Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya Ziara ya kutembelea na
Kukagua Miradi ya Maendeleo ya
Halmashauri ya Wilaya ikiwa ni utekelezaji wake kila robo ya mwaka.
Kamati hiii
iligawanyika katika makundi mawili kundi A na B makundi hayo yalifanya ziara
hiyo siku ya tarehe 17/7/2017 kundi A liliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa
Halmashauri Mhe Kambona, na Kundi B liLiongozwa na Mhe Mwenyekiti wa Kamati Rashidi
Nakumbya akiambatana na wajumbe.
Kamati ilitembelea
Miradi 9 ambayo ni Mradi wa kuona shule ya sekondari Kassim Majaliwa, kata
ya Nachingwea, Kisima cha Maji,
Mkanjiro, Ujenzi wa Vyoo, Mabweni na Madarasa, Nkowe Sekondari, Kisima cha Maji
Namakuku, ,Kuona Ujenzi wa Zahanati ya Mibure, Mibure, kuona ujenzi wa Vyumba
vya Madarasa Mnacho Sekondari, Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Ndandawale, ujenzi
wa jengo la Utawala(Hawa Mchopa).
|
Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa akitoa taarifa kwa wanakamati ya Fedha, Uongozi na Mipango baada ya kutembelea shule hapo |
|
Mwenyekiti wa Kamati Rashidi Nakumbya akiangalia uiamala wa madirisha wakati wa ziara ya kamati ya Fedha |
|
Serikali ya kijiji cha Makanjiro pamoja na wajumbe wa Kamati wakiangalia mradi wa kisima kijijini hapo |
|
Mhandisi wa Maji Kabange akiwa anatoa maelezo ya mradi Makanjiro |
|
Mwenyekiti wa Kamati akiwa na wajumbe akikagua matundu ya vyoo katika shule ya sekondari Nkowe |
|
Wanakamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakiwa wanaangalia mashimo ya choo yaliyojengwa shuleni Nkowe |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri Rashidi Nakumbya akikagua mradi wa bweni ulipo katika shule ya sekondari Nkowe, Mabweni hayo yanategemewa yawe ya kidato cha tano |
|
Mkuu wa Shule ya Nkowe Maliki Ahmed akiwa anatoa maelezo ya mradi kwa waheshimiwa Madiwani |
|
Bweni la wasichana linalojengwa katika shule ya Nkowe kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano mwakani |
|
Vyumba vya darasa katika shule ya sekondari Mnacho mradi huu umekamilika na wanafunzi wameishaanza kufaidika nao |
|
Katikati)Mwenyekiti wa kamati Rashidi Nakumbiya akiwa anasikiliza taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Nandawale |
|
Jengo la Utawala katika shule ya sekondari Mnacho lilioanzwa kujengwa kwa nguvu za wananchi na Halmashauri kusaidia nguvu hizo |
|
Chumba cha Darasa kinachojengwa shule ya Sekondari Hawa Mchopa |