NA MWANAKHERI ALLY
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe, Shaibu Ndemanga aliyekuwa anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani, amewataka
waendesha Pikipiki kujifunza alama za barabarani kwa umakini na kuzitumia kama
ambavyo zinaelekezwa.
Mhe, Ndemanga aliwataka waendesha pikipiki wanavyoenda
kujifunza kuandesha chombo hiko cha moto wanapaswa kuzingatia somo la alama barabarani
kwani hii itasaidia sana kupunguza ajali
Mgeni Rasmi Mhe, Ndemaga aliyasema hayo katika siku ya
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani Kimkoa katika Wilaya
ya Ruangwa iliyofanyika kuanzia 20/11/2017 hadi 24/11/2017.
Pia Mhe, Ndemaga alisisitizi suala la kujifunza alama za
barabarani lisiwe ni la madereva tu wanaoendesha chombo hiko hata wananchi
wanapaswa kujifunza na kuzielewa alama hizo ili kufanikiwa kupunguza ajali za
barabarani.
“Lindi isiyo na jali za barabarani inawezekana na katika
kufanikisha hili ni wajibu wa kila mwananchi wa Mkoa wa Lindi kujifunza umuhimu
wa alama hizo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kwa ajali
zinazotokea”alisema Ndemanga.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Lindi aliwataka waendesha
pikipiki kwa ajili ya kujipatia riziki kuheshimu kazi hiyo na kuiona kama ni
kazi nyingine kwani ndiyo sehemu inayowaingizia kipato na kufanya kuendesha
maisha yao ya kila siku.
“Kazi mnayoifanya mnapaswa kuiheshimu kwa kiasi kikubwa
kwani haina tofauti na kazi ya mtu anaenda ofisini kila siku asubuhi, nidhamu
katika kazi yako ni chachu ya maendeleo” alisema Mhe, Ndemanga.
Vilevile Mgeni Rasmi aliwataka maafisa wa zimamoto
kupita katika kila ofisi ya serikali kuangalia kama wanamifumo na vifaa vya
kuzimia moto na ofisi itakayokosa vifaa hivyo basi mara moja iweke vifaa hivyo.
“Siyo tu maofisini hata katika taasisi zote za serikali
kama shule na zahanati inapaswa ziwe na vifaa hivyo kwani hizi ni sehemu za
mfano hata kwa jamii, wekeni vifaa vya zima moto katika maeneo hayo
muhimu”alisema Ndemanga.
Pia Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Kupunguza Umasikini na Kutunza Mazingira(APEC) Masalu Regu Rwandiko alitoa
shukurani na kuiomba serikali kuendelea kuipatia ushirikiano taasisi hiyo
inapofika katika Wilaya au Mmkoa kwa ajili ya kutoa huduma za elimu ya Usalama
barabarani, elimu ya ujasiliamali na ulinzi shirikishi kwa waendesha pikipiki.
Masalu alisema kwa elimu wanayoitoa katika maeneo mbalimbali
inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza
ajali barabarani na kwa Wilaya ya Ruangwa ajali zimepungua kwa asilimia 76 .
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph
Mkirikiti aliwataka wakazi wa Ruangwa kutumia fursa zinazojitokeza kama ya kukopeswa
pikipiki ambapo mkopeshwaji atapaswa kulipia kiasi cha fedha laki 4 za
kitanzania kwa kuanzia alafu atapewa pikipiki hiyo na ataendelea kulipia
kidogokidogo huku akiwa amekabidhiwa pikipiki yake
Aidha Mhe, Mkirikiti aliwataka vijana kuacha kukaa katika
vijiwe muda wa kazi, fursa hizo zinajitokeza wanapaswa kuzipokea kwa mikono
miwili na kuanza kufanya utekelezaji wake.
“Ikifika 2018 sitaki kuona vijiwe na nitavivunja mchana
kweupe ndani ya Wilaya yangu sitaki watu wazembe na ndiyo maana nilipambana
katika kuvunja vijiwe vyote vya (pull table) sasa ikifika huo mwaka nitamaliza
vijiwe vyote vilivyobaki”alisema Mhe, Mkirikiti.
Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha
wananchi wa Mkoa Lindi na walio nje ya Lindi kuhudhuria katika sikukuu ya
Maulidi ambayo kitaifa itafanyika katika Wilaya ya Ruangwa mkesha tarehe
30/11/2017 na sikukuu yenyewe itakuwa 1/12/2017.
“Karibuni tushereke siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad
(S.A.W) tumejiandaa kupokea wageni kila mwenye nafasi anakaribishwa kujumuika
na wanarungwa katika siku muhimu kama hiyo”alisema Mhe, Mkirikiti.
|
Ndugu Selemani Issa akiwa anakimbia na gunia kabla ya kilele cha maadhimishi kulianza michezo mbalimbali |
|
Selemani issa akiwa anapokea mkono wa hongera kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi baada ya kushinda kukimbia kwa gunia |
|
Washiriki wa kuvuta kamba wakishindana kuvuta kamba katika uwanja wa shule ya msingi Likangala |
|
Mshirikia wa mchezo wa kukimbiza kuku maarufu kama Yondo sista akiwa ameshika kuku aliyemkimbiza wakati wa shindano hilo |
|
Maandamano ya washiriki walifunzu mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani, elimu ya Ujasilimia Mali na Ulinzi na shirikishi kwa Waendesha pikipiki
|
|
Wanafunzi wa shule ya Msingi Likangara na Ruangwa wakiwa kwenye maandamano siku ya kilele cha Maadhimisho ya Wiki Nenda Kwa Usalama Barabarani |
|
Katikati)Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Shaibu Ndemanga (kulia kwake) Kamanda wa Polisi Mkoa Renata Mzinga (RPC) na (kushoto) Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakipokea maandamano ya washiriki waliopata elimu kutoka kwa( APEC) |
|
(kushoto)Mkuu wa Polisi Wilaya (katikati)Mkuu wa TAKUKURU Edings Mwakamboja wakipokea msafara wa maandamano |
|
Mgeni Rasmi Shaibu Ndemanga akisaini kitabu cha wageni katika banda la TAKUKURU alipokuwa anatembelea mabanda |
|
Afisa TAKUKURU Angela Mwakalambo akitoa maelezo kwa wageni baada ya banda lao kutembelewa |
|
Mtekenelojia wa Maabara Godfrey Eriyo akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi baada ya kutembelea baada la Afya |
|
Mgeni Rasmi akioneshwa vifaa vinavyotumika barabarani na maaskari kwa ajili ya kudhibiti mwendo kasi |
|
Mgeni Rasmi akitokea kukagua mabanda yaliyopo katika viwanja vya likangala |
|
Wacheza ngoma wa Ndege la Jeshi wakitumbuiza katika kilele cha Maadhimisho ya Kilele cha Wiki Nenda Kwa Usalama |
|
Mhe, Ndemanga akipokea zawadi ya kitamba cha suti kutoka kwa washiriki waliofunzu mafunzo yaliyotolewa na (APEC) |
|
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa (RTO) Joseph Shilinde akizungumza na wananchi katika siku ya kilele cha Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani |
|
Mgeni Rasmi akihutubia siku ya Kilele cha Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Kimkoa Katika Wilaya ya Ruangwa |
|
Mshiriki wa mafunzo yaliyotolewa na (APEC) akipokea cheti na mwanamke pekee aloiyeshirikia katika mafunzo hayo ya elimu ya usalama barabarani, elimu ya ujasilimia mali na ulinzi shirikishi kwa waendesha pikipiki. |
|
Kipa wa timu ya Bodaboda akienda kupokea zawadi ya timu yao baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mpira wa miguu |
|
Mwanafunzi wa shule ya msingi Ruangwa akienda kupokea zawadi kwa niaba ya wanakwaya wenzie baada ya kushinda nafasi ya tatu |
|
Mwananfunzi wa Shule ya Msingi ya Likangala akipokea zawadi kwa niaba ya wanakwaya wenzie baada ya kuibuka wa shindi wa kwanza |
|
Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akifunga Kilele cha Maadhimishio Ya Wiki Ya Nenda Kwa Usalama Barabarani |