Na Mwanakheri Ally
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji Elias Nkane,
amewataka wakuu wa shule wanaopewa pesa
kwa ajili ya kuongeza vyumba vya madarasa, chumba cha kukaa walimu na vyoo
wazitumie pesa hizo kwa mahitaji yaliyokusudiwa.
Mh, Nkane Alisema pesa za lipa kulingana na matokeo (P4R)
zinazopelekwa katika mashule ni nyingi hivyo zisiwatie tamaa wakuu wa shule na
kuanza kuzitumia katika mipango isiyokusudiwa kwani kufanya hivyo ni kosa
kisheria.
Mwenyekiti alisema hayo wakati wa ziara ya kamati ya
huduma za jamii, zilipotembelea katika miradi katika kijiji cha Nachiungo,
Mnacho, Chimbila A na Michenga, kamati ilitembelea shule ya msingi Nachiungo,
shule ya sekondari Mnacho, mradi wa maji Michenga na kuangalia eneo la ujenzi
wa zahanati katika kijiji cha Chimbila A.
Aidha Mwenyekiti aliutaka uongozi wa kijiji cha Chimbila A, kuhakikisha eneo lilotengwa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati alivamiwi na
wanakijiji kwa ajili ya shughuli za kilimo na makazi,
``Jitahidi mpaka mwezi wa 8 mwaka huu zahanati iwe
imesimama hata mkiomba nguvu kutoka Halmashauri itakuwa ni rahisi kusaidiwa,
serikali ya kijiji mjitahidi katika kukusanya michango`` alisema.
Naye Diwani wa Mbwemkuru aliwasisitiza viongozi vya serikali
ya kijiji cha Chimbila kukusanya michango ya ujenzi wa zahanati bila kuangalia
wala kupendelea ili kuweza kifikia lengo walilojiwekea.
Katika kuonesha madiwani wako karibu na wananchi wao
madiwani wawili walichangia fedha za ujenzi wa zahanati hiyo bila kuangalia kuwa siyo
kata yao, vilevile mganga mkuu wa Wilaya naye alichangia fedha kwa ajili ya
ujenzi wa zahanati hiyo.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya dr Japhet Simeo aliupongeza
uongozi wa shule ya sekondari Mnacho kwa juhudi walizozionesha za kuanza ujenzi
wa vyumba ya kukaa walimu ambavyo havikuwa katika mpango wa (P4R)kwani ni
ubunifu mzuri ulioufanywa na uongozi wa shule hiyo.
Pia aliushauri uongozi wa kijiji cha Chambila A, kuwa
na ushirikiano na jamii inayowazunguka ili kuweza kufanikisha jambo hilo, kwasababu hao ndiyo watu watakaoweza
kusaidia kuendeleza au kushia njiani kwa ujenzi wa zahanati hiyo
 |
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nachiungo Gabrier Issa Mshiro akiwa anasoma taarifa ya mradi mbele ya wanakamati wa huduma za jamii |
 |
vyumba vya madarasa vitatu vinavyojegwa katika shule ya msingi Nachiungo |
 |
Wanakamati wakiwa wanasikiliza taarifa iliyokuwa inayosomwa na mwalimu mkuu |
 |
(Katikati)Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji akiwa anasikiliza maoni ya wajumbe(kushoto)Mganga mkuu wa Wilaya |
 |
Mganga mkuu wa Wilaya Dr Japhet Simeo akiwa anaongea baada ya kusomewa taarifa |
 |
Mwenyekiti wa kijiji cha Narung`ombe Hamisi Omari akiwa anajibu swali aliloulizwa na Mwenyekiti wa kamati |
 |
(kushoto)Diwani wa viti maalumu Paulina muya akiwa anatoa maoni yake kwa wanakamati ya ujenzi wa shule ya msingi Nachiungo |
 |
Mkuu wa shule ya sekondari Mnacho akiwa anasoma taarifa yake mbele ya kamati ya huduma za jamii ilivyofanya ziara yake katika shule hiyo |
 |
Waheshimiwa madiwani wakiwa wanasikiliza taarifa ya ujenzi kutoka kwa mkuu wa shule |
 |
Mwenyekiti wa Kamati akiwa anasikiliza taarifa kutoka kwa mkuu wa shule wa Mnacho |
 |
Ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika shule ya Mnacho |
 |
Vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa pesa za (P4R) katika shule ya sekondari Mnacho |
 |
Wajumbe wa kamati wakiwa wanasikiliza taarifa |
 |
Mwenyekiti wa Kamati Elias Nkane akiwa anaongea baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya darasa |
 |
Mh. Nkane akiwa anaonesha wanakamati uimara wa tofali zilizojengewa choo katika shule ya sekondari mnacho |
 |
Wajumbe wa kamati wakiwa wanaangalia shimo la choo |
 |
(kushoto)Diwani wa kata ya Mbwemkuru Selemani Likuche akiwa anatoa maoni yake baada ya kuona ujenzi katika shule ya Mnacho |
 |
(katikati)Diwani wa kata ya Matambalale akiwa anatoa maoni yake baada ya kuona mradi(kulia) Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya na(kushoto) Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo |
 |
Mh, Diwani wa kata ya Mandawa Abdallah Nachingi akiwa anatoa ushauri wake kwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mnacho baada ya kuona hali ya ujenzi |
 |
Mh, Nkane akiwa anahamasisha wanakijiji wa Chimbila A, kuanza ujenzi wa Zahanati katika kijiji hiko |
 |
Serikali ya kijiji ya Chimbila A, na kamati ya huduma za jamii wakiwa wanamsikiza Mwenyekiti wa Kamati |
 |
Mh, Diwani wa Viti maalumu akiwa anatoa ushauri kwa serikali ya kijiji cha Chimbila A, kuhusu ujenzi wa Zahanati |
 |
Waheshimiwa madiwani wakiwa wanaangalia mradi wa maji katika kijiji cha Michenga |
 |
Wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maji wakiwa katika kijiji cha michenga wakiangalia mradi wa maji |
 |
Kaimu Mtendaji wa kijiji bi, Zaituni Natunga akiwa anasoma taarifa mbele ya wanakamati |
 |
Mwenyekiti akitoa maoni yake baada ya kuuona mradi wa maji na baada ya kusomewa taarifa |