NA MWANDISHI WETU
Waziri Mkuu, Kassim
Majaaliwa amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa
Kilimo kutoka mikoa inayolima korosho, washirikiane kupata takwimu mpya za
wakulima wa zao hilo.
Ametoa agizo hilo leo
mchana jumapili, Desemba 31,2017) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya
Upandaji wa Mikorosho Bora na Mipya milioni 10 msimu wa 2017/ 2018 mjini
Ruangwa, mkoani Lindi.
“Maafisa Kilimo na
Maafisa Ushirika mkisimamiwa na Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, mshirikiane na
kusimamia kwa umakini upatikanaji wa twakimu za wakulima na maeneo yanayolimwa,
haiwezekani kila mwaka takwimu ziwe ni zilezile tu” alisema Waziri Mkuu
“Afisa kilimo wa Wilaya
lazima ujue una wakulima wangapi, je hao wakulima wako, kila mmoja analima
ekari ngapi? Na katika ekari hizo ana miche mingapi, na ana mahitaji ya
pembejeo kiasi gani “alisema.
Pia nilikwisha waagiza
maafisa ushirika na viongoi wa vyama vya msingi(AMCOS) mpaka chama kikuu cha
ushirika, kuwa kila mmoja anapaswa atambue ana wanachama wangapi katika chama
chake. Hili litawezekana pia kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au
Mwenyekiti wa kijiji, kwasababu wao wanaidadi kamili za watu wanaowaongoza”alisema.
“Ninaimani tukifanya
hili tutamaliza tatizo la takwimu na Serikali itakuwa nauwezo mkubwa wa
kuwahudumia wakulima wake, tutaweza kuweka bajeti ya kutosha kuhudumia mahitaji
yao”alisisitiza
Waziri Mkuu alipanda
mche mpya wa korosho ili kuanzisha zoezi la upandaji miche hiyo na kisha kugawa
miche kwa wakulima 10 kutoka Likunja, Kitandi, Kilimahewa na Nachingwea ambao
waliwakilisha wenzao
Mapema kabla
ya kuzungumza na wananchi Waziri Mkuu alikagua vitalu vya miche ya mikorosho
vilivyopandwa na Halmashauri ya Ruangwa na kuelezwa kuwa miche hiyo ipo ya aina
mbili ambapo aina ya kwanza ni ile iliyotokana na mbegu za pili iliyotokana na
vikonyo
![]() |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia maji mche mpya wa korosho, baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi |
![]() |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mche mpya wa korosho ,mara baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa mkoani lindi |
![]() |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wakati wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018 |
![]() |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania Hassani Jarufu wakati akikagua kitalu cha miche mipya ya korosho |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua miche ya mikorosho alipotembelea vitalu vya miche hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 msimu 2017/2018 |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue |
Miche ya Mikorosho Mipya na bora iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa |