Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Afya, Elimu na Maji imefanya Ziara ya kutembelea na Kukagua Miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ikiwa ni utekelezaji wake kila robo ya mwaka.
kamati hiii iligawanyika katika makundi mawili kundi A na B makundi hayo yalifanya ziara hiyo siku ya tarehe 19/7/2017 kundi A liliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe Eliasi Nkane , na Kundi B liLiongozwa na Mhe wa Kamati akiambatana na wajumbe.
Kamati ilitembelea Miradi ambayo ni Mradi wa kuona shule ya awali , kata ya Nangurugai, Kisima cha Maji , Mihewe , Ujenzi wa Zahanati, Namtatila, , ,Kuona Ujenzi wa vyumba vya madarasa Nambilanje, kuona ujenzi wa Zahanati Chikundi.
Kupitia Ziara hii Mhe Mwenyekiti Eliasi Nkane aliwataka wananchi waendelee kujitolea katika kufanya shughuli za kimaendeleo katika kata zao na kuacha kutegemea kila jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,alisema kijiji kitakachoanzisha mradi kitapewa kipaumbele cha kusaidiwa.
"Halmashauri inamipango mingi ya kimaendeleo kukaa kusubiri yenyewe ndiyo ijekuwaanzishia miradi ni kujichelewesha, tumieni fursa zenu vizuri katika kuanzisha miradi kwani serikali ya Wilaya ipo pamoja na nyie"alisema Nkane
Kaimu Afisa Elimu Kifu akitoa maelezo katika shule ya awali iliyojengwa kwa nguvu za wananchi. |
(kulia)Diwani wa kata ya Mbwemkuru Mhe Likuche na( kushoto) wakiwa wanasikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Elimu Msingi |
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii akiwa anaangalia mazingira ya shule ya awali iliyojengwa kwa nguvu za wananchi |
Mazingira ya Nje ya chumba kinachohifadhi mitambo ya kusafishia maji kijiji cha Mihewe |
Mitambo ya kusafishia maji iliyopo katika kijiji cha Mihewe |
Mwenyekiti wa Kamati akiwa anasikiliza taarifa kutoka kwa Fundi Sanifu Maji Ng"itu |
Katikati Mganga Mkuu wa Wilaya Dr Japhet Simeo(kulia) Kaimu Afisa Elimu wakiwa wanaangalia jengo la Zahanati ya Namtatila |
(kushoto) Mhe Diwani ya Kata ya Mandawa na (kulia) Mhe Diwani wa kata ya Ruangwa Hassani Pendeka wakiwa wanasikiliza Mwenyekiti wa Kijiji Cha Namtatila akisoma Taarifa ya Zahanati wanayojenga |
Waheshimiwa Madiwani wa viti Maalumu wakiwa wanasikilia taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Namtatila |
Serikali ya Kijiji ikiwa katika jengo la Zahanati ya ikitoa maelezo juu ya ujenzi huo |
Jengo la Zahanati ya Namtatila lililojengwa kwa nguvu za Wananchi mpaka kufikia hapo |
Vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nambilanje vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi na kushirikiana na Halmashauri |
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nambilanje Charles Chitawala akiwa anasoma taarifa kwa wanakamati ya huduma za jamii |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chikundi Issa Rashidi akitoa maelezo ya Zahanati |
Mtendaji wa kijiji cha Chikundi akisoma taarifa ya ujenzi kwa wanakamati ya Afya, Elimu na Maji |
Jengo la Zahanati ya Chikundi lililojengwa kwa nguvu za wananchi mpaka kufikia hapo |