Thursday 25 May 2017

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour Awaasa Wananchi wa Ruangwa Katika Kukuza Uchumi wa Viwanda



Wakulima Wilayani Ruangwa, wameaswa kushiriki utekelezaji wa dhamira ya kufikia na kufanikiwa mpango wa serikali wa kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda.

Wito huu alitolewa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Amour Hamad Amour, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nandalaga alipotembelea shamba na kiwanda cha kukamua mafuta ya zao la Alizeti.

Aliwataka wananchi kuongeza bidii katika sekta ya kilimo ambayo itapelekea kuwa na viwanda kwa wingi kwasababu kilimo na viwanda ni vitu viwili vinavyotegemeana. Wakulima  wanao wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kuifanya nchi kufikia uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.

Alibainisha kwamba idadi kubwa ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa ni wakulima, hivyo wanayo nafasi ya kushiriki mpango huo wa serikali kupitia kazi wanazofanya. Amour, alifananua kuwa ili wakulima waweze kufanikisha azima hiyo wanapaswa kubadilisha mtazamo na fikra kutoka kwenye kilimo cha kawaida na kwenda kwenye kile cha viwanda.

"Badala ya kuuza mazao ghafi, wakulima wanapaswa kufikiria kuuza yaliyotengenezwa viwandani. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmeongeza thamani mazao mnayozalisha na mtakuza uchumi wenu wenyewe" alisema Amour.

Aidha alisema kama Tanzania ikifanikiwa kuwa nchi ya viwanda, basi kutakuwa na faida nyingi kama kuongeza ajira ya mtu mmoja mmoja, kukuza uchumi wa taifa na kubadilisha mfumo wa maisha kutoka katika hali duni mpaka kuwa na hali nzuri.

"Lengo ni  kuona hadi kufika mwaka 2025, wananchi wameondoka kwenye lindi la umasikini na kufikia uchumi wa kati. Ila kufanikiwa katika suala la viwanda inabidi wananchi wakazane kufanya kilimo kwa wingi na wabadili mbinu za kilimo" alisema Amour.

Vile vile alimtaka Mkuu wa Wilaya kuweka mkakati wa kuzuia matumizi mabaya ya chandarua kwasababu wananachi wanabadili matumizi ya vyandarua. Badala ya kufunga kwenye vitanda vyao wanafunga kwenye bustani zao. Hivyo aliwataka wananchi kuwa na fikira za kubadilika na si kuishi kwa mazoea.

Wakati huo huo, Mkimbiza Mwenge , Fredirick Joseph Ndahani, alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa mapokezi mazuri waliyoyapata  na kusisitiza Halmashauri kuongoza jitihada za kusaidia vikundi vya wajasiriamali na hasa vijana.


Mkuu wa Wilaya Lindi  Shaibu Issa Ndemanga akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Rukia Muwango

Mkimbiza Mwenge Uhuru Bahati Mwaniguta Lugodisha akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru Kitaifa

Mkimbiza Mwenge  Bahati Lugodisha akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Talawa Twaha Mpembenwe

(katikati)Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour(kushoto kwake)Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue na (kulia kwake)Kaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango (kushoto kwake) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe

Wakuu wa Idara wakiwa wanausubiri Mwenge wa Uhuru  baada ya kuwasili katika uwanja wa shule ya msingi Nandagala

Katikati)Kaimu Mkuu wa Idara ya Tehama Jitetete Mbonde (kushoto kwake) Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Bihuria Shabani na( kulia) Mkuu wa idara ya Utawala Festo j Mwangalika

Wananchi wakiwa wanasubiri Mwenge wa Uhuru ufike katika kijiji cha Ipingo

Mkimbiza Mwenge Fedrick Joseph Mdahani akiwa anatoa maelezo katika banda la kuku Ipingo


Mkimbiza Mwenge Ndahani akiwa anatoa maelekezo ya vifungashio vya sabuni kwa wakikundi ipigo

Katikati Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrea Chezue (kulia) Mkimbiza mwenge Bahati Lugodisha na (kushoto) Katibu Tawala Twaha Mpembenwe

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Hawa Mchopa wakiwa wanasikiliza burudani kutoka kwa mwanafuzni mwenzao

Wananchi wakiwa katika uwanja wakamsikiliza Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiongea


Mwenge wa uhuru Kitaifa ukiwa katika Shule ya Hawa Mchopa

Mkimbiza Mwenge Bahati Mwaniguta Lugodisha akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Nangumbu


Kikundi cha wanawake wakiwa na mafuta waliokamua ya alizeti


Bwana shamba wa Nandagala Amanzi Mbeo akiwa anatoa maelezo ya shamba la alizeti

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa anazungumza na wanakijiji cha Nandagala baada ya kutembelea shamba na kiwanda cha kukamua alizeti

Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiwa anaweka zege katika ndoo kwenye Zahanati ya Nandagala kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili

Wakimbiza Mwenge wakiwa wanaagalia jinsi ya kutega mbu

Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anagawa chandarua kwa mwanakijiji wa Nandagala


Mkimbiza Mwenge Kitaifa Amour akiwa anaangalia jinsi amplifaya inavyofanya kazi iliyotengenezwa na kikundi cha Mkuti


Mkimbiza Mwenge Kitaifa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za lami mjini Ruangwa

Mhandisi wa Ujenzi Mashaka Nalupi akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara za lami mjini Ruangwa



Kaimu Mkuu wa Wilaya Rukia Muwango akiwa anatoa maelekezo kabla ya kwenda Nachingwea kukabidhi

Mkimbiza Mwenge Fredirick Joseph Ndahani akitoa neno la shukurani baada ya kuwasili Ruangwa mjini

(katikati)Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour akiwa ameishakabidhiwa Wilaya ya Nachingwea(kulia)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Bakari Mohamed Bakari

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akimkabidhi Mwenge wa Uhuru  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Andrea Chezue akiwa anatoka kukabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Nachingwea