Thursday 20 April 2017

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Ya Wilaya Kukagua Maendeleo ya Miradi ya Kijamii

NA Mwanakheri Ally

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa kata ya Mbekenyera Rashid Nakumbiya amewataka watendaji wa serikali za vijiji kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha tofauti za vyama.

Alisema jukumu la kiongozi kuitumikia jamii iliyompigia kura ni wajibu wa kila mmoja wao, aliwakata kujenga umoja kwa kuangalia masilahi ya wananchi waliowapiga kura kwa ajili yao.

Aliyasema hayo wakati akiongea na watendaji wa serikali za vijijini wakati wa ziara ya kutembelea Miradi ya kamati ya fedha Uongozi na Mipango,Iliyofanyika katika maeneo ya Chikundi, Namichiga, Namilema na Ruangwa mjini.

Mwenyekiti alisema ushirikiano ni muhimu kwa pande vyama vyote vya kisiasa katika kuleta maendelea na wasifanye vyama vikawaga wao wote ni watanzania na sifa ya mwafrika ni umoja na ushikamano

Aidha aliuomba uongozi wa Halmashauri kuwafanyia utaratibu wa kupata tenki za maji katika shule ambazo zinauhaba wa maji ili waweze kuvuna maji ya kutumia wanafunzi kipindi cha ukame.

Hata hivyo Mh.Nakumbiya alitoa pongezi  kwa uongozi wa halmashauri kwa kuweza kuwasaidia wanakijiji walioonesha nguvu zao na kuanzisha miradi ya maendeleo katika kata zao.

Pia alitoa pongezi za kipekee kwa viongozi wa serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kwa kuweza kufanikisha zoezi la kuanzisha miradi kama zahanati na shule zao na kuwaomba wawe na moyo huo huo kwani maendeleo katika kijiji yanaanzwa kuletwa na wahusika wa eneo

 Kamati ya Fedha na Uongozi na Mipango walitembelea mradi wa zahanati ya kijiji cha chikundi, ujenzi wa vyumba vya madarasa Namichiga sekondari, ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namileya na barabara za lami za mjini Ruangwa.



(Kushoto)Mwenyekiti wa kamati ya fedha, uongozi na mipango Rashidi Nakumbya akiwa anaangalia mafundi wanaendelea na kazi

Mwandishi wa mkutano Bashiru Kauchumbe akitambulisha msafara aliongozana nao

Afisa Mtendaji wa kata ya Mandawa Masunga Salida akiwa anatambulisha uongozi wa kijiji waliokuja kukutana na wanakamati


Mjumbe wa serikali ya kijiji akitoa shukurani kwa mwenyekiti wa kamati kwa ujio wao katika kjijiji cha Chikundi


(kushoto)mwenyekiti wa kamati akiwa anasikiliza risala kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji(kulia)diwani wa kata ya Nandanga Shabani Kambona



Mwenyekiti wa kamati akiwa anapokea risala iliyoandaliwa na serikali ya kijiji baada ya kusomwa mbele yake na mwenyekiti wa kijiji Muhidini Tumaini

(kushoto)Afisa Mipango Thomas Luambano akiwa anamsikiliza mh. Mwenyekiti (pili) Rashidi Nakumbya akitoa maneno yake baada ya kusomewa risala

Mh. mwenyekiti akiwa anakagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Namichiga(kushoto) mwenyekiti wa bodi ya shule

Moja ya mradi uliotembelewa na wanakamati wa vyumba vya madarasa namichaga sekondari

(kulia) Mkuu wa shule Ya Namichiga akiwa ameongozana na Afisa Mipango wa Wilaya

Mwenyekiti wa Kamati akiwa anaangali ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari Namichiga

Wanakamati wa fedha, uongozi na mipango wakiwa wanakagua karo la choo katika shule ya Namichiga



Mtendaji wa Kijiji cha Namichiga Vicent Mapunda akikabidhi Risala yake kwa Mwenyekiti wa Halmashauri

Mh. Diwani wa kata ya Nanganga Shabani Kambona akiwa anatoa ushauri wake kwa serikali ya kijiji

Mh. Diwani ya kata ya Chienjere Rashidi Mnunduma akiwa anaongea na serikali ya kijiji na wanakamati


Diwani wa kata ya Namichiga Mikidadi Mbute akiwa anatoa kero zake mbele ya mwenyekiti wa kamati Rashidi Nakumbya




Mhandisi wa Ujenzi ndg. Saidi Munguja akiwa anasoma risala mbele ya wanakamati

Mwenyekiti akiwa anatoa maoni yake baada ya kuona mradi wa barabara za lami za mjini ruangwa

Wanakamati wakiwa wanamsikiliza mwenyekiti na wajumbe wengine maoni yao baada ya kumaliza ziara






Wednesday 19 April 2017

KATIBU TAWALA AWAASA WANASACCOS KUFANYA MAREJESHO YA MKOPO KWA WAKATI



NA MWANAKHERI ALLY

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ramadhani Kaswa amewataka wanavikundi wa saccos wanaokopa kutoka katika mfuko wa halmashauri kuweza kurejesha mkopo wao kwa wakati.

Alisema kuweza kufanya hivyo kwa wakati itasaidia kuwapa nafasi vikundi vingine kuweza kukopa na kubadili kiwango cha maisha kutokana na biashara watakazokuwa wanafanya.

Ameyasema hayo wakati akiongea na kikundi cha vijana saccos mjini Ruangwa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maendeleo miradi ya Halmashauri.

Aidha alisema ni vyema wahasibu wa kwenye saccos wapewe mafunzo ya kuweza kuendesha mifumo ya utunzaji fedhana vitabu vya kifedha ili waweze kuandesha saccos zao kitaalamu zaidi na itasaidia kuwa na umakini katika suala za kifedha.

Wakati huo huo Katibu Tawala alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa kufanikiwa kujenga shule mpya kwa wakati mfupi na kwa kuzingatia viwango na ubora vya kiufundi

‘’Mazingira ya shule ni mazuri kwa mwanafunzi kupatia elimu ila mafundi zidisheni kasi ili shule iweze kumalizika mapema na wanafunzi waanze kutumia majengo yao”alisema

Pia alimtaka Mhandisi wa Maji kufikiria mbinu za kuweza kuwasaidia Shule ya Sekondari Mbekenyera ili waweze kupata jenereta lao la kutumia kupampu maji katika kisima.


jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya lililopo katika hatua za ukamilishaji


Katibu Tawala Ramadhani Kaswa akiwa anakagua jengo jipya la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Ruangwa

Katibu Tawala akiangalia ujenzi ulipofikia wa jengo la ofisi ya Mkuu wa wilaya Joseph Mkirikiti

Katibu Tawala(katikati)  na msafara wake wakiwa  katika shule mpya iliyopo kata ya Nachingwea

Wanafunzi wakiwa wanafanya usafi katika maeneo ya shule mpya


Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotegemewa kuhamia katika shule hiyo mpya wakiwa wanasafisha mazingira


Wanafunzi wakiwa wanapanda maua mbele ya vyumba vya madarasa

Muonekano wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule mpya inayoitwa Kassim Majaliwa

Mtambo wa kusafishi maji uliopo katika kijiji cha Mihewe kilichopo katika Wilaya ya Ruangwa


(Kulia)Mhandisi wa Maji wa Wilaya Lawrence Mapunda akiwa anatoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi alipotembelea mradi wa maji katika kijiji cha Mihewe


k(kushoto katibu Tawala akiwa anaongea anaangalia eneo lililojengwa jengo kisima cha kuchujia maji(kulia)Afisa Elimu wa Wilaya Bihuria Shabani

(katikati)kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri akiwa anamuonesha(kushoto) Katibu tawala tanki lililojengwa katika kijiji cha mihewe

Tanki la kuhifadhia maji lililojengwa katika kijiji cha Mihewe lenye ujazo wa lita elf 25


Chumba cha darasa kilichopo katika shule ya Mbekenyera High school

Katibu tawala Ramadhani Kaswa akiwa anaongea na wataalamu kutoka Halmashauri na walimu katika shule ya sekondari Mbekenyera

Baadhi ya wakuu wa Idara mbalimbali wakiwa wanasikiliz risala inayosomwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo


Mkuu wa Shule ya Mbekenyera akiwa anasoma risala mbele ya katibu tawala wa mkoa wa lindi Ramadhani Kaswa


(kushoto)Katibu tawala akiwa ameongozana na kaimu Mkurungenzi wakielekea katika vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Namilema

Katibu tawala akiwa anaangalia mradi wa vyumba vya madarasa Namilema

Wakuu wa idara wakiwa na Katibu Tawala wakiangalia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Mbekenyera