitwa Kassim Majaliwa |
|
Mtambo wa kusafishi maji uliopo katika kijiji cha Mihewe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa |
|
(Kulia)Mhandisi wa Maji wa Wilaya Lawrence Mapunda akiwa anatoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mihewe |
|
k(kushoto katibu Tawala akiwa anaongea anaangalia eneo lililojengwa jengo kisima cha kuchujia maji(kulia)Afisa Elimu wa Wilaya Bihuria Shabani |
|
(katikati)kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri akiwa anamuonesha(kushoto) Katibu tawala tanki lililojengwa katika kijiji cha mihewe |
|
Tanki la kuhifadhia maji lililojengwa katika kijiji cha Mihewe lenye ujazo wa lita elf 25 |
|
Chumba cha darasa kilichopo katika shule ya Mbekenyera High school |
|
Katibu tawala Ramadhani Kaswa akiwa anaongea na wataalamu kutoka Halmashauri na walimu katika shule ya sekondari Mbekenyera |
|
Baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa wanasikiliz risala inayosomwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo |
|
Mkuu wa Shule ya Mbekenyera akiwa anasoma risala mbele ya katibu tawala wa mkoa wa lindi Ramadhani Kaswa |
|
(kushoto)Katibu tawala akiwa ameongozana na kaimu Mkurungenzi wakielekea katika vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namilema |
|
Katibu tawala akiwa anaangalia mradi wa vyumba vya madarasa Namilema |
|
Wakuu wa idara wakiwa na Katibu Tawala wakiangalia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mbekenyera |