Tuesday 25 July 2017

DC Mkirikiti: Wazazi Waliowapeleka Watoto Unyago Kipindi Hiki Cha Masomo Wachukuliwe Hatua za kali za Kisheria.

 Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mh. Joseph  Mkirikiti amewataka wenyeviti wa Vijiji vilivyopo wilayani Ruangwa kuwachukulia hatua za kisheria watu walio wapeleka watoto wao katika sherehe za unyago wakati shule zimefungiliwa.

Alitoa msisitizo huo baada ya kutembelea shule ya Msingi Makanjiro na kugundua upungufu wa wanafunzi nane wa darasa la 3 ambao wamepelekwa jando  huku masomo yanaendelea mashuleni.

Wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika kata ya Makanjiro yenye vijiji vitano (5), ambavyo ni Chinokole, Chikoko, Mbagara, Makanjiro na Chilangalile.
Mkuu wa Wilaya alisema hapingi suala la wakazi wa Ruangwa kufanya masuala ya unyango, anaruhusu ila yafanyike wakati wa likizo kama anavyowaeleza katika mikutano yake.

“Kila sehemu inamila yake na watu wanatakiwa kuheshimu mila hizo naheshimu mila za wakazi wangu wa Ruangwa ila suala la elimu ni muhimu na nitajitahidi kulifuatilia kwa ukaribu zaid hivyo fanyeni shughuli za unyango wakati wa likizo”alisema, Mhe,Mkirikiti

Aidha wakati wa ziara hiyo Mh.Mkirikiti alisema msimu huu wa korosho atakua makini zaidi na watu ambao wamekuwa na tabia ya kuwaibia wakulima korosho kwani  huwarudisha nyuma wakulima na kuwakatisha tamaa.

“Mwaka jana wizi ulikuwa mkubwa ila tulikuja kungundua hilo mwishoni mwa msimu mwaka huu mwanzo tu wa msimu nitafuatilia kila mahala, mkulima wa korosho hakikisha umeshasajiliwa kwenye daftari la wakulima”alisema Mhe, Mkirikiti.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya Twaha Mpembwene aliwataka wananchi wa kata ya Makanjiro kuishi kwa upendo na watumishi  walio katika kata hiyo kwani wao ndiyo kama wazazi kwao.

Pia aliwataka walimu wa shule ya Sekondari Makanjiro kuwa wavumilivu kwani wao ni watu muhimu katika jamii hiyo na pia Serikali inawategemea katika kuzalisha matokeo mazuri kwa wanafunzi wa shuleni hapo.


MKuu wa wilaya ya Ruangwa akizungumza na wajumbe wa serikali ya Kijiji cha Chinokole kata ya Makanjiro

Moja ya Bustani inayohudumiwa na mradi wa umwagiliaji wa Chinokole


Mkuu wa wilaya akitoa maelekezo ya utunzaji wa Scheme ya umwagiliaji iliyopo katika kijiji cha Chinokole

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mh, Joseph Mkirikiti na Afisa Utumishi wa Wilaya ya Ruangwa Festo Mwangalika wakikagua mradi wa bwawa la umwagiliaji Chinokole


Mkuu wa wilaya ya Ruangwa na Afisa Tawala (aliyevaa miwani) wakizungumza na wavamizi wa eneo la umwagiliaji ambalo wanalitumia kama sehemu ya kufyatulia matofali

Wavamizi wa eneo la mradi wa umwagiliaji kama walivyokutwa wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya Ruangwa wakiendelea na shughuli zao za ufyatuaji wa matofali.

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Chinokole na wataalam waliongozana na Mkuu wa wilaya wakisikiliza maagizo kutoka kwa mkuu wa wilaya kuwa eneo la umwagilijaji ni mali ya jamii.


Mtendaji wa kata ya Makanjiro Mohamed Mamba akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Chinokole kwa Mkuu wa wilaya ya Ruangwa.

wananchi wa kata ya makanjiro wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ruangwa



Afisa Tawala wa Wialaya ya Ruangwa Mh. Twaha Mpembenwe akizungumza na wananchi wa wa kata ya Makanjiro wakati wa ziara yakikazi ya mkuu wa wilaya Ya Ruangwa

Add caption

Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Makanjiro Glory Kiria akimsomea MhMkuu wa wilaya taarifa ya Bima ya Afya ya jamii (CHF)



(kulia) Mh. Diwani wa kaa ya maknjiro na walimu wa shule ya sekondary makanjiro wakiwa wanamsikiliza mkuu wa wilaya ya Ruangwa

walimu wa shule ya sekondari Makanjiro wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake katika shule hiyo.

Wataalam wa Kata ya Makanjiro wakisikiliza maelekezo ya mkuu wa wilaya Mh. Joseph Mkirikiti

wananchi wa kijiji cha chikoko kata ya Makanjiro wakisikiliza hotuba ya mh. mkuu wa wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake

Mh, Joseph MKirikiti akihutubia wananchi wa kijiji cha Chikoko  Kata ya makanjiro wakati wa ziara yake ya kazi (kulia) Afisa Tawala wilaya ya Ruangwa Mh. Twaha Mpembenwe