Friday 14 July 2017

Waziri Mkuu Akabidhi Magari Mawili Ya Kubeba Wagonjwa Katika Hospitali ya Ruangwa

Na Mwandishi wetu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa.

Amesema kati ya magari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pili litapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12, 2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.

Amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.

 “Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

Waziri Mkuu amesema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa  wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa.

 Kabla ya kukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya  akina  mama na ya  watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwamba ameridhishwa na hali ya utoaji huduma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Mheshimiwa Rashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali mtoto Nasib Robert,(kushoto) ni mama wa mtoto Veronica Chilala,wakati alipo tembelea wodi ya watoto katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wakati alipo tembelea hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua vifaa ndani ya gari la kubebea wagonjwa baada ya kukabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua gari ya kubebea wagonjwa wakati alipokabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya  Wilaya Ruangwa, akiwa kwenye ziara ya kikazi
Gari la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa na Waziri Mkuu katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa wakati wa Ziara yake ya kikazi

Waziri Mkuu akisalimiana na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya  dr Bogia

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akitoa neno la shukurani kwa Waziri Mkuu baada ya kukabidhiwa gari za kubebea wagonjwa mbili.