WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze
kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Amekabidhi pikipiki hizo leo (Jumatano, Julai 12, 2017),
baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi
Likangara.
Baada ya kukabidhi
pikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu
kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.
Amesema vijana wanaoendesha
pikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili
kuepusha ajali.
“Ukiendesha pikipiki
lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako
na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”
Wakizungumza baada ya
kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha
pikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembelea
mradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Nandagala na
kuridhishwa maendeleo yake.
Amesema kukamilika kwa
majengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma za afya kwa mama na
mtoto. Pia itawapunguzia kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizo
katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi SACAP.
Rajab Nyange, wakati alipo tembelea na kukagua ujenzi wa Gereza la Wilaya
Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi |
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi seti ya tv na king’amuzi chake Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Lindi SACAP. Rajab Nyange, wakati akikagua ujenzi
wa Gereza la Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi |
 |
PMO_1616 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza
na wananchi wa Ruangwa Mjini katika mkutano wa hadhara aliyo uitisha,
akiwa kwenye ziara
ya kikazi |
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Liwale Zuberi Kuchauka,
katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne
Mkoani |
 |
Add captio1692
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Lindi Hamida Abdallah katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,
akiwa kwenye ziara
ya kikazin |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Lindi Manispaa,
Selemani Kaunje, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini,
akiwa kwenye ziara
ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi
 |
Add captionWaziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira Mbunge wa Nachingwea Elias Masala,
katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne
Mkoani Lindi, Julai 12, 2017 |
 |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi mipira na jezi Diwani wa Kata ya
Luchelegwa, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku nne
Mkoani Lindi, Julai 12, 2017 |
 |
Add captionWaziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi king’amuzi chake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue,wakati akikabidhi pikipiki kwa vijana, kiwa kwenye ziara ya kikazi |
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akipokea pikipiki aina ya SANLG kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Alan Lin katika mkutano wa hadhara uliyofanyika
Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikazi |
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Wauza Pikipiki na spea Taifa
Martin Mbwana katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku nne
Mkoani Lindi |
 |
Add captionWaziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi pikipiki kwa niaba ya waendesha bodaboda 49 wa
Wilaya ya Ruangwa waliokabidhiwa pikipiki Juma Selemani, katika mkutano wa
hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa kwenye ziara ya kikaz |
 |
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waendesha bodaboda waliokabidhiwa pikipiki
49 kwa mkopo, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa
kwenye ziara ya kikazi |