Friday 14 July 2017

Majaliwa:Hakuna Kijiji Tanzania Kitakachoachwa Bila Ya Umeme



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

Amesema Serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Julai 11, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa aliyasema hayo katika mikutano aliyoifanya kwenye vijiji vya Chiapi, Nandanga, Mbecha na Luchelegwa, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya ya Ruangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Pia Waziri Mkuu amesema  mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba  lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.


Waziri Mkuu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti alipowasili katika kijiji cha Likwachu


Mkuu wa Wilaya Joseph Mkirikiti akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi ili aendelee na itifaki nyingine

Wakazi wa Kijiji cha Likwachu wakiwa wanamsikiliza Waziri Mkuu alipokuwa anazungumza


Waziri Mkuu akizungumza nawakazi wa kijiji cha Likwachu alipofanya ziara yake katika kijiji cha Likwachu

Waziri Mkuu akisalimiana na wanakijiji cha Litama alipofika katika kijiji hiko

Waziri Mkuu akisalimia wananchi alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Ruangwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mradi wa daraja la Likuledi, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi
Waziri Mkuu akifungua Hospitali ya Watu wenye mahitaji maalumu Nandanga alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo






Mbunge wa Liwale Zuberi akiwa anasalimia wakazi wa kijiji cha Likwachu alipopewa nafasi hiyo na Mkuu wa Mkoa



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Andrea Chezue akiwa anaelezea jinsi watakavyokarabati Zahanati la Likwachu

Wananchi wakiwa wanamsubiri Waziri Mkuu katika kijiji cha Litama

Mbunge wa Ndanda Mwmabe akitoa shukurani kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapelekea Mradi mkubwa wa kujenga daraja linalounganisha Wilaya ya Ndanda na Ruangwa katika kijiji cha Nandanga kilichopo Wilaya ya Ruangwa
 
Mhandisi wa Ujenzi Mashaka Nalupi akipokea maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu katika kijiji cha Likwachu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anasalimiana na mafundii,wanalojenga daraja linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi,kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 201