Thursday 29 December 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAAGIZA MAAFISA ELIMU WILAYANI RUANGWA KUPELEKA WALIMU SHULE ZA VIJIJINI

Na: Mwanakheri Ahmed

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Maafisa Elimu  Msingi na Sekondari Wilaya ya Ruangwa, kuwapeleka Walimu katika Shule za Vijijini kwa kupunguza Walimu waliopo katika Shule za Mjini Ruangwa ili kupunguza uhaba wa Walimu katika shule hizo.

Waziri Mkuu alisema kukaa na kuendelea kusubiri mpaka Serikali itoe vibali vya ajira ni kutaka kushusha kiwango cha elimu Wilayani hapo, kwani inawezekana Walimu wa Mjini wakapungunzwa kutokana uwingi wao katika shule

'' Shule hizi za Ruangwa mjini zina Walimu wapatao 30, ambao wanagawana mpaka somo moja moja Mwalimu huyo anaingia darasani kwa wiki mara moja, sasa kama shule moja inaweza kuwa na Walimu wengi hivyo kwanini wengine wasipelekwe katika shule za Vijijini'' alisema.

Ameyasema hayo alipotembelea Vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi,Chibula wakati akifanya muendelezo wa Ziara yake ya kikazi iliyoanza jana Wilayani Ruangwa

Wakati huo huo Waziri Mkuu aliwataka watendaji wa Vijiji na Kata ambavyo havina  Zahanati kuhakikisha wanaanza ujenzi wa Zahanati hizo kwa kujenga Boma na Halmashauri kutia nguvu zake katika kumaliza ujenzi huo.

kwa upande wake Waziri Mkuu   alitoa ahadi ya kuchangia bati mia moja katika vijiji ambavyo vitaanza ujenzi wa Boma hizo za Zahanati, naye Mkadarasi anayeitwa Wanyumbani alitoa ahadi ya kupeleka mifuko 100 katika kijiji cha Namilema.