Thursday, 20 April 2017

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Ya Wilaya Kukagua Maendeleo ya Miradi ya Kijamii

NA Mwanakheri Ally

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Mbekenyera Rashid Nakumbiya amewataka watendaji wa serikali za vijiji kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha tofauti za vyama.

Alisema jukumu la kiongozi kuitumikia jamii iliyompigia kura ni wajibu wa kila mmoja wao, aliwakata kujenga umoja kwa kuangalia masilahi ya wananchi waliowapiga kura kwa ajili yao.

Aliyasema hayo wakati akiongea na watendaji wa serikali za vijijini wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya kamati ya fedha Uongozi na Mipango,Iliyofanyika katika maeneo ya Chikundi, Namichiga, Namilema na Ruangwa mjini.

Mwenyekiti alisema ushirikiano ni muhimu kwa pande vyama vyote vya kisiasa katika kuleta maendelea na wasifanye vyama vikawaga wao wote ni watanzania na sifa ya mwafrika ni umoja na ushikamano

Aidha aliuomba uongozi wa Halmashauri kuwafanyia utaratibu wa kupata tenki za maji katika shule ambazo zinauhaba wa maji ili waweze kuvuna maji ya kutumia wanafunzi kipindi cha ukame.

Hata hivyo Mh.Nakumbiya alitoa pongezi  kwa uongozi wa halmashauri kwa kuweza kuwasaidia wanakijiji walioonesha nguvu zao na kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata zao.

Pia alitoa pongezi za kipekee kwa viongozi wa serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha zoezi la kuanzisha miradi kama zahanati na shule zao na kuwaomba wawe na moyo huo huo kwani maendeleo katika kijiji yanaanzwa kuletwa na wahusika wa eneo

 Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango walitembelea mradi wa zahanati ya kijiji cha chikundi, ujenzi wa vyumba vya madarasa Namichiga sekondari, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namileya na barabara za lami za mjini Ruangwa.



(Kushoto)Mwenyekiti wa kamati ya fedha, uongozi na mipango Rashidi Nakumbya akiwa anaangalia mafundi wanaendelea na kazi

Mwandishi wa mkutano Bashiru Kauchumbe akitambulisha msafara aliongozana nao

Afisa Mtendaji wa kata ya Mandawa Masunga Salida akiwa anatambulisha uongozi wa kijiji waliokuja kukutana na wanakamati


Mjumbe wa serikali ya kijiji akitoa shukurani kwa mwenyekiti wa kamati kwa ujio wao katika kjijiji cha Chikundi


(kushoto)mwenyekiti wa kamati akiwa anasikiliza risala kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji(kulia)diwani wa kata ya Nandanga Shabani Kambona



Mwenyekiti wa kamati akiwa anapokea risala iliyoandaliwa na serikali ya kijiji baada ya kusomwa mbele yake na mwenyekiti wa kijiji Muhidini Tumaini

(kushoto)Afisa Mipango Thomas Luambano akiwa anamsikiliza mh. Mwenyekiti (pili) Rashidi Nakumbya akitoa maneno yake baada ya kusomewa risala

Mh. mwenyekiti akiwa anakagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Namichiga(kushoto) mwenyekiti wa bodi ya shule

Moja ya mradi uliotembelewa na wanakamati wa vyumba vya madarasa namichaga sekondari

(kulia) Mkuu wa shule Ya Namichiga akiwa ameongozana na Afisa Mipango wa Wilaya

Mwenyekiti wa Kamati akiwa anaangali ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Namichiga

Wanakamati wa fedha, uongozi na mipango wakiwa wanakagua karo la choo katika shule ya Namichiga



Mtendaji wa Kijiji cha Namichiga Vicent Mapunda akikabidhi Risala yake kwa Mwenyekiti wa Halmashauri

Mh. Diwani wa kata ya Nanganga Shabani Kambona akiwa anatoa ushauri wake kwa serikali ya kijiji

Mh. Diwani ya kata ya Chienjere Rashidi Mnunduma akiwa anaongea na serikali ya kijiji na wanakamati


Diwani wa kata ya Namichiga Mikidadi Mbute akiwa anatoa kero zake mbele ya mwenyekiti wa kamati Rashidi Nakumbya




Mhandisi wa Ujenzi ndg. Saidi Munguja akiwa anasoma risala mbele ya wanakamati

Mwenyekiti akiwa anatoa maoni yake baada ya kuona mradi wa barabara za lami za mjini ruangwa

Wanakamati wakiwa wanamsikiliza mwenyekiti na wajumbe wengine maoni yao baada ya kumaliza ziara






Wednesday, 19 April 2017

KATIBU TAWALA AWAASA WANASACCOS KUFANYA MAREJESHO YA MKOPO KWA WAKATI



NA MWANAKHERI ALLY

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ramadhani Kaswa amewataka wanavikundi wa saccos wanaokopa kutoka katika mfuko wa halmashauri kuweza kurejesha mkopo wao kwa wakati.

Alisema kuweza kufanya hivyo kwa wakati itasaidia kuwapa nafasi vikundi vingine kuweza kukopa na kubadili kiwango cha maisha kutokana na biashara watakazokuwa wanafanya.

Ameyasema hayo wakati akiongea na kikundi cha vijana saccos mjini Ruangwa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maendeleo miradi ya Halmashauri.

Aidha alisema ni vyema wahasibu wa kwenye saccos wapewe mafunzo ya kuweza kuendesha mifumo ya utunzaji fedhana vitabu vya kifedha ili waweze kuandesha saccos zao kitaalamu zaidi na itasaidia kuwa na umakini katika suala za kifedha.

Wakati huo huo Katibu Tawala alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa kufanikiwa kujenga shule mpya kwa wakati mfupi na kwa kuzingatia viwango na ubora vya kiufundi

‘’Mazingira ya shule ni mazuri kwa mwanafunzi kupatia elimu ila mafundi zidisheni kasi ili shule iweze kumalizika mapema na wanafunzi waanze kutumia majengo yao”alisema

Pia alimtaka Mhandisi wa Maji kufikiria mbinu za kuweza kuwasaidia Shule ya Sekondari Mbekenyera ili waweze kupata jenereta lao la kutumia kupampu maji katika kisima.


jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya lililopo katika hatua za ukamilishaji


Katibu Tawala Ramadhani Kaswa akiwa anakagua jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ruangwa

Katibu Tawala akiangalia ujenzi ulipofikia wa jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya Joseph Mkirikiti

Katibu Tawala(katikati)  na msafara wake wakiwa  katika shule mpya iliyopo kata ya Nachingwea

Wanafunzi wakiwa wanafanya usafi katika maeneo ya shule mpya


Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotegemewa kuhamia katika shule hiyo mpya wakiwa wanasafisha mazingira


Wanafunzi wakiwa wanapanda maua mbele ya vyumba vya madarasa

Muonekano wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule mpya inayoitwa Kassim Majaliwa

Mtambo wa kusafishi maji uliopo katika kijiji cha Mihewe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa


(Kulia)Mhandisi wa Maji wa Wilaya Lawrence Mapunda akiwa anatoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mihewe


k(kushoto katibu Tawala akiwa anaongea anaangalia eneo lililojengwa jengo kisima cha kuchujia maji(kulia)Afisa Elimu wa Wilaya Bihuria Shabani

(katikati)kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri akiwa anamuonesha(kushoto) Katibu tawala tanki lililojengwa katika kijiji cha mihewe

Tanki la kuhifadhia maji lililojengwa katika kijiji cha Mihewe lenye ujazo wa lita elf 25


Chumba cha darasa kilichopo katika shule ya Mbekenyera High school

Katibu tawala Ramadhani Kaswa akiwa anaongea na wataalamu kutoka Halmashauri na walimu katika shule ya sekondari Mbekenyera

Baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa wanasikiliz risala inayosomwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo


Mkuu wa Shule ya Mbekenyera akiwa anasoma risala mbele ya katibu tawala wa mkoa wa lindi Ramadhani Kaswa


(kushoto)Katibu tawala akiwa ameongozana na kaimu Mkurungenzi wakielekea katika vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namilema

Katibu tawala akiwa anaangalia mradi wa vyumba vya madarasa Namilema

Wakuu wa idara wakiwa na Katibu Tawala wakiangalia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mbekenyera


Wednesday, 5 April 2017

MKUU WA WILAYA RUANGWA AMEWATAKA WANANCHI WA RUANGWA KUCHUKUA TAHADHARI KWA KUJENGA NYUMBA IMARA NA BORA



(kushoto)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaangalia mkorosho ulioanguka na anasikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo
Moja ya shamba la nyumbani lililoharibika na mvua kali iliyoambatana na upepo mkali
Mkuu wa Wilaya akiwa anatoa maelekezo baada ya kuona nyumba iliyoezuliwa na bati




Moja ya nyumba iliharibiwa na mvua kali iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Chinongwe


 Mkorosho ulioangushwa na upepo mkali baada ya kunyesha mvua kubwa kijijini hapo
Mkuu wa Wilaya na timu yake wakiwa wanaangalia nyumba iliyoharibu na kumpa pole mhanga wa maafa hayo
(Katikati)Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na viongozi wa kijiji na wahanga wa mafuriko(Kushoto)Mwenyekiti wa Kijiji
Mtendaji wa Kijiji Jafari Namtima(aliyesimama) akiwa anasikiliza maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
Wanakijiji wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya akiwafariji na kuwapa mbinu za kuweza kujenga nyumba imara na bora
Na: Mwanakheri Ally

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo kujenga nyumba zenye ubora na uimara kwa kufuata taratibu za ujenzi.

Aidha, Mkuu wa Wilaya amewataka mafundi wanaojishughulisha na shughuli za ujenzi wa nyumba kutumia fani zao za kiufundi kuwashauri wateja wao viwango vya nyumba imara vinavyoitajika kabla ya kuanza ujenzi. 

Mhe. mkirikiti ameyasema hayo wakati anaongea wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Chinongwe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa, mafuriko hayo yametokea usiku wa kuamkia jana baada ya kunyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Mhe. Mkirikiti aliwapa pole waathirika wote waliokubwa na hali ya kuezuliwa nyumba zao na kuharibikiwa na mashamba ya majumbani na kuwataka kutokutaka tama na hali hiyo.

Halikadhalika, Mkuu wa Wilaya aliwataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kuchukua tahadhari mapema kwani hali ya mvua iko maeneo yote hivyo ni wajibu wa kila Mwananchi kudhibiti eneo lake.

“Nimetembea katika nyumba zote zilizokubwa na upepo huo wa jana na nikagundua tatizo hatujengi nyumba zenye ubora na uimara kuanzia sasa viongozi wa kijiji waanze kusimamia masuala ya ujenzi wa nyumba zenye kiwango kunachotakiwa”alisema

Naye Afisa Kilimo Wilaya ya Ruangwa, aliwataka Wananchi kukata mikorosho iliyokaribu na nyumba zao kwani inaweza kuleta madhara makubwa ikiendelea kuachwa, kwasababu mikorosho hiyo haijapandwa kufuata vipimo vinayoitajika.

“Shimo la mkorosho linatakiwa kuwa na futi mbili ila hiyo mikorosho iliyopandwa majumbani mingi imepandwa kiholela basi naomba ambaye mkorosho wake upo karibu na nyumba na umepandwa bila kipimo husika aukate mara moja kuepusha madhara mengine makubwa”alisema

Mafuriko hayo yameharibu nyumba za watu 55, mashamba ya majumbani  na majeruhi 1 ambaye kwasasa amelazwa Hospitali ya Ndanda na hali yake anaendelea vizuri kwasasa.




Tuesday, 21 March 2017

NAIBU WAZIRI TAMISEMI, SULEIMAN JAFO AMUAGIZA MKANDARASI ANAYEJENGA BARABARA WILAYANI RUANGWA KUZINGATIA UBORA NA THAMANI YA FEDHA ZA UJENZI


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Selemani Jaffo akiwa anatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wakati alivyotembelea shule mpya
Mh Naibu Waziri Mhe.Selemani Jafo akiwa anazungumza na Watumishi wa Ruangwa katika ukumbi wa CWT(kulia)Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ramahani Kaswa(kushoto)Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa pamoja na timu ya Usalama Wilaya wakiwa wanamsikiliza Naibu Waziri Mhe. Jafo alipokuwa anazungumza na Watumishi hao
Naibu Waziri Jafo akiwa anakagua ujenzi wa wodi mbili zinazijengwa katika hospitali ya Nadangala(kulia) Kaimu Mganga Mkuu Peter Mnyale  (kushoto) Mkuu wa Wilaya Mhe. Joseph Mkirikiti
Barabara ya Nachingwea ikiwa katika hatua za mwanzo za ujenzi wa lami

Na: Mwanakheri Ally

Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo amemtaka mkandarasi anaemiliki Kampuni ya Wanyumbani Construction anayejenga barabara za lami katika Wilaya ya Ruangwa kujenga barabara hizo katika kiwango cha ubora unaotakiwa na kwa muda uliopangwa.

Pia amemtaka Mkadarasi huyo kutumia malighafi za ujenzi zilizokusudiwa ili kuweza kufanikiwa kuwa na barabara zenye ubora uliokusidiwa na zitakazodumu muda mrefu.

Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati akikagua barabara za lami zinazojengwa na mkadarasi mwenye Kampuni ya Wanyumbani Construction wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurungezi wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Andrea Chezue kuendelea kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule mpya inayojengwa Wilayani hapo ili shule hiyo iweze kuwa na ubora.

“kwa kuangalia jinsi majengo yalivyo, inaonesha kabisa majengo haya yana ubora unaotakiwa hivyo hongereni sana na hongera zaidi kwa Mbunge wa Jimbo kwa msaada alioutoa na anaoendelea kuutoa katika ujenzi wa shule hiyo” alisema

Wakati huo huo Naibu Waziri Jaffo amewataka Watumishi wa Wilaya ya Ruangwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kufikia kasi inayotakiwa.

Alisema Naibu Waziri Watumishi wa Ruangwa wanapaswa kuwa mfano wa kuingwa katika Wilaya nyingine kwani wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili wasimuangushe Waziri Mkuu.

“Msijibweteke na msifanye kazi kwa mazoea huu ni wakati wa kubadilika na kuwa Watu wapya kama ujabadilika basi fanya kubadilika mara moja ili uweze kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli” alisema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe.Joseph Mkirikiti aliwataka Watumishi kuzingatia maagizo ya Naibu Waziri na kuyafanyia kazi kwani ni wajibu wa kila Mtumishi kufanya kazi kwa bidii na kufuata taratibu za kiutumishi. 

Aidha alimuahidi Naibu Waziri kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa na kuyatafutia ufumbuzi kama inavyotakiwa mara moja.