Monday 1 May 2017

RC- ZAMBI AWATAKA WAKURUGENZI WA WILAYA ZA MKOA WA LINDI KUHAKIKISHA HOSPITALI HAZIKOSI WAUGUZI LICHA YA CHANGAMOTO YA UHABA WA WATUMISHI KWENYE SEKTA YA AFYA



Na Mwanakheri Ally

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfery Zambi amewataka wakurungenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Liwale, Kilwa na Nachingwea kuhakikisha Zahanati zilizopo ndani ya Wilaya hizo hazifungwi kutokana na upungufu utakaojitokeza wa watumishi waliokutwa na tatizo la vyeti feki.

Mh Mkuu wa Mkoa Zambi alisema wakurungenzi watendaji wa Halmashauri hizo wajitahidi kuhamisha wauuguzi watakaokuwa wengi  katika eneo moja wapelekwe katika zile zahanati ambazo zinautaji zaidi ya watumishi.

Aliyasema hayo wakati akihutubia katika sherehe za siku ya wafanyakazi dunia iliyofanyika katika Wilaya ya Ruangwa kwenye uwanja wa shule ya msingi likangara ambapo inafanyika kwa mwaka mara moja mwezi wa 5 tarehe 1.

Kauli hiyo imetokana na agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli la watumishi waliokutwa na vyeti feki waache kazi mara moja laasivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha alisema Serikali imejipanga kupambana na watumishi wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea kwani uongozi wa awamu hii haupo katika kulea watu wasiotaka kubadilika.

Pia aliwataka walimu wa shule za msingi na sekondari waache kunung’unika kuhusu  ya maslahi yao kwani manunguniko yanaweza wasababisha washindwe kufanyakazi ipasavyo na kusababisha matokea mabaya ya mitihani ya taifa.
“Serikali inajitahidi kutatua matatizo yanaowakabili hivyo ni wakati wa walimu huko mashuleni kufanya kazi kwa bidii na kubadilisha matokea ya darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka huu”alisema.

Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali katika shughuli za mwenge ambazo katika mkoa wa Lindi mwenge utapokelewa tarehe 21 na wilaya ya Ruangwa tarehe 23 na 24 mwezi wa tano.

Wakati huo huo Mratibu wa Tucta mkoa wa Lindi Fatma .s. Chaunga aliomba serikali kuweza kupunguza kiwango cha kodi kwa wafanyakazi ipungue kutokana asilimia 9 mpaka 7 kwani bado hiyo asilimia 9 nikubwa kutokana na mshahara wa watumishi wengi.

Pia aliomba serikali  kuangalia uchumi wa viwanda uweze kuzingatia ajira kwa wazawa kwanza kwasababu kunawatu wengi wanaelimu ya kutosha kufanya kazi katika viwanda hivyo.

Hata hivyo Bi Fatma aliipongeza serikali kwa juhudi zake za elimu bure, hali hii imesababisha wazazi wengi kupata nafasi ya kupeleka watoto wao shule kwasababu hamna gharama ya ada wanayokutanayo na imesaidia kupunguza watoto wazururaji huko vijijini na mjini.


Watumishi wakiwa katika maandamano kabla ya kuanza kwa sherehe

Wafanyakazi wa Nida wakiwa katika maandamano

wafanyakazi wa Tanesco wakiwa katika maandamano wakiwa na bango linalisema Lipa deni lako ili kutimiza azma ya serikali ya uchumi wa viwanda



Chama cha wafanyakazi Talgwu Halmashauri ya Lindi wakiwa na bango linalosema uchumi wa viwanda uzingatie haki na heshima ya wafanyakazi



Watumishi wakiwa wanasubiri kuingia katika uwanja wa shule ya likangara ili mgeni rasmi apokee maandamano hayo

(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akiwa anaangalia kikundi cha ngoma cha dege la jeshi wakitumbuiza


Kikundi cha dege ya Jeshi cha Ruangwa kikiwa kinatumbuiza mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa

(kushoto) Mratibu wa Tucta Mkoaakiwa anaangalia ka umakini ngoma inayotumbuizwa(kulia kwake) Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea



Wananchi wakiwa wamejitokeza katika uwanja wa Likangara kuangalia sherehe za Mei Mosi

Watumishi waliohudhuria katika sherehe ya mei mosi wakiwa wanaangalia burudani mbalimbali

Wananchi wakubwa kwa watoto wakiwa katika uwanja wa likangara wakiangalia sherehe zinavyoendelea

Wafanyakazi waliojitokeza kucheza ngoma pamoja na dege la jeshi

Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa katika banda la Nmb akipokea maelezo kutoka wafanyakazi wa bank hiyo

(kushoto)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa Rashid Nakumbya akiwa na Msahiki Meya wa Lindi


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nachingwea Bakari M bakari

Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa katika banda la Nida akisikiliza maelezo kwa Afisa Msajili wa Nida Khalaf Mwalim

Katikati)Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa akiwa na Mkurungenzi wa ya Liwale

Mkurugenzi Mtendaji Andrea Chezue akiwa anamkabidhi mteja kitambulisho chake baada ya kutembelea banda la nida


Kikundi cha ngoma cha wanafunzi wakiwa wanatumbuiza


Mratibu wa Tucta Mkoa wa Lindi Fatma S Chaunga akiwa anasoma risala mbele ya mgeni rasmi

Mh, Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anahutubia wafanyakazi katika uwanja wa likangara

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa akiwa anatoa ahadi yake ya kuwasaidia kikundi cha dege ya jeshi nguo rasmi za kuvaa sehemu kama hizo


Mfanyakazi hodari akiwa anapokea pesa na cheti kutoka kwa mkuu wa mkoa

Bwanashamba wa rondo akienda kupokea zawadi yake kwa kuwa mtumishi hodari


Mwalimu wa shule ya Sekondari Mnacho Benjamin akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi

Afisa Uchaguzi wa Wilaya Yusuph Chilumba akipokea cheti chake na kiasi cha pesa laki 3

Mfanyakazi wa Shirika la Umeme (Tanesco) Happiness Mpaza fundi akipokea zawadi kutoka kwa mkuu wa mkoa

Mfanyakazi wa Shirika la umeme akipokea zawadi ya tv nch 32 kwa mkuu wa mkoa