Thursday 29 December 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAAGIZA MAAFISA ELIMU WILAYANI RUANGWA KUPELEKA WALIMU SHULE ZA VIJIJINI

Na: Mwanakheri Ahmed

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Maafisa Elimu  Msingi na Sekondari Wilaya ya Ruangwa, kuwapeleka Walimu katika Shule za Vijijini kwa kupunguza Walimu waliopo katika Shule za Mjini Ruangwa ili kupunguza uhaba wa Walimu katika shule hizo.

Waziri Mkuu alisema kukaa na kuendelea kusubiri mpaka Serikali itoe vibali vya ajira ni kutaka kushusha kiwango cha elimu Wilayani hapo, kwani inawezekana Walimu wa Mjini wakapungunzwa kutokana uwingi wao katika shule

'' Shule hizi za Ruangwa mjini zina Walimu wapatao 30, ambao wanagawana mpaka somo moja moja Mwalimu huyo anaingia darasani kwa wiki mara moja, sasa kama shule moja inaweza kuwa na Walimu wengi hivyo kwanini wengine wasipelekwe katika shule za Vijijini'' alisema.

Ameyasema hayo alipotembelea Vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi,Chibula wakati akifanya muendelezo wa Ziara yake ya kikazi iliyoanza jana Wilayani Ruangwa

Wakati huo huo Waziri Mkuu aliwataka watendaji wa Vijiji na Kata ambavyo havina  Zahanati kuhakikisha wanaanza ujenzi wa Zahanati hizo kwa kujenga Boma na Halmashauri kutia nguvu zake katika kumaliza ujenzi huo.

kwa upande wake Waziri Mkuu   alitoa ahadi ya kuchangia bati mia moja katika vijiji ambavyo vitaanza ujenzi wa Boma hizo za Zahanati, naye Mkadarasi anayeitwa Wanyumbani alitoa ahadi ya kupeleka mifuko 100 katika kijiji cha Namilema.














Wednesday 28 December 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAONDOA HOFU WANANCHI WA RUANGWA KUHUSU KUPATIKANA KWA MAJI SAFI NA SALAMA

Na Mwanakheri Ally

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kuwa wavumilivu na wenye subira katika suala la kupatikana kwa maji safi na salama katika kila Kijiji kilichokuwa ndani ya Wilaya hiyo, kwani anafanya jitihada za kila namna ili kuweza kumaliza changamoto hiyo.

Alisema ndani ya Uongozi wake wa miaka mitano hii ya mwanzoni anataka kuhakikisha anakabiliana na kumaliza changamoto ya Umeme na Maji katika Wilaya ya Ruangwa, kwani ameshaanza mikakati ya kutafuta Wafadhili watakaowasaidia kuchimba visima virefu na kupima maji kama ni salama kwa matumizi ya Binaadamu.

Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza wa Wananchi wa kijiji cha Chimbila A, Manokwe, Ng'au, na Nadagala wakati wa Ziara yake aliyoifanya ndani ya Wilaya ya Ruangwa siku ya Tarehe 27 mwezi Desemba 2016



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya Ziara ya Kikazi katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mohammed Mtopa

Waziri Mkuu akisalimiana na Mkurugenzi wa Nachingwea{DED} Bakari Mohamedi Bakari

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT 843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu 

















Monday 26 December 2016

MKUU WA MKOA WA LINDI APIGA MARUFUKU MATUMIZI MABAYA YA CHAKULA KWENYE SHEREHE ZA KIMILA

Na: Mwanakheri Ahmed
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi wa huu wa Disemba mpaka Mei 2017.

Shughuli hizo ni pamoja na Unyago, Ndoa na Ngoma za Majini. Alisema shughuli hizo zinazofanywa na Wananchi zimekuwa zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga la njaa mkoani hapo.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi aliwataka Wananchi kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga la njaa halichagui Mkoa bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilo kwa Wananchi wote.

“Sitaki kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye Mkoa wangu umekutwa  na janga la njaa kwani hii ni aibu kubwa hivyo Watu wawe makini katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe".

Wakati huo huo Mhe. Zambi aliwataka Wananchi  wa Ruangwa wajenge vyoo imara na vya matumizi ya muda mrefu, ili kuweza kujiepusha na maradhi ya Kipindupindu kama ambavyo yanaikabili Wilaya ya Kilwa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa aliwataka Watendaji wa vijiji kusimamia zoezi la kila Mwananchi wa eneo lake anakuwa na choo imara na Mtu atakaekaidi kufanya ujenzi wa choo cha nyumbani kwake basi achukuliwe hatua za kisheria.

Vilevile aliwasa Wananchi kuwa na matumizi mazuri ya pesa wanazoipata za kuuza korosho au fidia wanazolipwa na kuacha matumizi mabovu ya pesa hizo kama ambaVyo inafanywa na baadhi ya Watu.

Mhe. Zambi aliwakata Wananchi kutumia pesa wanazozipata katika kutengeneza maisha yao kama katika kusomesha Vijana wao na kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia zao.


Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anaongea na wanakijiji wa Kijiji cha Makanjiro











Mkuu Wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wananchi wa kijiji cha Mandawa





Wednesday 21 December 2016

NAIBU WAZIRI POSSI AWAHIMIZA WANANCHI WA RUANGWA KUSAIDIA WATU WENYE ULEMAVU

Na: Mwanakheri Ahmed 
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu; Watu wenye ulemavu Dkt. Abdallah Possi ameitaka Halmashauri ya Mji wa Ruangwa kusaidia kituo cha Walemavu cha Nandaga kwa kupeleka matunzo yote yanayostahili kwa Watu wanaoishi katika kituo hicho.

 Aidha, Dkt Possi alieleza swala la kusaidia Walemavu hao si suala la Watu fulani kama vile Watu wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii au Madaktari, bali ni jukumu la kila Mtu. Dkt. Possi aliyaongea hayo alipotembelea kituo cha Walemavu cha Nandaga